Eti Rais Samia Suluhu Hassan anaweza kweli kuwa nyuma ya uovu anaotendewa Tundu Lissu?

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
11,999
Reaction score
24,328
Sitaki kuamini kwamba MamaSamia2025 yuko nyuma ya mpango wa hiki kinachoendelea.

Ninafahamu kwamba MamaSamia2025 ni MTU mwenye dhamira safi licha ya kwamba watu walipotekwa alisema ni vijidrama na Mzee Kibao alipouawa na watu wanaodaiwa ni Polisi, akawapa Polisi haohao KAZI ya kujichunguza na mpaka hawajaja na majibu wala MamaSamia2025 hataki kufuatilia uchunguzi umefika wapi?

Huyu kiumbe aliyekatwa Jana, huko Mbinga, ni mpakwa mafuta wa Bwana, msimdhuru, wala msimbambikizie kesi yoyote. Kufanya hivyo ni kujiweka kwenye hatari kubwa, kwani kumchokoza Mpakwa Mafuta wa Bwana ni sawa na kuichezea mboni ya jicho la Mungu mwenyewe.

MamaSamia2025 , tunafahamu kwamba wewe ni mbobevu wa maswala ya kidemokrasia, huyu Tundu Lissu asikutishe kitu, hata akikishinda ni kwamba yeye alizaliwa ili ashinde, nenda naye kidogo kidogo. Kwa mamlaka iliyokuwa ndani yako, waamuru Polisi kumwachia mara moja bila masharti yoyote.

Kuhusu NO REFORM NO ELECTION, wala isikukondeshe, maboresho hayo ni kwa faida ya sisi wananchi wote bila kujalisha chama, dini wala kabila la MTU yeyote.

Kwa leo niishie hapo, lakini kaa ukijia huyo jamaa si MTU wa kawaida, ana roho ya Mungu ndani yake inayomuwezeshaga ku survive hata akipigwa na bomu, nini risasi?

Tundu Lissu AACHIWE BILA MASHARTI YOYOTE NA ASIBAMBIKIZIWE KESI YA UHAINI KAMA MLIVYOPANGA
 
Yeye akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na Usalama anawajibika kwa matendo maovu ya Jeshi la Polisi, kifupi hizo ni amri zake baada ya kuona Chadema inapata uungwaji mkono wa kiwango kikubwa juu ya Kauli Mbiu yao ya No Reforms No Election.
 
Ila chadema walikuwa wanataka kufika h7ku tulipo Leo, binafsi n8lihudhuria kikao Cha ndani alichofanya LISSU mkoa Fulani.

Mjumbe aliuliza endapo serikali ikaendelea na maandalizi ya uchaguzi Hadi ukafanyika tufanyeje? Tha guy akajibu tutachoma moto vituo vya kupigia kura na ofisi za serikali kwakuwa vipo katika maeneo yetu. Pia aliwataka wananchi kukinukisha( kufanya fujo)

Hivi Sasa kama wewe ndo jamhuri utamruhusu mtu apite kuhamasisha watu kufanya uvinjifu wa amani?


Au ni vile walitaka wakamatwe Ili movement izidi kutrend?
 
Yeye akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na Usalama anawajibika kwa matendo maovu ya Jeshi la Polisi, kifupi hizo ni amri zake baada ya kuona Chadema inapata uungwaji mkono wa kiwango kikubwa juu ya Kauli Mbiu yao ya No Reforms No Election.
NO REFORM NO ELECTION
 
Wewe ni team MBOWE au team CCM?
 
Behind the scene kuna watu wana nguvu ya kimaamuzi na kimamlaka kuliko Mh. Rais, Mh Rais anaelezwa tu mh. We subiri hii ni kazi yetu!!
 
Rais ni amir jeshi mkuu, hawa wote waliopo chini yake wanafanya kazi kwa ajili yake au kwa niaba yake kama amir jeshi mkuu hivyo yote yanayofanywa na polisi ni yake.
 
Hakika
 
Unaonaje wewe kama ni jamuhuri usirekebishe kero zinazotokana na tume ya uchaguzi Ili viongozi wapatikane kwa haki bila kupendelea chama chochote?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…