Eti hawa ni wapiga kura 2020, nimesikitika sana!

Usicheke ndugu yangu!!
Itatuchukua vizazi vitano mpaka haya mazalia ya ujinga wa CCM yaishe. Nyerere alikuwa mtu mkali ila alitupa elimu ambayo ilitusaidia. Alipofanya makosa ya kutaifisha shule za makanisa tukaanza ujinga na ukaanza kuenea ndo baadaye akaleta UPE ikavuruga kila kitu. Wenzake wakaja na mitaala ya ajabu kama ya Mungai aliyevuruga wizara. Wakaja na shule za kata za Kayumba na tunaona vinavyoyumba.
 
Ndege na SGR ni muhimu sana kuliko elimu ya hawa watu na watoto wao,sasa hiyo reli na ndege zitasafirisha nini wakati wanaojengewa na kuletewa dreamliner ndio hawa-anaejua jibu la swali hilo ni Magufuli tu
 
Upuuzi mtupu
 
Inasikitisha na kuumiza sana!
Kwangu lililonisikitisha na kuniumiza ni kwamba tuna watu wakitazama video kama hiyo wanaishia kucheka. Naamini mtu anayecheka ujinga wake ni maradufu tena ujinga wake ni wa hatari kwa taifa kuliko hata hao anaowacheka. Hao ndio mtaji wa CCM katika uchaguzi.
 
Hii video ni tamthilia/mchezo wa kuigiza au ni hali halisi?
Siyo Tamthiliya wala mchezo wa kuigiza ndugu yangu huo ni uhalisia na kama anavyosema Mag3 hilo siyo jambo la kucheka hata kidogo bali ni kitu cha kututafakarisha na kusababisha tuchuke hatua dhidi ya hali hiyo!!
 

Mzee hapa sio suala la dharau. Hali hii kiukweli inasikitisha sana, hii inaonyesha ni jinsi gani kama taifa tuna safari ndefu sana
 
haaaa haaaaa Leo nmecheka Hadi machozi upinzani kwenda kijijini ni kupoteza pesa
 
Oh my goodness. Jamani jamani tunashida yaani. Na changamoto kubwa ni kwamba hawa ulizwi wana malengo gani na watoto hawo. Maendeleo gani haya jamani. Ndugu zake wa mjini wata koma kweli
 
3:04 Baba anapotoa kicheko cha kujiamini daah! Nimecheka sana

Sasa hebu fikiria hiyo familia ipewe Khanga moja kofia mbili na tishet za kijani mbili saa kumi ya usiku wanajipanga kwenye msitari wa Kura.
Sasa mtu kama huyo apewe ofisi ya juu ya serikali si lazima watu wapotee kama mbuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…