Euro 2020 - Special Thread | Pata kujua yanayojiri katika Michuano hiyo

Euro 2020 - Special Thread | Pata kujua yanayojiri katika Michuano hiyo

Bado Italia na Spain hizi nazo zikitolewa nitafurahi Sana.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
#Team Denmark
 
Belgium atakufa mapema sana. Italy wanaupiga mwingi balaa. Wanapanda na kushuka kwa speed ya bombadear.
Austria wamewatoa jasho sembuse Hawa watoto wa mbwa Ubelgiji??? Hii game tutarajie Italia akitoka mapema ..zile game za makundi alikutana na vibonde
 
Thorgan Hazard ni mchezaji wa soka wa Ubelgiji ambaye kwa sasa anacheza kama kiungo wa kushambulia au kama winga wa klabu ya Ujerumani iitwayo Borussia Mönchengladbach iiliyopo ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga na timu ya taifa ya Ubelgiji. Yeye ni ndugu mdogo kwa Eden Hazard na kaka wa Kylian Hazard. Wikipedia
Dogo Yuko vizuri bonge la goli, alikuwa Chelsea kwa Sasa Yuko wapi?
 
Mbona Bruno amecheza vizuri sana Leo? Apart na mashuti yake ya kulenga mnazi ametengeneza chance za kutosha, dribble na pasi zenye macho. Na vyote hivyo akiwa out of position.

Huyu kocha tu ana small team mentality, kumchezesha Bruno/silva/Felix kama mawinga na wote ni top playmakers kunatia mashaka.
Acha kumetetea huyu con artist hakuna kitu amefanya Jana.
 
Thorgan Hazard ni mchezaji wa soka wa Ubelgiji ambaye kwa sasa anacheza kama kiungo wa kushambulia au kama winga wa klabu ya Ujerumani iitwayo Borussia Mönchengladbach iiliyopo ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga na timu ya taifa ya Ubelgiji. Yeye ni ndugu mdogo kwa Eden Hazard na kaka wa Kylian Hazard. Wikipedia
Aha Yuko ligi ya ujerumani aise anajitahidi sana.
 
Netherlands Wamepigwa 2 - 0 nafikiri kikosi chao bado hakijasimama sawia yani kinakosa wachezaji bora eneo la kiungo na ushambuliaji mtu kama de jong (aliestaafu) angewasaidia sana pia 9 yap sio nzuri waliochezq 9 leo depay na hata promes alieingia sub aio natural strikers ......

pili maturity ni ndogo refer red card na maamuzi ya kimpira bado wanachanfamoto.....pia hata mfumo wao wa 5 - 3- 2 sio mzuri
Timu imejaa wachezaji wachanga sana ndiyo maana bado haijakaa sawa.
 
Back
Top Bottom