MoseKing
JF-Expert Member
- Jul 5, 2017
- 4,928
- 8,976
Watanzania wengi sana wanaishi kwa CHUKI inayosababishwa na WIVU Mkali.Nilichogundua hapa JF.
-Karibu 80% tuna maisha duni sana
-Karibu 19% wana maisha ya kati.
-Sio zaidi ya 1% ndio wana maisha bora (na huwa hawajisemi wala kuwapondea wengine)
Wengi wanaficha ficha hili kwasababu Wana DNA ya UNAFIKI.
Nakuthibitishia hili, Hakuna watu wanaoongoza kuchukiwa na watu kama wale wenye kipato fulani, aidha MTUMISHI au Mfanyabiashara mwenye vipesa fulani.
Na Kama kungekuwa na Chama Cha siasa ambacho sera yake Ni kudhibiti Watumishi na Wafanyabiashara, basi kingepata wafuasi wengi sana.
Unakuta jitu linaponda kazi fulani mbaya na hailipi, kumbe lenyewe linaitaka hiyo kazi.