Ethiopia inaenda kuvunjika kama Yugoslavia

Uko sahihi kabisa mkuu, kwa jamii zetu za Africa ni rahisi sana kupata madaraka kwa kutumia kete ya kikabila au dini na unaweza kufanikiwa sana kwa njia hiyo na ukakaa madarakani kwa raha zote na utajihisi tena hakuna kama wewe.

Ila siku ukianguka basi anguko lako litakuwa kubwa Sana.
 
👍👍
 
Serikali ya majimbo ni hatari sana kwa muungano wa kitaifa, CHADEMA 2020 ndio walikuwa sera yao hiyo ya kuunda serikali ya majimbo, kitu ambacho ni hatari sana, tunaona jinsi Ethiopia wakipambana na jimbo la Tigray, kwani Jimbo la Tigray lina Rais wake, jeshi na kila kitu kama serikali ilivyo, sasa inapambana na serikali kuu, yaani Federal Government..!!
 
Kabla utumwa haujapigwa marufuku ethiopia. Hao wa kaskazini (watigray na Amhara) walikuwa wakifanya hawa wa kusini , weusiweusi, waoromo kama watumwa. Na Ethiopia wamechelewa sana kukomesha utumwa, mwaka 1931.
Hii imekaa kama ya wenzetu Hutu na Tutsi uhasana kama huu unagawa nchi
 
Hao ni makabila tena hasimu toka enzi na enz hawakubali kabila jingine kutawala..wanaviziana asiye na madaraka anataka kupokonya mwenzake...sio majimbo
 
USA nayo ni federal government iko mbali kimaendeleo kichizi. Wafrika ujinga wao ni kufikiria negativity tu. Yaani ukimpa glass ya maji nusu yeye atakwambia Half empty glass badala ya Half full glass.
 
Mkuu agiza chochote nakuja kulipa...umemjibu vizur sana huyo shwain[emoji35]
 
Kwani Chadema walisema kila jimbo litakua na Rais wake na jeshi lake?

Au mmeamua kuitumia Ethiopia kama mfano ili kuendeleza propaganda zenu?
 
Wewe ndo umeleta mwanga kwenye hii habari at final point chanzo cha hi vita inayoendelea sasa hivi.
 
Najiso Ethiopia mwenye mamalaka ni Waziri mkuu
 
USA nayo ni federal government iko mbali kimaendeleo kichizi. Wafrika ujinga wao ni kufikiria negativity tu. Yaani ukimpa glass ya maji nusu yeye atakwambia Half empty glass badala ya Half full glass.
USA ni federal hata Urusi pia ni federal ila hazina migogoro hata Nigeria pia ni federal sema udini,ukabila na ufisadi uliokithiri ndio unawagharimu.

Fatilia hata China angalia namna utawala wao ulivyo utagundua hakuna huu mtindo wa kila kitu kuhodhiwa na serikali kuu.

Tatizo huku Tz watawala wana hofu ya kupoteza madaraka na ulaji hivyo wanatumia propaganda kuupiga vita na kuupaka matope huu mfumo wa wa serikali za majimbo.

Mbaya zaidi na raia wengi hawapendi kusoma na kutafiti hivyo wanadanganyika kirahisi na propaganda za watawala na wapambe wao.
 
Ndo maana kuna kipindi kulitokea machafuko Oromia hawataki ardhi yao ichukuliwe wakat wa kutanua jiji la Adis Ababa. Na kweli serekali ilisalimu amri
 
Ndo maana kuna kipindi kulitokea machafuko Oromia hawataki ardhi yao ichukuliwe wakat wa kutanua jiji la Adis Ababa. Na kweli serekali ilisalimu amri
Ni wakati ule wanajenga zile appartments za kuuzia wananchi (condominiums) eenh?
 
Na watutsi na wahutu Wana laana ya kikristo??
Kimsingi wale walichonganishwa na Mfaransa na habari yao ilishaisha, ila migogoro penye waislam wengi haiishi...hata kama wanaishi wenyewe
 
Hii ndio safi sana. Lazima wanaume wachapane ili adabu iwepo.

Mambo ya kuburuzwa kama kondoo halafu unaambiwa tunza amani, ni mambo ya kipuuzi.

Dunia sio lelemama. It is survival for the fittest.

Mnabembelezana kama makondoo ati oooh "amani ya nchi" huku mafisi yanatumbua keki ya Taifa.
 
Kimsingi wale walichonganishwa na Mfaransa na habari yao ilishaisha, ila migogoro penye waislam wengi haiishi...hata kama wanaishi wenyewe
Ethiopia kuna waislam wengi eenh? Hebu tupe source ya hiyo taarifa yako. Hebu kuwa realistic uweke mbali chuki zako dhidi ya hao waislam.

Kwa experience yangu ya ethiopia naona kama majority ni Orthodox christians wakifuatiwa kwa karibu na waislam. Sasa sijui wewe unataarifa zipi?
 
mi nadhani shida kubwa ni hao wa Tigray waliozoea kukalia madaraka na kujipatia mali, sasa wanaona wanaonewa.
Hii mbona inakuja kuwa sawa kabisa na hapa kwetu tz kuna watu Fulani wao walijiona kuwa ndo wamesoma na wanastahili kutawala.JP hakuteua hata waziri mmoja wakaleta mjadala kuwa JP ana shida gani na tigray mana hajatupa waziri mmoja jamani.
So saivi wanajiona kama wanaonewa ila enzi zao walijiona wao ndo wajanja wamesoma Kumbe walipewa madaraka afu wakafanya ofisi za serikali kama za familia zao.
Sie Wa promo, Amhara na huku sudani kusini Wa fugaji tu Wa ng'ombe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…