Ester Matiko: Kama Chama kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari

Ester Matiko: Kama Chama kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari

Rasmi nimejiunga na CCM Milele,, aisee kweli njaa mbaya
 
Mimi naamini kwenye mijadala watatuwakilisha vyema; kwenye kuamua mambo kwa kura ndipo watazidiwa kutokana na uchache wao.

Kama kuna pesa kama nchi itakuja wewe ulitaka tukose hiyo pesa ili hilo pengo lizibwe na nani? Waendelee kukamua wafanyabiashara mpaka tukose ada za watoto wetu?
always mlipia ngoma ndiye huwa anachagua wimbo, usitegemee kina halima kwenda kinyume na aliyewanunua
 
Acha kukariri wewe kwani wale walioanza kukisaliti chama na kuhamia CCM kama nyumbu wanaotafuta malisho walikuwa ni wanawake?

Mbona watu mnapoteza kumbukumbu haraka sana.
Nyumbu huwa hawatunzi kumbukumbu unajisumbua tuu hawaelewi Hawa.
Wamepayuka weeee hawaitambui serikali Mara hawatambui uchaguzi mara haooo bungeni.
 
Anaongea kwa kiburi kwa sababu jana usiku walikutana na meko na spika, meko kawahakikishia kuwa hakuna wa kuwagusa iwe mahakamani ama wapi.. ester atakuwa naibu spika na mdee pia atakuwa naibu spika.imeisha hiooo. dont trust politicians
Ulikuwepo?
 
Nimewalaumu sana hawa kina dada waheshimiwa, baadae nikajaribu kujiweka kwenye nafasi zao nikaona huenda hata mimi ningechukua maamuzi kama yao.

Guys, hebu fikiria ulikuwa kila mwezi kuna mzigo unaingia kwenye account yako alafu gafla zinakata na hauna plan B. Kukaa bila kazi kwa miaka hii sio mchezo. Alafu gafla inakuja ofa ya kuingia kwenye orodha ya wafaidi keki ya taifa, na wanaokupa hiyo ofa wana nguvu, mamlaka na uwezo wa kukulinda unapokula ugali wako. Nafikiri tukiangalia kwa angle hii hatutoendelea kuwalaumu hawa kina dada.

Hebu angalia wenzao waliopita njia hizo; Silinde, Slaa, Mollel, Waitara etc alafu wao wakatae ofa hiyo eti wafe njaa kisa waonekane mashujaa? Tuwe wakweli kizazi cha mashujaa wa hivyo hakipo tena kwa sasa.
Watu wa kwanza kuwahangaikia ni familia yake halafu wanafuata wananchi wasiojulikana.

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
We dada ule udhalilishaji uliofanyiwa na wale Mapolice umeukubali kwa kukisaliti chama kwa kulipwa ujira huu? Kweli dunia ina mambo!!
Ana haki ya kushikwa matako, kumbe in was hovyo. Hao tunawatomasa matako kwenye baa, wanawake Malaya wa fedha ndiyo zao na stahili zao in hizo ikiwemo ya kuruka ukuta
 
Mimi hao wengine wote sina muda nao, nalia na Halima tu mimi.
Halima amekivunja chama kabisa, Halima tulimuamini na kumpa jeshi letu la wanawake na nilitegemea pasi na shaka Mbowe akistaafu uwenyekiti basi kama sio Lissu, Heche basi ni yeye!
I’m disappointed

Taifa kwanza! Haya ya chama na mengine sana sana ni maslahi binafsi.
 
Mimi hao wengine wote sina muda nao, nalia na Halima tu mimi.
Halima amekivunja chama kabisa, Halima tulimuamini na kumpa jeshi letu la wanawake na nilitegemea pasi na shaka Mbowe akistaafu uwenyekiti basi kama sio Lissu, Heche basi ni yeye!
I’m disappointed
🤣🤣🤣🤣
 
Kwa maoni yangu, wananchi tunahitaji watu wa kutusemea Bungeni hata kama ni wachache. Wale wengi wapo upande wa serikali hivyo hawatakuwa upande wetu sana; hawa 20 ni bora waachwe tuu kwani wachache hupewa nafasi kubwa ya kusikilizwa naamini tutawakilishwa vyema.

Hayo mengine yaliyotokea kwa kuwa wanasiasa wengi huubiri suala la KUJIAJIRI ni vizuri NAO wakajiajiri hii miaka mitano.
Wewe umeandika upuuzi mtupu sasa wabunge hawa wameshakula mlungula na keshokutwa wanapewa unaibu waziri kwa maslahi yao binafsi na matumbo yao lakini wamewasaliti Watanzania milioni mangapi waliokuwa wakiungana kuwachangia katika matatizo mbali mbali yaliyowakuta wakiwa na Chadema halfu unakuja na lugha nyepes namna hii hapa jf? unafkiri Halima mdee ana habari tena na watu wa Kawe sijui kigamboni? angalia kina wale Kafulila, Machali, Lowassa, Lipumba, Sumaye, dr slaa, sijuwi Mashinji nk. hawa woote umewahi kusikia wakiikosoa serikali? kila mmoja ni yeye na alichopatana kupewa akaendesha maisha yake.

Hawa kina mdee unafkiri atasema nini bungeni wakati bosi wake ni Magufuli? Ata jambo hili unahitaji darasa la uelewa.
 
Baada ya jana wabunge wa viti maalum kuapishwa, waandishi wa habari walifanikiwa kufanya mahojiano madogo na mbunge mmojawapo, Ester Matiko huku wengine wakigoma. Yafuatayo ni maswali kutoka kwa waandishi na majibu kutoka kwa Ester Matiko.

MWANDISHI: Mmepata baraka za Chama?

MATIKO: Nadhani wote tunajua taratibu za viti maalum mpaka kuweza kufika wabunge kuteuliwa, kuna utaratibu ambao unaendelea ndani ya chama kupitia wings mbalimbali na baadae chama kinabariki na majina yanaenda kwenye tume ya Taifa ya uchaguzi, binafsi nilitaarifiwa nimeteuliwa ndio maana nimefika hapa kuja kuapa.

MWANDISHI: Ulitaarifiwa na katibu?

MATIKO: Na mamlaka husika

MWANDISHI: Lakini katibu wa chama anasema hana taarifa na hilo na watachukua hatua kali dhidi yenu, hili unalizungumziaje?

MATIKO: Sijui zaidi ya hapo, kwa uchache wetu ambao tumekuja hapa, nipende tu kuwaambia watanzania, wategemee makubwa kwetu pamoja na kwamba tuko 19. Tunajua yote yaliyojiri kwenye uchaguzi mkuu ulioisha hadi tukapata hiki kidogo katika ushindi wetu mkubwa tuliokuwa nao.

MWANDISHI: Endapo chama kikiwafuta uanachama, mmejiandaa kuchukua hatua?

MATIKO: Tupo hapa kwa sababu ya chama kwa hiyo kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari.

MWANDISHI: Awali msimamo wa chama chenu ilionekana haukubaliani kuweza nyie kushiriki hapa

MATIKO: Nadhani leo jukumu kubwa ni kuapa na tumetimiza hilo, yanayojiri mengine yote yanawezwa kuzungumzwa kwa wakati muafaka. Katika neno letu la shukrani tumesema dhahiri kabisa tunakishkuru chama cha demokrasia na maendeleo kututeua sisi watu 19 kukiwakilisha katika bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuweza kuwasemea watanzania na chama chetu sasa mengine kama yalijiri yakaenda yakarudi, yatazungumzwa kwa wakati muafaka. Asante.

MWANDISHI: Ndio kusema mmesalimu amri

MATIKO: Sio msemaji wa chama, mimi ni mbunge mteule, ASANTENI SANA.

Uyu matiko hana cha kujibu anatia ulimi puani
 
Mimi hao wengine wote sina muda nao, nalia na Halima tu mimi.
Halima amekivunja chama kabisa, Halima tulimuamini na kumpa jeshi letu la wanawake na nilitegemea pasi na shaka Mbowe akistaafu uwenyekiti basi kama sio Lissu, Heche basi ni yeye!
I’m disappointed
yaan upinzan wa tanzania ni dhaifu na ovyo kabisa kuliko wapinzani wa nchi zote zinazotuzunguka, sasa hawa kina mdee wamekuwa wabunge miaka yote leo hii wanakomalia kwenda kwa nafasi za viti maalum! hizo zilikuwa nafasi za kuwainua wanawake wengine kama vile kina matiko walivyoinuliwa na kufikia hapa, yaan hapa wamepoteza kabisa credibility hawa watu, CCM wanavyosema watatawala milele inawezekana ikawa kweli loh!
 
Ni kama anaulizwa umekula mchana naye anajibu hapana sababu chips na mishikaki kwetu sio chakula.
 
Baada ya jana wabunge wa viti maalum kuapishwa, waandishi wa habari walifanikiwa kufanya mahojiano madogo na mbunge mmojawapo, Ester Matiko huku wengine wakigoma. Yafuatayo ni maswali kutoka kwa waandishi na majibu kutoka kwa Ester Matiko.

MWANDISHI: Mmepata baraka za chama?

MATIKO: Nadhani wote tunajua taratibu za viti maalum mpaka kuweza kufika wabunge kuteuliwa, kuna utaratibu ambao unaendelea ndani ya chama kupitia wings mbalimbali na baadae chama kinabariki na majina yanaenda kwenye tume ya Taifa ya uchaguzi, binafsi nilitaarifiwa nimeteuliwa ndio maana nimefika hapa kuja kuapa.

MWANDISHI: Ulitaarifiwa na katibu?

MATIKO: Na mamlaka husika

MWANDISHI: Lakini katibu wa chama anasema hana taarifa na hilo na watachukua hatua kali dhidi yenu, hili unalizungumziaje?

MATIKO: Sijui zaidi ya hapo, kwa uchache wetu ambao tumekuja hapa, nipende tu kuwaambia watanzania, wategemee makubwa kwetu pamoja na kwamba tuko 19. Tunajua yote yaliyojiri kwenye uchaguzi mkuu ulioisha hadi tukapata hiki kidogo katika ushindi wetu mkubwa tuliokuwa nao.

MWANDISHI: Endapo chama kikiwafuta uanachama, mmejiandaa kuchukua hatua?

MATIKO: Tupo hapa kwa sababu ya chama kwa hiyo kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari.

MWANDISHI: Awali msimamo wa chama chenu ilionekana haukubaliani kuweza nyie kushiriki hapa

MATIKO: Nadhani leo jukumu kubwa ni kuapa na tumetimiza hilo, yanayojiri mengine yote yanawezwa kuzungumzwa kwa wakati muafaka. Katika neno letu la shukrani tumesema dhahiri kabisa tunakishkuru chama cha demokrasia na maendeleo kututeua sisi watu 19 kukiwakilisha katika bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuweza kuwasemea watanzania na chama chetu sasa mengine kama yalijiri yakaenda yakarudi, yatazungumzwa kwa wakati muafaka. Asante.

MWANDISHI: Ndio kusema mmesalimu amri

MATIKO: Sio msemaji wa chama, mimi ni mbunge mteule, ASANTENI SANA.

Very intelligent Mbunge! Wabunge hawa hawachaguliwi kwa kura ngapi kila mmoja amepata kutoka kwenye sanduku la kura bali viti hivi vina utaratibu wa kupatikana ndo maana kila Chama kinapata Namba ya viti tofauti kila Uchagyzi. Baada ya Uchafuzi wa mwaka huu, CHADEMA WAMEPEWA VITI 18 ingawa kwenye sanduku la kura wamepata kiti kimoja tu ambacho kinafanya CHADEMA kuwa na Wabunge 19 Bungeni. Mwandishi angekuwa intelligent kama Mh. Matiko na hatafuti uteuzi kama mstaafu wetu Mayalla (Njaa), labda angehoji kwa nini wao 18 kama ana mashaka na walioapishwa na siyo 18 wengine toka hukohuko CHADEMA anaowafahamu kuwa wangefaa zaidi kuliko hawa. Si Pascal pekee anayetafuta uteuzi kuganga njaa yake bali ni waandishi wote ndo maana sasa hata Media Houses zote zimeungana na TBC kusifu na kuunga mkono juhudi. CHADEMA wako kwenye kikao kuwajadli Wabunge wao hawa tutegemee watatumia busara kuwaacha watuwakilishe!
 
Back
Top Bottom