Eti Morogoro kunapatikana samaki wakubwa kuliko wale wa Ziwa Victoria?

Eti Morogoro kunapatikana samaki wakubwa kuliko wale wa Ziwa Victoria?

Morogoro ya wapi ambayo ina samaki wakubwa kuliko wale L.Victoria ?
 
Kuna ziwa hapo Moro linaitwa lake Mogela wanapatika kwa wingi sana hao samaki,
 
Naomba nikujibu kitaalam kidogo.
Kwanza sio kweli kwamba Samaki aina ya Kitoga ni mkubwa kuliko ''samaki wa ziwa Viktoria'' kama ulivyouliza hapo juu.

Kitoga anaweza kuwa samaki mkubwa kuliko aina kadhaa za samaki wa ziwa Viktoria lakini hawezi kuwa mkubwa kuliko ''samaki wote'' wa Viktoria. (Maana swali lako ni jumuishi)

Kwenye Ziwa Viktoria kuna Samaki anaitwa SANGARA, kwa kizungu wanamwita NILE PERCH au kitaalam anaitwa Lates niloticus

Huyu bwana ndiye SAMAKI MKUBWA KULIKO SAMAKI WOTE BARANI AFRIKA ukiondoa samaki wanaopatikana baharini.

Ukubwa wake unafikia hadi urefu wa futi 6.5 (kitanda cha 6x6 kina futi 6.0) na uzito wa pauni takriban 500 ambazo ni sawa na kilogram zipatazo 227 (uzito wa mifuko minne ya simenti na mmoja wa chokaa).

Kuhusu suala la utamu, hilo ni suala ''subjective'', watu tofauti wanaweza kuwa na maoni tofauti juu ya utamu wa kitu kimoja dhidi ya kingine.

Nilitaka kuliweka sawa hilo la ukubwa kwanza.

NB: Tunaweza kuwagawa samaki katika makundi mawili, samaki wa maji chumvi (baharini) na samaki wa maji baridi (maziwa, mito, mabwawa, n.k) ambapo katika kundi hili Sangara ndiye mkubwa wao hapa barani Afrika.
 
Morogoro ya wapi ambayo ina samaki wakubwa kuliko wale L.Victoria ?

Fika Msamvu area utawapata ila angalia usikamatwe na Kamanda Wilbroad Mtafungwa RPC wa Moro kwani anafuata agizo la kutunza nyara za serikali zisitumike vibaya
 
Ukiambiwa Morogoro siyo kule kwa wachomoa betri ni Kilombero nenda Mlimba, mito mikubwa inapita Moro.
Unajua Hapo Msamvu Kwa Wachomoa Battery Hakuna Mito Mingi Na Mikubwa
Fika Kilombero Hasa Kidatu Wanazalisha Umeme

Unaambiwa Kuna Nyakati Wanafunga Maji Kutoka Kwenye Mitambo Ya Umeme Watu Huwa Wanapata Samaki Wengi Sana Wakubwa Yaani Mpaka Mamba Wanabidi Watoke Mtoni
Maana Maji Yanakauka
 
Ya kweli hayo mkuu
Au ww ndio uliempiga fix Jamaa mpaka kaja kuuliza huku

Mkuu,sina shaka na taarifa niliyoitoa kabisa,hebu jaribu na wewe pia kufanya utafii kwa kuwaulizia watu wanaowafahamu hao samaki then uje kuleta mrejesho humu.
 
Kama aliyekuambia ni mluguru au mkaguru usimwamini, hao watu kila kitu kwao ni kikubwa, kwa masikio yangu nimewasikia wakisema
  1. Mindu ndiyo bwawa kubwa kuliko yote Afrika Mashariki na Kati
  2. Round about ya Msamvu ndiyo kubwa kuliko zote Afrika Mashariki na Kati
  3. Stand ya Msamvu ndiyo kubwa kuliko zote Afrika Mashariki na Kati
  4. Mlima Uluguru ndiyo wa pili kwa urefu katika Afrika Mashariki baada ya Kilimanjaro
  5. Morogoro ndiyo inaongoza kuwa na vyuo vikuu vingi Tanzania
  6. Morogoro ndiyo inaongoza kwa kutoa wachezaji nyota Tanzania (sina uhakika)
  7. Na sasa Morogoro ndiyo yenye samaki wakubwa kuliko wa ziwa Victoria
  8. Very soon watawaingiza wahanga wa lory la mafuta kwenye records (tusubiri)
 
Mologolo ni jiji kasolo Bahali sasa hao Samaki wakubwa wanatokea wapi
duh.... rakini lafiki wewe rire jiji kasolo bahali rinakosa samaki kweri.... mologolo jiji kasolo bahali rakini rina mito na mabwawa razima riwe na samaki.....
 
Mkuu ukiwa Ifakara ndio utaamini ni kweli halafu hawana bei nilienda kule nilishuudia
 
Kama aliyekuambia ni mluguru au mkaguru usimwamini, hao watu kila kitu kwao ni kikubwa, kwa masikio yangu nimewasikia wakisema
  1. Mindu ndiyo bwawa kubwa kuliko yote Afrika Mashariki na Kati
  2. Round about ya Msamvu ndiyo kubwa kuliko zote Afrika Mashariki na Kati
  3. Stand ya Msamvu ndiyo kubwa kuliko zote Afrika Mashariki na Kati
  4. Mlima Uluguru ndiyo wa pili kwa urefu katika Afrika Mashariki baada ya Kilimanjaro
  5. Morogoro ndiyo inaongoza kuwa na vyuo vikuu vingi Tanzania
  6. Morogoro ndiyo inaongoza kwa kutoa wachezaji nyota Tanzania (sina uhakika)
  7. Na sasa Morogoro ndiyo yenye samaki wakubwa kuliko wa ziwa Victoria
  8. Very soon watawaingiza wahanga wa lory la mafuta kwenye records (tusubiri)
La chuo nakubaliana nao
Round about nakubaliana nao
Stand kwa sasa nakubaliana nao
Mabwawa ya kutengeneza Mindu nakubaliana nao
Mengine siwez jibia
 
Mkuu ukiwa ifakara ndio utaamini ni kweli alafu hawana bei nilienda kule nilishuudia
Kaka nakataa katika hili mimi nipo Ifakara hapa viwanja 60 ila naweza sema kuwa ukubwa wa kitoga huwezi ukalinganisha na ukubwa wa sangara na hata radha kwa upande wangu. Hili utaweza kubisha kama hujawahi kukaa maeneo kama mwanza, ukerewe, kinesi, kibuyi, shirati na maeneo yanayozunguka ziwa Victoria.

Kwani sangara mara nyingi sokoni inabidi akatwe vipande kisha kuuzwa kwa kilo maana mtu moja hawezi nunua labda apelekwe kiwandani.

Na ukiacha huyo kitoga hao wengine hamna kitu kama perege, ndungu, kambale. Hamna kitu.
 
Sasa kama umeamua kuwa Thomaso si uende ukajionee?
 
Back
Top Bottom