Liverpool VPN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2020
- 6,958
- 16,358
- Thread starter
- #21
Kwenye ajira za Utumishi Kuna kundi la watu aina mbili.....Cha ajabu ni nini!? Nenda siku moja inteview pale Dodoma mara nyingi zinafanyika pale Udom, utakuta magari makali hatari yamepaki nje wamiliki wapo ndani wanapambana na written interview.
Si hivyo tu, nimeenda interview nimekutana na jamaa wanafanyi benk wanalipwa m1 + lkn wanagombea mshahr wa laki 7 pale Udom.
1. Kuna waajiriwa tayari wa serikali ila wanataka fursa kwengine, then wanaomba.
Mtu ni muhasibu Wizarani anaomba Kazi na kwenda interview ili ahamie TRA
2. Kuna wanaofanya Kazi private, Hawa nataka kuhamia serikalini kwasababu ya job security.
Mimi sina shida na watu kama hao
Mimi mshangao wangu upo kwa Hawa watu wa JF ambao wao Kazi yao ni kuuponda uwalimu kwenye nyuzi nyingii ila leo WANAUKIMBILIA..!!
Yaani unamponda demu kwa masela halfu kesho unamuoa kweli?
Kama kitu unakipenda na wakati huo huna si uchune tu na sio kukiponda?
#YNWA