Kwa uchovu na uvivu niliyafumbua macho yangu kwa tabu!,hakuna kilichonipokea zaidi ya giza hafifu!
Malengelenge na mawenge machoni pangu ndio kwanza yalibisha hodi!.. hata masikio yangu yalinisaliti kwa muda,hakuna nilichoweza kusikia.
Nilipojaribu kujitikisa mwili wangu ilikuwa kama mtu ninaejitonesha vidonda! Ndo kwanza kwa tabu nikaanza kujitutumua kuamsha fikra zangu walau nikumbuke nipo wapi..?
Sikuwa nakumbukumbu yoyote mpaka sasa zaidi ya kuendelea kuhisi maumivu kwa kila kiungo nilichokitikisa!.. Giza hafifu liliendelea kunizodoa nakufanya nijione kama nipo kuzimu nikiusubiri moto wa jehanam tayari kwa kupikwa kama sio kukaangwa!.
Nilifikiri tena ndipo mara hii kumbukumbu zangu zikaanza kunirejea taratibu hata kulikumbuka jina langu! " Mimi ni Jonas" niliwaza! Kisha nikajiuliza "na huku nimefikaje..?" Sikuwa namajibu.. nilijituliza kwa sekunde kadhaa ndipo nikaamua walau nijivute kidogo nijue hata kama nimelala au nimekaa!. Nilipojaribu kufanya hivyo nilijikuta nikipiga ukelele wa maumivu ambao haukupokelewa na kitu chochote zaidi ya kuisikia sauti yangu ikijirudia kwa mbali!.. nilijiuliza nipo kwenye holu gani..?
Baada ya tafakuri zisizokuwa namajibu nilijipa muda kidogo huku mara hii nikianza kuuhisi mwili wangu ukianza kuingia nguvu zaidi ya hapo awali!.. mara hii ya tatu nilipojivuta angalau mwili uliitika nakunifata vile nilivyohitaji. Kumbe loh! Nilikuwa nimelala japo sikujua mahali gani nipo!.. macho yangu yenye malengelenge yalianza kupata ahueni baada ya kuanza kuona vyema kwa kupitia mwanga hafifu ambao sikutambua bado ulitokea kona ipi,hata pua yangu ilirejelewa na uhai pale nilipoanza kuhisi harufu kwa mbali.. Kuna muda nilihisi Kama ni harufu nilizokuwa nikizitambua lakini sikutilia maanani..
Punde nikajikuta nikilikumbuka jina "eve" Tena nikamalizia "Evelyn!!" Hapohapo kumbukumbu zangu zikaanza kurejea kwa kasi ya ajabu!. Nilianza kwa kuukumbuka usiku ule wa ulevi uliopindukia hadi kujizolea jina la ndama!,ikanijia na sura ya yule binti mzuri,binti ambae niliona alikuwa kiumbe cha kawaida tu kumbe abadani alikuwa ni stadi kazi alieweza kuijua michezo ya kutumbukiza risasi hata ktk mwili wa mtu!. Kumbukumbu zikanirejesha hadi nilipokuwa garini na wale watekaji nisiowafahamu! Mzungu mwenye pua yake ndefu,bunduki kichwani pangu na dereva mwenye miraba minne ambae ndie aliekuwa akirushiana risasi na eve,baada ya hapo ghafla kitambaa cheupe kilitua mkabala na pua yangu tokea hapo nikazirai kwa muda!.. nilipokuja kuzinduka nilijikuta kwenye chumba hichi huku nikiwa nimefungwa kwenye kiti cha chuma!.. niliendelea kukumbuka mateso makali yaliyoujeruhi mwili wangu huku nikilazimishwa niseme kile ambacho sikijui!..
Watesaji wangu walikuwa ni walewale yule mzungu mwenye kuvuta sigara na yule mtu mweusi wa miraba minne!.. nilikumbuka nilivyohojiwa kwa ukali "Una uhusiano gani na Evelyn..?" Majibu yangu hayakuwa ya kulizisha hivyo zawadi yangu ilikuwa ni ngumi ambazo hazikuchagua mahali pakupiga!,makofi na mabanzi yalisemeshwa vyema kwenye mashavu yangu hadi kutaka kujikojolea!. Ilikuwa Kama watu waliopeana zamu alianza yule baunsa akafata yule mzungu na kiswahili chake kisichofanisi!.
Majibu yangu yasiyoridhisha yaliwakasirisha watesi wangu hivyo muda mwingine nilipokea kipigo ambacho hakikuambatana na hoja yoyote!. Hatima yake walihamia kwenye korodani zangu!,kijasho chauoga kilinitoka hata ndimi zangu zilizokuwa zikisema ukweli zilianza kudanganya!.. nilipoulizwa eve ni nani..? Sikusita kujibu ni mchumba wangu!.
Anafanya kazi gani..? Nilijibu "ni karani!!" Ulikutananae vipi..? Hapo napo nikausingizia mwaka 2020 nakutoa historia ambayo hata sijui ilitokea wapi!!. Majibu hayo yote yalitoka ili kuzinusuru korodani zangu ambazo zilikuwa zimeshikwa barbara huku zikimwinywa kwanguvu nakujikuta nikigugumia kwa maumivu ambayo hayakujaliwa na watesi wangu!.
Licha ya maelezo yangu hakuna kilichosaidia!,kipigo kizito kiliendelea kunikabili mpaka pale nilipozimia nakujikuta nikiwa chini badala ya kitini nilipokuwa nikiteswa!.
Nilitoka kwenye kumbukumbu nakujivuta kwa nyuma mpaka nilipohisi nimeeagamia kitu kama ukutu!,nilipotazama vizuri niligundua nilikuwa sahihi ni kweli ulikuwa ni ukuta!..
Niliibetua shingo yangu nakutazama upande wapili niliona kidirisha kidogo ambacho ndicho haswa kilipitisha mwanga hafifu ambao ulinisaidia kuona ndani ya chumba kile.. nilikohoa kwa tabu Kisha nikaitupia macho miguu yangu iliyokuwa imepauka huku mguu mmoja tu wakushoto ndio uliokuwa umebakiwa na kiatu!.. vumbi liliutapakaa mwili wangu mithiri ya mtu aliekuwa akifanya kazi mgodini,sikujua mkoti wangu ulitupiliwa wapi zaidi yakubaki nashati langu amabalo lilikuwa limechanika nakubaki nusu ya tumbo langu kuwa wazi.
Damu iliyoganda niliiona ktk mkono wangu wa kulia! Ilikuwa ni jeraha la kisu nililojeruhiwa na watesi wangu pale nilipoleta ubishi!..
Niliyahamisha machoyangu nakuanza kutalii chumba kile kibovu ambacho hakukuwa nalaziada zaidi ya mimi mwenyewe,kiti pembeni yangu,vumbi pamoja na mbao zilizoishaisha zilizokuwa zimetapakaa chumbani humo!.
Kwa mbele yangu nilitazamana na mlango ambao ulionekana kuwa imara licha ya chumba chenyewe kuonekana kibovu!.
"Niko wapi..?"Mara hii nilijiuliza tena huku nikijigeuza kuelekea upande kulipokuwepo kile kidirisha kidogo!. Kimya ndio lilikuwa jibu peke ambalo ningelipata!. Kwa kujizoazoa nilijitahidi kusimama na kukaribia ktk kidirisha kile kujaribu kuangalia labda ningeweza kujijibu nipo wapi!!.
Hakuna chaziada nilichoona zaidi ya miti na vichaka na ndipo hapo nilipogundua kuwa ilikuwa ni mida ya jioni. Nilistaajabu kumbe nilitumia muda mrefu ktk chumba kile,nilipojitazama mkononi sikuiona saa yangu!,hata nilipojipapasa mifuko ya suruari yangu hakukuwa na chochote! Nilifyonza nilipojua walichukua hata simu yangu.
Kwambali nilianza kuhisi tumbo Kama likitoa lawama!. Zilikuwa ni lawama zilezile za njaa kiu chamaji nacho kilichombeza na kulikaba Koo langu!.
Ni mara hii ndipo machoyangu Kama yalipigwa na bumbuwazi!. Chumba hiki kipana kilikuwa kama na uwazi ambao kulikuwa na mlango kuacha ule niliouna mwanzo! Nilijiuliza ina maana sikuuona mlango huu hapo kabla!..?
Taratibu nilianza kuusogelea mlango ule ulioonyesha kuwa wazi kwa kijisehemu kidogo,nilipoukaribia niliufungua nakutahamaki kile nilichojionea ndani yake. Ilikuwa ni chumba kidogo chenye kiza zaidi,niliona watu wawili wenye jinsia mbili tofauti! Yule wakiume alikuwa kitini amefungwa huku kichwa chake akiwa amekielekezea kwa chini! Akiwa Kama mtu asiejiweza hata kutikisika!.. nae yule wakike alikuwa sakafuni penye mavumbi akiwa amelala pasipoutambuzi. Mapigo ya moyo yakaanza kunisaliti kwa kudunda hovyo! Kwaujasili niliamua kuingia na kuchunguza kile nilichokiona ili nijiridhishe Kama haikuwa ndoto.
Nilikaribia mpaka kitini alipokuwa ameketi yule wakiume kwa umakini mkubwa nilimsogelea nakumgusa ndipo nilipohisi ubaridi usiokuwa wa kawaida!,moja kwa moja nilijua mtu yule alikuwa tayari ameshapoteza uhai wake! Mapiga yangu ya moyo yaliendelea kunisaliti zaidi pale nilipougeukia ule mwili wakike uliokuwa umejilaza pale chini,nilijua nao utakuwa vivyohivyo Kama huyu!.. nilimeza funda la mate kisha nikausogelea mwili ule wakike,alionekana kuwa mdada mzuri mwenye nywele ndefu zilizofikia mabegani akiwa amevali Sweta jeupe lenye maneno niliyoyasomeka kwa tabu kutokana na giza yalisomeka "Sweetie" sikujishugulisha nayo bali niliiangalia miguu yake iliyokuwa imevalia suruari yakubana yenye rangi ya blue huku akiwa amevalia raba nyeupe zilizochakazwa na vumbi!.. hakuwa nakamba Wala kizingiti chochote kilichomzuia.. nilimsogelea na kushika mkono wake kwa sekunde kadhaa!,Jambo nililoligundua toafauti na yule wakiume binti huyu mwili wake ulikuwa na umotomoto jambo lililonipa ahueni na kuamua kupeleka sikio langu ktk kifua chake kilichojaa nyonyo za wastani,lengo lilikuwa ni kusikilizia mapigo yake ya moyo kama yalikuwa bado yapo ktk chati!.. lakini ktk punde hiyohiyo nilisikia muungurumo wa gari ukija kwa kufuata uelekeo chumba hiki tulimokuwemo!!..
Narudi..
Hakika! komaa tu hadi mwisho.
Tuendlee jamnii
Sent from my TECNO KC8 using
JamiiForums mobile app