Ethiopia inaenda kuvunjika kama Yugoslavia

Ethiopia inaenda kuvunjika kama Yugoslavia

Wagweno si kama wachagga chunguza utagundua
Kwa wapare kuna wagweno......nasikia hata mila zao kidogo ni tofauti na za wapare wengine hao ndo nasikia walitokea Ethiopia maana wana tamaduni nyingine ambazo ni tofauti kdg na za wapare wabantu
 
Duuuh....taifa lina "ukabila" Hilo...

Yaani pamoja na kuwa hawamsupport Abiy,ila kwenye "mtanange" wamekaa Upande wake....😂😂

Mwalimu Nyerere ALIONA MBALI SANAA....

May His Soul Rest In Peace aamen aaamen.
Kabisa! Na kinachombeba Abbiy ni zaidi wa Amhara na waoromo wachache. Maana wazazi wake Baba ni Muoromo na mama ni Amhara. Hivyo anaushawishi kutoka kwa makabila yote mawili ingawa waoromo walitegemea favor zaidi kutoka kwake hivyo kama wanakinyongo fulani hivi.

Cha kufurahisha kwenye hili la kuwachapa Tigray waoromo wamemuungamkono na wanamgambo wakioromo wapo tayari kwenda front line kuzichapa.
 
Wako vizuri wale na umoja. Makabila mengine wivu tu. Ila Abiy angechelewa tu kidogo tu sasa kungekuwa na taifa la Tigray. Amhara wamemsaidia sana jamaa. Nembo ya Tigray na bendera hapi chini
...bora kawawahi...maana ni mwanajeshi huyo!!!

Halafu Kuna kipindi BATTALION ya jeshi ilikwenda kumvamia ikulu...akawatuliza...je nao walikuwa wanaongozwa na hayo ya UKABILA Jeshini?!!!!
 
Duuuh....taifa lina "ukabila" Hilo...

Yaani pamoja na kuwa hawamsupport Abiy,ila kwenye "mtanange" wamekaa Upande wake....😂😂

Mwalimu Nyerere ALIONA MBALI SANAA....

May His Soul Rest In Peace aamen aaamen.
Kwakweli japokuwa alikuwa na mabaya mengi tu lakini kwenye hili la kuthibiti ukabila mwalimu Nyerere kwakweli alifanya la maana sana
 
Yugoslavia ilivunjika na kutoa Mataifa kutokana na makabila, naona Ethiopia ikienda mlengo huo.

Ethiopia ina makabila makuu manne.

Oromo ndiyo kubwa kama 35 asilimia wanafuata Amhara asilimia 30, Tigray asilimia 6 na wasomali asilimia 6.

Hawa wengi wanaishi kwenye majimbo yao ambayo yana Rais na jeshi lao. Miaka ya mwanzoni mwa 90 watigray japo wachache waliangusha utawala wakijamaa nakuongoza nchi hadi alipokuja waziri mkuu wa sasa ambaye ni muoromo mwaka 2017.

Waoromo walinyanyaswa sana kipindi cha utawala wa watigray. Kwahiyo na sasa watigray wanaona kama wannyanyaswa.

Kimsingi Ethiopia kuna machafuko na vita ya kikabila. Ethiopia inaweza kusambaratika?
1605546681652.png
1605547320590.png
 
Kwasababu yeye anataka eti kui-unify Ethiopia iwe kitu kimoja, yaani waoromo wasahau yaliyopita wagange yajayo. Waoromo walinyanyasika sana kipiti watigray wapo madarakani, Tigrayans na Amhara walikuwa wanawatreat kama seconda class citizens waoromo. Sasa alioingia Abbiy jamaa wakajua ndiyo muda wao sasa wa kulipa kisasi halafu yeye akawakata stimu kwamba wagange yajayo.

Huyo Jawara Muhammed amewaahidi akishika nchi hadi Addis ababa atairudisha kwa waoromo. (Kijiographia Addis ababa ipo Oromia region)
Hatareee....

Kwangu Abiy Ahmed ni "kiona" mbali...
Abiy anafuata siasa za "mandela" japo hazifanani na " hayo"😂

Ni mtazamo tu....kwa wale wenye mitazamo ya kila mtu "ashike chake" kama ilivyotokea kwa SUDAN KUSINI na UINGEREZA kutoka EU,ama Polisario kuachana na Morocco basi ABIY AHMED ni kizingiti....

Ila kwa sisi tunaotaka unification (japo Kuna kipindi ni ngumu) kama mwalimu Nyerere basi ABIY AHMED ni HERO HASWAAA....
 
Bora ungekaa kimya tu kuliko kukurupuka! Huu ugomvi wa Ethiopia hakuna Msomali anayehusika hata kidogo. Yaani kwenye siasa za Ethiopia hawa wasomali wa Ethiopia hawapo kabisa na wala huwa hawajioni kama wao ni waethiopia wanajiita wasomali. Abbiy Ahmed japokuwa ni mu-oromo (Kabila lenye waislam wengi) lakini yeye ni Mpentekoste na Tigray majority kama sio wote ni wakristo wa madhehebu ya Orthodox.

Hapo Msomali na Uislam umeingiaje?
Mkuu ulipotelea wapi. Kipindi sijajiunga JF nilikuwa nakuona sana humu sikuhizi kulikoni
 
Tigray ni wachache ila wananguvu sana na Mali. Na ndio hao walimng'oa dikteta Mengistu Haile Mariam. Tigray wapo hadi Eritrea na wanaongea lugha moja Tigrinia japo mipaka tu na siasa imewatenganisha.

Rais wa Eritrea Isias alikulia na kusomea Addis Ababa akarudi Eritrea na kuanza siasa zake chafu.

Melez Zinawi aliingoza TPLF na akaleta maendeleo sana Ethiopia.

Wasomali wa Ethiopia wako jimbo la ogaden wenyewe wanjiona hawako Ethiopia. Djibouti ni Wasomali hawajawahi kuwa Ethiopia.

Cha kushangaza wote hao Ethiopian hawawezi kujitofautisha kwa sura wanakuja kujitofautisha na kujua flani katoka kabila flan wanapoongea.

Queen sheba (Sabaah) kipenzi cha mfalme Suleiman alitokea Tigray.

Pia kuna makabila mengi madogo madogo kusini mwa Ethiopia 'Southern nations' omo river valley kama gurage, Hamar.

Nilishaletaga Uzi humu miaka ya nyuma kuhusu uhasama wa makabila ya Ethiopia kwenye id yangu pendwa iliyopigwa life ban copen hagen DN
Kumbe wewe ndio Coppenhagen DN?
 
Kwa mustakabali waethiopia Abbiy Ahmed inabidi abaki madarakani. Jamaa yupo focused sana na uchumi wa Ethiopia utapaa zaidi chini ya huyu mtu. Kwasasa hadi ameanza ku-attract foreign investment na anamipango kabambe ya kubadilisha sera za kiuchumi za ethiopia ikiwepo kuruhusu biashara huria kutoka kwenye kila kitu kushikiliwa na serikali. Mimi naona angegeuka tu dikteta kama Zenawi ili aifikishe nchi mbali, hizi demokrasia anazotaka kuziweka kwenye nchi ya wakorofi haitawezekana
Oooo....

Demokrasia ni mfumo mzuri na bora ilioje kwa "wastaarabu" si "Walugaluga".....

Ndio mana BARA ARABU wanapata shida sana kwa kulazimishiwa mfumo "alien"....

Sasa ona kichekesho,nchi Kama Lebanon ambayo kidogo ina values za nchi za kimagharibi(wafaransa) lakini bado NGOMA mbichi.......

So Abiy Ahmed ajitahidi kubalance....aendelee kuihuisha DEMOKRASIA kidogodo....ajenge nchi kimkakati...ila WAKOROFI asiwaonee "SONI"....

Naona Jawar ameshapigwa kesi ya TREASON na TERRORISM loooh pagumu hapo...
 
Nguseroh unakosea kuwapendelea Watigray kisa eti "ni wazuri na smart". Ethnicity yeyote inayoleta ujuaji huwa siikubali kabisa na Abiy namuunga mkono sana.

Hizi jamii za Ethiopia pamoja na ugumu wake zinatakiwa ziisikilize Federal government. Vita ilitakiwa iwepo zamani pale jamii zilipoanza kumiliki majeshi, hakuna jambo la maana linatokea kila mmoja akiwa na jeshi lake.

Abiy namuunga mkono sana ila nina wasiwasi na Egypt kama haihusiki kwa siri. Kuna uzi nilichangia nikasema Egypt hawezi jiangaisha kupigana na Ethiopia wakati kuna ethnicity. Anatoa fedha Na silaha tu anatumia gharama kidogo na anakaa na majeshi yake kwake.

Naona tutakuwa na vita kama Biafra
 
Hawa ndugu zetu wenye asili na nywele za kikemikali na pua ndefu kidogo wanajionaga class fulani hivi, acha wanyooshane tu mpaka watakapopata akili.
😂😂
Mkuu binadamu wenzako hao....ha ha ha waache na hulka zao...
Tumeumbwa tofauti...
Tuna experience tofauti....

Yaap ndio hivyo wanachapana tena
 
Namfahamu sana Muhammed Jawar! Alipotua Addis ababa mji ulisimama, nilikuwepo Addis wakati jamaa anarudi Ethiopia kutokea Marekani. Wa-Oromo wanamuona ndiye muokozi wao baada ya Abbiy Ahmed kugoma kuwapa upendeleo waoromo wenzake. Huyu Jawar ni threat sana kwa Abbiy ndiyo maana kila siku anapigwa kesi na kurundikwa jela kama viongozi wa CHADEMA(Joke).
Huyu alipaswa aungana na Abiyy ili atumie ushawishi wake kuiunganisha nchi ila jamaa anatumia kete ya ukabila kusaka madaraka.
 
Huyu alipaswa aungana na Abiyy ili atumie ushawishi wake kuiunganisha nchi ila jamaa anatumia kete ya ukabila kusaka madaraka.
Nimewaza Kama WEWE...huyo JAWAD ni mkabila sana tu.....

Halafu ukabila wake unaonekana kwani yeye ni PURE Oromia ila Abiy Ahmed ni chotara(Oromo+Amhara).

Ukabila ni kitu KIBAYA MNO....
Ukiukumbatia kipindi fulani ujue kitakuja KIPINDI nguvu hizo ZITAPOTEA....angalia TIGRINYA kwa miaka mingi walivyokuwa WANATAMBA chini ya Zenawi....leo NGUVU ile imewandoka....WANAITAFUTA TENA my foot....

Rip Baba wa Taifa JKN,aaamen aaaamen!!
 
Back
Top Bottom