Ester Matiko: Kama Chama kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari

Bila siasa watakufa njaa.
Mimi naona yaliyopita yashapita na hayawezekani kuyarekebisha. Maana cdm kukaa miaka 5 bila kusikika inaweza poteza umaarufu. Muhimu wapeleke viti maalumu majembe ili wakaendelee kuuwasha Moto bungeni.
 
We dada ule udhalilishaji uliofanyiwa na wale Mapolice umeukubali kwa kukisaliti chama kwa kulipwa ujira huu? Kweli dunia ina mambo!!

Action - reaction. Siamini Mtii wa sheria angeumizwa tu.
 
Matiko Yuko vizuri yeye kaambiwa kateuliwa na mamlaka husika inatosha mamlaka husika ni Mweyekiti wa Chama na NEC katibu mkuu kazi yake kuandika Minute tu za vikao vikivyoitishwa na mwenyekiti akijisikia kuitisha

Si kila kitu katibu lazima ashirikishwe
 
We dada ule udhalilishaji uliofanyiwa na wale Mapolice umeukubali kwa kukisaliti chama kwa kulipwa ujira huu? Kweli dunia ina mambo!!
Hivi mnadhani wanasiasa wana-survive kwa kula hewa?
 
Wasaliti ni ninyi wananchi....Hahahahaaa

Sasa mlitaka wafanyaje? Ninyi mnasema kura ziliibwa... Wakawaita mwende barabarani mkaandamane hamkuwaunga mkono... Mnataka nini sasa???

Eti oooo wasaliti??? Wasaliti ni nyinyiiii....
 
Kumbukeni hao mabinti bado wadogo, hawajui biashara, wakikaa mtaani watafanya nini?
 
Sio maoni yako. Kazi ya mbunge ni kuwasemea na kuwasilisha kero za wananchi, awe CCM au Upinzani. Kwa hiyo hakuna huyu ni wa wananchi na huyu si wa wananchi tofauti ni uwasilishaji tu. Wengine wanaongea uhalisia, wambeya na wako wakuongeza chumvi.
 
Sio maoni yako. Kazi ya mbunge ni kuwasemea na kuwasilisha kero za wananchi, awe CCM au Upinzani. Kwa hiyo hakuna huyu ni wa wananchi na huyu si wa wananchi tofauti ni uwasilishaji tu. Wengine wanaongea uhalisia, wambeya na wako wakuongeza chumvi.
Sheria kandamizi zinapitaje Bungeni na tuna wa kutusemea?
 
Sheria kandamizi zinapitaje Bungeni na tuna wa kutusemea?
Hakuna sheria kandamizi, sheria inatungwa kudhibiti uharifu. Una uhuru wa kutoa mawazo sio uhuru wa kutukana na kutoa uongo kuzua taharuki. Una uhuru wa kutoa taarifa zilizohakikiwa sio za kuzua. WAJIBIKA hakuna atakaye kugusa.
 
Siku Shangazi nae akija kuunga juhudi napo pia utajolaumu kukosa fursa maana nae si alifanyiwa hivyo hivyo na polisi.
 
Ujue watu wa humu Jf wanashanaza sana,wao hawajulikani humu maisha yao yakoje usikute nao wanakula keki ya taifa kwa namna yao ila wakija humu ndio wanawaambia wenzao wanajali matumbo sijui ni wasaliti,wakati wao ukiwaambia waingia road wafanye maandamano hawatoki wamejificha tu mitandaoni wao zao kuongea tu.
 
Hii mechi kacheza Mbowe na Mnyika ata Lissu hii chenga amebaki kajishika kiuna
Lissu mwenyewe baada ya maji kumfika shingoni alisema anataka maridhiano na serikali, kwa taarifa yenu hayo ndo maridhiano. Hii ishu ya kukubali kupeleka viti maalum bungeni ni kwamba wameshirikiana wote mbowe, lissu na mnyika, sema wanataka waipotezee kwa wananchi ili wasiaibike, ndo kina mnyika wanajifanya hawajui wala hawana taarifa kuhusu hilo. Wanasiasa wahuni sana, wanaweza kuwasababishia watu wakapigana vita mwisho wa siku wanakutana kwa pamoja meza ya bata na kugonga cheears. Sema nini?, watanzania wajanja wanajitambua walikataa kuingizwa kwenye maandamano kwasababu walisha tambua hilo zamani. Cha msingi serikali iliyopo ipambanie maendeleo kwa kila raia na nchi kiujumla.
 
Njaa mbaya sana..
 
Huu ni udhalilishaji wa wanawake.. kwamba wanawake hawana misimamo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…