Eti ma-senior wenzangu katika kilele chao kati ya Ray-C na Lady Jay Dee, nani alikuwa bora kuzidi mwenzie?

Eti ma-senior wenzangu katika kilele chao kati ya Ray-C na Lady Jay Dee, nani alikuwa bora kuzidi mwenzie?

Ray C alizidiwa kiuno hadi na Fifi Moto bwana. Taji lake lilikuwa hatarini kama Fifi angeamua kudumu humo.
Jide mlia machozi alikuwa ndio SI unit ya muziki wa bongo kwa wanawake. Wimbo wa kwanza tu akaenda kutumbuiza na Kora Awards huko Kusini mwa Afrika.
Yaliyokuja baada ya hapo ni kisanga.
Alipambana na kila aina ya presha ya wadau wa muziki bongo, kwanini nisimuite Komando?
Aliwaweka mbali zaidi washindani wake kwa Distance kubwa sana kwa kuchanganya Lugha za neno Nakupenda kutoka mataifa mbalimbali.
Tukamuita Mama Some Food nae hakutuacha tuzubae kwa kutufungulia mgahawa, nahisi ndio alikuwa msanii wa kwanza kuwa na biashara inayoonekana na kuwa na maana.
Tumesahau hata aliponunua prado? Na baadae akaja kumuuzia produza Lamar. Ikafikia hatua Marehemu Ngwair akaimba kwenye ngoma yake "Sikiliza" akiwahusia mabinti kuhusu kumiliki Prado kama Lady Jay Dee?
Huyu Mkurya atanimalizia wino kwa kuandika.
Maua yake hayatoshi hata niseme niyanunue kwa gharama za pesa zote zilizoko B.O.T
 
Ray C kadumu kwenye game kwa muda mfupi zaidi ya Jide, lakini ndani ya muda huo mfupi alifika kwenye peak ya juu sana ambayo Jide hajawahi kufikia
Peak gani hiyo ya juu ambayo Rac alikua na jide hajawahi kufika hadi leo??

NB. Kinachojadiliwa sio uzuri na uno feni.
 
Peak gani hiyo ya juu ambayo Rac alikua na jide hajawahi kufika hadi leo??

NB. Kinachojadiliwa sio uzuri na uno feni.
Mkuu Juma Nature ndiye rapa aliyefikia peak ya juu kabisa kuliko Rapa yeyote yule Bongo ingawaje wapo Marapa wengi sana bora kuliko yeye

Mr Nice ni Diamond ndio anaweza kuwa amepita peak aliyofikia Mr Nice enzi hizo

Hakuna mwanamuziki wa kike alifikia peak ya Ray C ingawaje kuna wasanii wengi sana wa kike bora kuliko yeye

Kuna wanamuziki wanaweza kutoa album moja tu au hata wimbo mmoja tu ukavuma sana na kufikia viwango vya juu sana lakini wakashindwa ku maintain ubora wao
 
Ukiondoa mwonekano ambao pia ni moja ya sifa za kufanikisha kazi za Sanaa, uimbaji wa Ray C ni kawaida mno...

Silaha ya Lady JD ni kipaji halisi cha kuimba ambacho hakihitaji Autotunes ndo maana hata leo hii bado yupo yupo sana...
 
unarudia nyuzi. walishawahi kupambanishwa kitambo ungetafuta uzi usingejkuja kutusumbua.
kwa akili yako ray c amfunike jide? utakua unaota motoni. jide ni moto wa nyika hauzimwi kizembe
 
Back
Top Bottom