Naomba nikujibu kitaalam kidogo.
Kwanza sio kweli kwamba Samaki aina ya Kitoga ni mkubwa kuliko ''samaki wa ziwa Viktoria'' kama ulivyouliza hapo juu.
Kitoga anaweza kuwa samaki mkubwa kuliko aina kadhaa za samaki wa ziwa Viktoria lakini hawezi kuwa mkubwa kuliko ''samaki wote'' wa Viktoria. (Maana swali lako ni jumuishi)
Kwenye Ziwa Viktoria kuna Samaki anaitwa SANGARA, kwa kizungu wanamwita NILE PERCH au kitaalam anaitwa Lates niloticus
Huyu bwana ndiye SAMAKI MKUBWA KULIKO SAMAKI WOTE BARANI AFRIKA ukiondoa samaki wanaopatikana baharini.
Ukubwa wake unafikia hadi urefu wa futi 6.5 (kitanda cha 6x6 kina futi 6.0) na uzito wa pauni takriban 500 ambazo ni sawa na kilogram zipatazo 227 (uzito wa mifuko minne ya simenti na mmoja wa chokaa).
Kuhusu suala la utamu, hilo ni suala ''subjective'', watu tofauti wanaweza kuwa na maoni tofauti juu ya utamu wa kitu kimoja dhidi ya kingine.
Nilitaka kuliweka sawa hilo la ukubwa kwanza.
NB: Tunaweza kuwagawa samaki katika makundi mawili, samaki wa maji chumvi (baharini) na samaki wa maji baridi (maziwa, mito, mabwawa, n.k) ambapo katika kundi hili Sangara ndiye mkubwa wao hapa barani Afrika.