Kwa hiyo unaamini kabisa wa kimtoa ndio mambo yatakuwa shwari? nchi haitatawalika watapigana miaka haya mambo sio kuyaongelea ki wepesi hivi. ziko sababu haya yametokea, huwezi kuna jimbo lina kikundi cha wapiganaji. Sasa hiyo mifano unayotolea yakitokea kwetu wakaja watu kusema tumepokonywa vyeo tuna njaa utaruhusu haya yatokee nchi yako? Leo wasukuma wakisema tumepokonywa vyeo sasa tunapigana utegemee serikali itakaa kimya. Haya ya Ethiopia ni mwanzo wa majanga ya muda mrefu sana yakiachwa yaendelee. shida za binadamu hatujifunzi kwenye makosa. Libya walisema kama haya upande mmoja unawaonea upande mwingine kila kitu Tripoli wakaungana wakamtoa Gaddafi, leo wana nini yale yale Tripoli wana Rais na Benghazi wana rais hakuna lolote walilofanya zaidi ya kuigawa nchi, lengo lao waliungana wakamtoa Gaddafi na walikuwa wanasema hivi hivi Tripoli wanatuonea kila kitu wao. Ethiopia itakuwa zaidi ya Libya kukosekana amani Ethiopia kutaleta athari mpaka nchi zetu za E. Africa. Tushangilie leo kesho tutakumbuka haya. South Sudan walifanya nini? wakamtoa wasiyemtaka wakaanza kumalizana wenyewe.