Eti Mbowe alitoa laki 6 kufadhili ugaidi. Seriously?

Eti Mbowe alitoa laki 6 kufadhili ugaidi. Seriously?

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Kabla ya Mbowe kusomewa mashtaka, watu waliipa Jamhuri "benefit of doubt" kwamba huenda ina ushahidi wa maana. Watu wakahisi labda Mbowe ana uhusiano na makundi ya kigaidi kama Al Shabab, Al Queda, Boko Haram etc na pengine anapeleka vijana huko kwa ajili ya mafunzo.

Hayo ndio yalikua matarajio ya wengi. Hata Kigogo alisema subirini asomewe mashtaka mtashangaa. Dada yetu wa Marekani nae akasema ameelezwa mambo mazito kuhusu tuhuma za Mbowe na ugaidi.

Lakini kilichotokea leo ni tofauti na matarajio ya wengi. Eti Mbowe alitoa laki 6 kufadhili ugaidi. Seriously? Huu ndio ule ushahidi mzito tuliokua tunaungojea? Hiki ndio kile ambacho Mama aliiambia dunia kwamba Mbowe alifadhili ugaidi halafu akatoroka nchi? Yani alifadhili ugaidi kwa laki 6 halafu akakimbia?🤣.

Kama ugaidi unaweza kufadhiliwa kwa laki 6, basi nchi yetu ingekua na vikundi mengi sana ya kigaidi. Kwa mujibu wa ripoti ya BBC ya December mwaka jana, Kundi la Al Shabab linakusanya zaidi ya $180M kama kodi kutoka kwa raia wa Somalia. Hizo ni sawa na TZS Bilioni 400. Pia wanapata ufadhili kutoka taasisi mbalimbali unaokadiriwa kufikia $900M kwa mwaka sawa na TZS 2.2 Trilioni.

Kwahiyo bajeti ya Al Shabab kwa mwaka ni zaidi ya TZS Trilioni 3. Hicho ni kikundi cha kigaidi ambacho kiko hapo Somalia. Lakini Tanzania tuna kikundi cha kigaidi cha Mbowe chenye bajeti ya laki 6 kwa mwaka. Funny but not funny.

Mashtaka ya leo yameonesha huenda serikali haikujipanga na kesi hii, na yamezidisha mashaka ya wale waliokua wakisema Mbowe amekamatwa kwa sababu za kisiasa ikiwemo kudai katiba mpya. Watu walitegemea hati ya mashtaka iliyosheheni "serious offence" za ugaidi, sio hiki kilichopelekwa mahakamani leo. Hata CCM wenyewe wamepigwa butwaa kusikia hizi tuhuma za Mbowe kufadhili ugaidi kwa laki 6.

Pia tuhuma za kutaka kuchoma vituo vya mafuta ni kituko kingine. Kama Mbowe alikua na "roho mbaya" kiasi hicho basi angepanga kuchoma vituo vya mafuta baada ya matokeo ya uchaguzi 2015, kwa sababu wananchi walikua tayari kwa lolote. Lakini akatumia hekima kuwatuliza. Akaonekana muoga lakini hekima ikamuongoza, kuhakikisha hakuna hata mtu mmoja anajeruhiwa kwa sababu ya uchaguzi.

Sasa kama aliweza kutiza watu waliokua kwenye "tention" kubwa kiasi kile akafanikiwa, angewezaje kupanga kuchoma moto vituo vya mafuta kwa sababu ya Sabaya? Halafu akishachoma yeye ndio anakuwa Mkuu mpya wa wilaya ya Hai? What a crap?

Pia tuhuma za kupanga kumuua Sabaya nazo zina ombwe. Askofu mmoja leo amesema Mbowe hawezi kupanga kumuua Sabaya, lakini Sabaya anaweza kupanga kumuua Mbowe. Ushahidi wa kimazingira unaonesha hivyo.

Sabaya amewahi kuvamia hotel moja ya kitalii akiwa na bunduki, akataka kuoneshwa chumba alicholala mwanamuziki mmoja wa bongoflava ili aende kumbaka. Walinzi wakakataa kumuonesha. Akiwa na mabaunsa wake wakawapiga wale walizi na kuwalaza rumande. Tukio hilo lilirekodiwa kwa CCTV camera za hoteli hiyo lakini wala hakujali.

Sabaya amewahi kutumia magari binafsi akayapachika namba za umoja wa mataifa kisha akaenda kufanya nayo uhalifu, bila kujali kwamba anaharibu diplomasia yetu kimataifa. Sabaya amewahi kumvamia diwani mmoja huko Machame na kutembeza kipigo kwa familia nzima, kisha akamkata sikio mtoto wa diwani huyo.

Sasa jiulize kati ya Sabaya mwenye rekodi za ukatili kiasi hiki, na Mbowe mwenye rekodi za kutumia hekima kutuliza "tention" za watu, nani anaweza kupanga kumuua mwenzie? Kusema Mbowe alipanga kumuua Sabaya ni sawa na kusema Papa Francis anapanga kumteka kiongozi wa Boko Haram. Future imposible tense.

Halafu kumbuka Sabaya ndiye aliyetoa tuhuma hizi za kutaka kuuawa. Watu wanauliza je kuna uhusiano gani kati ya Sabaya na Jamhuri kwenye kesi ya Mbowe?

Kwanini kesi ya Sabaya inaendeshwa kwa kasi sana? Mwanzoni ilikua inasikilizwa baada ya wiki mbili, lakini kwa sasa inasikilizwa kila siku? Kuna watuhumiwa wangapi ambao ushahidi umekamilika lakini kesi zao hazipelekwi kwa kasi kama ya Sabaya? Kwanini Hakimu alibadilishwa? Kwanini tuhuma za Sabaya kwa Mbowe zinapewa uzito sana kwa sasa?

Halafu kwa mujibu wa sheria ya ugaidi no.21 ya mwaka 2002, kifungu cha 4 ugaidi unahusisha halaiki ya watu sio mtu mmoja. Yani ukiua mtu mmoja hayo ni mauaji na utashtakiwa kwa maujai (murder), lakini ukiua halaiki ya watu huo ni ugaidi na utashtakiwa kwa ugaidi (terrorism). Sasa imekuaje tuhuma za kupanga kumuua Sabaya (mtu mmoja) ziitwe ugaidi?

Mimi nadhani Rais Samia amshauri DPP kuiondoa hii kesi mahakamani. Wala haitakua kuingilia uhuru wa mahakama. Rais Samia aliwahi kumshauri DPP kaziondoa mahakamani kesi za "kubambikia" na wala hakuonekana anaingilia uhuru wa mahakama. So anaweza kushauri kwa hii ya Mbowe pia.

Hii ni kwa sababu kesi hii inachafua sana serikali ya Samia, kitaifa na kimataifa. Kesi hii imemuondolea heshima yote aliyoijenga kwa siku 100 za kwanza. Hata wawekezaji watapungua kwa sababu hakuna mtu atakayekua tayari kurisk mtaji wake kuwekeza nchi yenye ugaidi. Hata wafadhili watapunguza misaada kwa sababu hakuna mtu anataka kufadhili nchi yenye ugaidi.

Kwahiyo Rais Samia anaweza kumshauri DPP kuifuta hii kesi kwa maslahi mapana ya serikali yake, maslahi mapana ya nchi yetu, na maslahi mapana ya demokrasia nchini.

Na hatakua wa kwanza kufanya hivyo. Mwaka 1970 Bibi Titi Mohamed na wenzake walifungwa gerezani kifungo cha maisha kwa tuhuma za uhaini. Kumbuka Bibi Titi ni mmoja wa watu waliopigania uhuru wa nchi hii, na ni Waziri wa kwanza mwanamke.

Watu wenye hekima wakamfuata Mwalimu Nyerere na kumwambia, athari za kumfunga bibi Titi ni kubwa kuliko za kumuachia huru. Kumuweka jela kunaiharibia zaidi serikali yako. Ukimuachia huru atakayefaidika zaidi ni wewe na serikali yako sio yeye. Nyerere akaelewa na mwaka 1971 akamuachia huru.

The same applies kwa kesi ya Mbowe. Ikiwa DPP ataamua kuifuta hii kesi, atakayenufaika zaidi ni Samia na serikali yake, si Mbowe wala Chadema.

Hata hivyo Samia ana uhuru wa kusuka au kunyoa. Kesi iendelee kusikilizwa na yeye aendelee kuchafuka na kujifungia fursa za wawekezaji (hata kama Mbowe atashinda) au amshauri DPP kuifuta kesi, apate heshima ya kufanya maridhiano ya kisiasa, na historia imkumbuke kama mama shujaa wa demokrasia. Kupanga ni kuchagua.!
 
Prosecution na defense wajifue tu tupate kufurahia uhondo. The rest judge atakavyohukumu so be it.
 
Gaidi alitaka kuchoma vituo vya mafuta tokea mwaka jana, wakamuacha tu azurure mwaka mzima. Leo tunaambiwa amefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya uhujumu uchumi.

Haina tofauti na kesi ya Mdude Nyang'ali kushtakiwa kwa kusafirisha madawa ya kulevya kutokea pakistani mpaka mbeya, mtu anaeshtakiwa hajawahi kupanda ndege hata za ATCL wala hajawahi kumiliki hata passport wala kitambulisho cha NIDA. Sijui alisafirisha kwa kutumia ungo!!!

Kinacho nishangaza,

● Gaidi ni mtu hatari kwa taifa, kwanini aliachwa mwaka mzima anazurura na kupiga misele??? Aliachwa ili atimize malengo yake ya ugaidi halafu jeshi la polisi lifurahi na lifanye sherehe?

● Kuachwa kwakwe mwaka mzima huru, si angefanya mashambulizi mengine ya kigaidi kama angekua gaidi baada ya kuona la vituo vya mafuta kufeli. Hii ya kumwachia huru gaidi si kuhatarisha usalama wa nchi?

● Kigezo cha yeye kuwa nje ya nchi, sio sababu ya kushindikana kumkamata kwake. Kwasababu walikua na uwezo wa kuomba mahakama itoe hati ya kukamatwa kwake na akamatwe huko huko alipo na asafirishwe (Arrest Order And Extradiction Order) mpaka tanzania kuja kujibu tuhuma. Hawakufanya hivi kwanini?

● Kwanini IGP na Mkuu Wa Usalama TISS, hawaja wajibishwa kwa kuhatarisha usalama wa taifa kwa kumuachia gaidi azurure mtaani mwaka mzima???

● IGP kutamka kwenye vyombo vya habari kwamba kuna ushahidi mzito wa ugaidi aliotaka kufanya Freeman Mbowe. Ndio ushahidi huu wa kufadhili Shillingi laki 6 (Yani kila mtuhumiwa alikua apokee Sh Laki 2)?

● Dunia nzima ilikuwa ikisubiri kuona ushahidi dhidi ya mtuhumiwa wa Ugaidi Freeman Mbowe, ukizingatia dunia inavyochukulia uzito wa makosa ya kigaidi. Ndio huu ugaidi wa sh laki 6?

● Swala la Freeman Mbowe kutaka kumshambulia au kumuua Ole Sabaaya, kwanini Mbowe hakufunguliwa mashtaka ya Attempt Murder au Assault au Causing Greviously Bodily Harm?

● Mashtaka ya kutoa Sh Laki 6, yanasimikwa kwa mashahidi 24 na vielelezo 19??? Kweli??? Wakati sms ya Mpesa na Tigopesa pamoja na wakala aliotuma tu yanatosha.

Jamhuri imefanya upuuzi wa hali ya juu katika hili la Freeman Mbowe. Hichi ni kichekesho hata kipindi cha JPM hakijawahi kutokea. Wanahitaji tuzo za "KILI AWARDS".

Hii ni kuisiriba kinyesi Tanzania katika sura ya ulimwengu.

Kwa mambo haya, sasa dunia nzima itajua kwanini watanzania wana umuhimu na uhitaji wa "KATIBA MPYA".
 
Wadigo wanasama "Usineme ukamara"Tusubili Mahakama itende Haki.
 
Mbowe lazima afungwe, naona mwanaharakati wa kichagga anamtetea mchagga mwenzake aliyeanzisha chama chakuwatetea wachagga Tanzania, mashahidi na mawakili wengi kwenye kesi ya Sabaya ndio nyie nyie, inatia mashaka.

Muangalie huyo wakili anamsimamia Sabaya koa mpaka dactari aliyekuja kutoa ushahidi mahakamani. Duh! Laana ya ukabila mbaya sana
 
Mbowe lazima afungwe..naona mwanaharakati wa kichagga anamtetea mchagga mwenzake aliyeanzisha chama chakuwatetea wachagga Tanzania

Mkuu fanyeni upuuzi woooooooooooote lakini hili la ukabila achaneni nalo kwani kila mtu atakuwa mhanga maana kila mtu ana kabila lake. Hii ni sawa na kuchoma nyumba ambayo uko ndani yake.
 

Gaidi anatumiwa salamu za rambirambi na raisi wa nchi wiki moja kabla ya kukamatwa kwake.

[emoji28][emoji28][emoji28],yaani Watanzania tumepatikana aisee
 
Back
Top Bottom