Evelyn wa chumvi...

Evelyn wa chumvi...

Ilisikika breki ya gari kwa ukali ikisimama mbele ya gari letu huku mwanga wake wa taa ukitupiga kwa ukali na kuleta kero katika macho yetu!.
"Ni yule mwehu!" Alisema eve huku akiangalia kwa tabu kule mbele liliposimama lile gari!. Kwa haraka niliivuta suruali yangu iliyokuwa magotini kisha nikafunga mkanda na kumalizia na zipu wakati huo eve alikuwa nae akimalizia kuvalia kabati lake ambalo sidhani hata Kama alikumbuka kuwa amepigeuza au lah!.

Punde hiyohiyo ulisikika mlango wa ile land cruiser ukifunguliwa kisha kufungwa,wakati huohuo nami tayari nishaikalia siti ya dereva na kushikia ufunguo tayari kuubinya nakuanza kuteleza na lami!.. Jambo nilisilofahamu ilikuwa nimeshachelewa!,ulisikika mlio mmoja mkali ukifuatiwa na sauti ya kutoka upepo huku gari likiegama kidogo mbele ktk tairi la kulia!.. mapigo ya moyo yalinienda kasi sana!,sikujua nini chakufanya zaidi ya kuyatumbua macho yangu yaliyojawa usingizi ambao haukufahamika ungetumika sangapi!..

Punde ilisikika sauti ya mtu kutokea nje ikihanikiza! "Tulieni hivyohivyo!" Ilitulia na kuhanikiza tena "atakaeleta ubishi tunamaliza pumzi zake" sikujua nini chakufanya zaidi ya kutii amri ambayo sikujua ilitoka kwa nani!!,nilimtupia jicho eve ambae alikuwa bado siti ya nyuma akiwa amejibanza kwa uoga asijue nini chakufanya!. Alinitazama nami nikamtazama tena lakini mara hii macho yake yalionyesha utofauti fulani ambao sikuuelewa!.

Sekunde kadhaa tena sauti ile iliendelea kuhanikiza zaidi "taratibu fungua mlango wa gari!" Mtu huyo alisema maneno hayo huku akiniangalia kwa ukali na mikono yake ikiwa imeshikilia pisto!.. bila hiana mkono wangu uliitoa loki ya gari nakuucha mlango wazi bila kufanya chochote!.. "toka nje!" Ilisikika tena ile sauti kwa ukali zaidi!.. kabla sijafuata hatua nilimtupia jicho eve na kumuona Kama mtu mwenye harakati fulani ambazo sikuzielewa.. mtu yule alishinikiza Tena "toka nje!" Niliyatoa macho yangu kwa eve na kuanza kuutoa mguu wangu wa kulia nje Kisha wakushoto lakini kabla sijafanya chochote cha zaidi niliamliwa tena niiweke mikono yangu juu!,nami nilifanya hivyo kisha nikautoa mwili wangu wote garini! Nilisimama huku nikimtazama mtu yule wa miraba minne aliekuwa mbele yangu akininyooshea pisto yake!,aliniamuru nipige magoti nami nikafuata kama alivyohitaji!.

Ilibidi niwe mpole kwani sikuwahi kukutana na hali ya namna hii vitisho na ukali wake hakuonyesha kuwa ni mtu mwenye masihara!,alinitazama kwa ukali kisha akaangalia kwenye gari lake ambalo bado liliendelea kuunguruma na taa ziwakazo kwa ukali akatoa Kama ishara na sekunde hiyohiyo akashuka mtu mwengine mwanaumme mwenye miraba minne ambae alikuja haraka nyuma yangu na kunifunga kwa kamba ngumu mikononi!,alininyanyua msobe msobe na kunipeleka katika gari lile kwa puta! Huku nikisindikizwa kwa makofi ya mgongo ambayo yalikuwa kama yakinigutua kutoka ktk uzuzu!,nilipofika garini nilikalishwa siti ya nyuma ambapo kulikuwemo mtu mwengine ila yeye hakuwa Kama hawa!,

Yeye alikuwa mwanaume lakini mwenye asili ya kizungu! Alinikaribisha kwa kuninyooshea bastora yake huku akiwa hana wasiwasi!,ilionyesha kuwa kama mtu aliezoea utekaji Kama sio ujangili!,kwa sigara yake aliichafua hali ya hewa ktk gari lile na kuonekana mtu asiejali hata nilipokooa mara kadhaa!.

Yule jamaa aliniacha na yule mzungu huku akiwa ameniwekea bastora yake mkabala na kichwa changu!. Baada ya kumtazama mzungu yule niliyarudisha macho yangu kuangalia kule nje nilipomuacha eve garini,japo sikuweza kuona vizuri kutokana na Moshi wa sigara uliokuwa umetanda ila niliweza kujua nini kiliendelea huko nje!..

"Mtu yule aliekuwa ameshika pisto aling'ata tena kwa ukali "Toka nje" akimtaka eve atoke nje ya gari!.
Lakini amri yake hiyo haikutekelezwa na eve! Akaamuru tena mara hii huku akipiga risasi moja hewani kama ishara ya kukazia amri yake na angeweza kufanya chochote cha yatari!. Badala yake hakuna ambacho kilitokea!,eve hakuonyesha dalili yoyote ya kufanya chochote.. nami nilipatwa mshangao na kumakinika zaidi kwa kile kilichokuwa kikitokea!.. nilihisi labda eve alikuwa amezirahi kwa uoga ama alihofu zaidi kutoka na kuona Kama ulikuwa mwisho wa maisha yake!.

Mtu yule alihamaki zaidi na mara hii aliamua ashike bastora yake kwa mkono mmoja na kisha kulisogelea gari na kushika kitasa cha mlango wa nyuma na kisha kukivuta kwa spidi!.. Hapo ndipo kulitokea kile ambacho sikukitarajia! Ilikuwa Kama cheche ya moto iliyochomoka toka katika Benz ile na kumuingia mtu yule ktk kifua chake kipana!,kitendo hicho kilienda sambamba na mlio mkali wa bunduki ambao bila shaka ulitokea ndani ya gari alilokuwemo eve!..

Kama gunia la mzigo mtu yule alianguka chini huku kwa wepesi mkali eve alitoka nje na akiutumia mlango wa gari kama kinga akijibizana mapigo ya risasi na mtu yule alienileta garini!.. sikuamini nilichokiona kwani eve niliemfikiria kuwa ni binti muoga mara hii kwa umahili mkubwa alijibizana mikito ya risasi na watu hawa walioniteka!.. kwa michupio ya haraka eve aliruka na kufika mpaka nyuma ya gari lake huku akiuacha mlango ule wazi ukiendelea kuadhibiwa na mtu yule ambae nae alijihadhari kwa kujikinga katika land cruiser ile iliyokuwa bado ikikoroma!.

Baada ya kuona hivyo mzungu yule aliamua kunibana zaidi kwa kunipiga kabali nakuonyesha msisitizo ya kwamba nilitakiwa kutulia, mbwembwe zangu zozote zingenipa tiketi ya kufukiwa ardhini!.
Mtanange huko nje uliendelea huku wapiganaji hawa wawili wakionekana kuogopana!,Nani angemkalibia mwenzake akaiponze roho yake..? Ilikuwa Kama watu wanaohesabiana punde mtu yule baada ya kuona eve Kama asiejibu mashambulizi alianza kusogea kwa tahadhari akizani labda bunduki ya eve ilikuwa tupu isiyoweza kuleta madhara!.. ni katika tambo yake ya pili tu bunduki ya eve ilicheua na kumkosasa mtu yule,alirudi kwa spidi katika mlango wa cruzer ile iliyomsaidia kama kinga!.. kimya kilitawala kidogo huku ikisikika muungurumo wa cruzer tu!..

Kwa mbali mbele kulionekana gari nyengine ikija kwa spidi! Ilikuwa upande ule aliokuwepo eve! Lakini kadri ilivyokaribia ilizidi kupunguza spidi,ilipofika karibu eve aliamua apige risasi juu Kama njia ya kutahadharisha gari ile isizidi kusogea!.. kwa wepesi wa hali ya juu dereva yule alionekana akikata Kona na kurudi ilipotoka!.. eve aliendelea kutulia kule nyuma ya gari akijidhatiti lakini punde hii upande wa watesi wetu waliamua kumkosa eve!.

Ilisikika sauti ya yule mzungu ikiongea kiswahili cha tabu! "Wacha huyo panda gari mume yake ipo humu hali shachafuka " Alikuwa akimuamlisha mtu yule aliekuwa akijibizana kwa risasi na eve!.. kwa kuchupa haraka mtu yule alidandia garini na kushika usukani nakuanza kurudisha gari nyuma huku akiwa makini kutazama Kama eve angefanya chochote!,lakini eve hakufanya hivyo bado aliendelea kuwa mtulivu mpaka tulipoliacha lile eneo na kupata nafasi ya kupiga Kona na kuanza safari ambayo sikuelewa hatima yake!..

.......
 
Kipande chengine tayari wakuu..

Utunzi kazi nyie najuta kuanza hichi kitu ambacho sijui hata hatima yake..
Hapa najiuliza sasa hiyo chumvi itakuja kuingiaje.🤣🤣
Chumvi mbona hata kwenye papa ipo😂😂😂😂
 
Kwa uchovu na uvivu niliyafumbua macho yangu kwa tabu!,hakuna kilichonipokea zaidi ya giza hafifu!
Malengelenge na mawenge machoni pangu ndio kwanza yalibisha hodi!.. hata masikio yangu yalinisaliti kwa muda,hakuna nilichoweza kusikia.

Nilipojaribu kujitikisa mwili wangu ilikuwa kama mtu ninaejitonesha vidonda! Ndo kwanza kwa tabu nikaanza kujitutumua kuamsha fikra zangu walau nikumbuke nipo wapi..?

Sikuwa nakumbukumbu yoyote mpaka sasa zaidi ya kuendelea kuhisi maumivu kwa kila kiungo nilichokitikisa!.. Giza hafifu liliendelea kunizodoa nakufanya nijione kama nipo kuzimu nikiusubiri moto wa jehanam tayari kwa kupikwa kama sio kukaangwa!.

Nilifikiri tena ndipo mara hii kumbukumbu zangu zikaanza kunirejea taratibu hata kulikumbuka jina langu! " Mimi ni Jonas" niliwaza! Kisha nikajiuliza "na huku nimefikaje..?" Sikuwa namajibu.. nilijituliza kwa sekunde kadhaa ndipo nikaamua walau nijivute kidogo nijue hata kama nimelala au nimekaa!. Nilipojaribu kufanya hivyo nilijikuta nikipiga ukelele wa maumivu ambao haukupokelewa na kitu chochote zaidi ya kuisikia sauti yangu ikijirudia kwa mbali!.. nilijiuliza nipo kwenye holu gani..?

Baada ya tafakuri zisizokuwa namajibu nilijipa muda kidogo huku mara hii nikianza kuuhisi mwili wangu ukianza kuingia nguvu zaidi ya hapo awali!.. mara hii ya tatu nilipojivuta angalau mwili uliitika nakunifata vile nilivyohitaji. Kumbe loh! Nilikuwa nimelala japo sikujua mahali gani nipo!.. macho yangu yenye malengelenge yalianza kupata ahueni baada ya kuanza kuona vyema kwa kupitia mwanga hafifu ambao sikutambua bado ulitokea kona ipi,hata pua yangu ilirejelewa na uhai pale nilipoanza kuhisi harufu kwa mbali.. Kuna muda nilihisi Kama ni harufu nilizokuwa nikizitambua lakini sikutilia maanani..

Punde nikajikuta nikilikumbuka jina "eve" Tena nikamalizia "Evelyn!!" Hapohapo kumbukumbu zangu zikaanza kurejea kwa kasi ya ajabu!. Nilianza kwa kuukumbuka usiku ule wa ulevi uliopindukia hadi kujizolea jina la ndama!,ikanijia na sura ya yule binti mzuri,binti ambae niliona alikuwa kiumbe cha kawaida tu kumbe abadani alikuwa ni stadi kazi alieweza kuijua michezo ya kutumbukiza risasi hata ktk mwili wa mtu!. Kumbukumbu zikanirejesha hadi nilipokuwa garini na wale watekaji nisiowafahamu! Mzungu mwenye pua yake ndefu,bunduki kichwani pangu na dereva mwenye miraba minne ambae ndie aliekuwa akirushiana risasi na eve,baada ya hapo ghafla kitambaa cheupe kilitua mkabala na pua yangu tokea hapo nikazirai kwa muda!.. nilipokuja kuzinduka nilijikuta kwenye chumba hichi huku nikiwa nimefungwa kwenye kiti cha chuma!.. niliendelea kukumbuka mateso makali yaliyoujeruhi mwili wangu huku nikilazimishwa niseme kile ambacho sikijui!..

Watesaji wangu walikuwa ni walewale yule mzungu mwenye kuvuta sigara na yule mtu mweusi wa miraba minne!.. nilikumbuka nilivyohojiwa kwa ukali "Una uhusiano gani na Evelyn..?" Majibu yangu hayakuwa ya kulizisha hivyo zawadi yangu ilikuwa ni ngumi ambazo hazikuchagua mahali pakupiga!,makofi na mabanzi yalisemeshwa vyema kwenye mashavu yangu hadi kutaka kujikojolea!. Ilikuwa Kama watu waliopeana zamu alianza yule baunsa akafata yule mzungu na kiswahili chake kisichofanisi!.

Majibu yangu yasiyoridhisha yaliwakasirisha watesi wangu hivyo muda mwingine nilipokea kipigo ambacho hakikuambatana na hoja yoyote!. Hatima yake walihamia kwenye korodani zangu!,kijasho chauoga kilinitoka hata ndimi zangu zilizokuwa zikisema ukweli zilianza kudanganya!.. nilipoulizwa eve ni nani..? Sikusita kujibu ni mchumba wangu!.

Anafanya kazi gani..? Nilijibu "ni karani!!" Ulikutananae vipi..? Hapo napo nikausingizia mwaka 2020 nakutoa historia ambayo hata sijui ilitokea wapi!!. Majibu hayo yote yalitoka ili kuzinusuru korodani zangu ambazo zilikuwa zimeshikwa barbara huku zikimwinywa kwanguvu nakujikuta nikigugumia kwa maumivu ambayo hayakujaliwa na watesi wangu!.

Licha ya maelezo yangu hakuna kilichosaidia!,kipigo kizito kiliendelea kunikabili mpaka pale nilipozimia nakujikuta nikiwa chini badala ya kitini nilipokuwa nikiteswa!.

Nilitoka kwenye kumbukumbu nakujivuta kwa nyuma mpaka nilipohisi nimeeagamia kitu kama ukutu!,nilipotazama vizuri niligundua nilikuwa sahihi ni kweli ulikuwa ni ukuta!..

Niliibetua shingo yangu nakutazama upande wapili niliona kidirisha kidogo ambacho ndicho haswa kilipitisha mwanga hafifu ambao ulinisaidia kuona ndani ya chumba kile.. nilikohoa kwa tabu Kisha nikaitupia macho miguu yangu iliyokuwa imepauka huku mguu mmoja tu wakushoto ndio uliokuwa umebakiwa na kiatu!.. vumbi liliutapakaa mwili wangu mithiri ya mtu aliekuwa akifanya kazi mgodini,sikujua mkoti wangu ulitupiliwa wapi zaidi yakubaki nashati langu amabalo lilikuwa limechanika nakubaki nusu ya tumbo langu kuwa wazi.

Damu iliyoganda niliiona ktk mkono wangu wa kulia! Ilikuwa ni jeraha la kisu nililojeruhiwa na watesi wangu pale nilipoleta ubishi!..

Niliyahamisha machoyangu nakuanza kutalii chumba kile kibovu ambacho hakukuwa nalaziada zaidi ya mimi mwenyewe,kiti pembeni yangu,vumbi pamoja na mbao zilizoishaisha zilizokuwa zimetapakaa chumbani humo!.

Kwa mbele yangu nilitazamana na mlango ambao ulionekana kuwa imara licha ya chumba chenyewe kuonekana kibovu!.
"Niko wapi..?"Mara hii nilijiuliza tena huku nikijigeuza kuelekea upande kulipokuwepo kile kidirisha kidogo!. Kimya ndio lilikuwa jibu peke ambalo ningelipata!. Kwa kujizoazoa nilijitahidi kusimama na kukaribia ktk kidirisha kile kujaribu kuangalia labda ningeweza kujijibu nipo wapi!!.

Hakuna chaziada nilichoona zaidi ya miti na vichaka na ndipo hapo nilipogundua kuwa ilikuwa ni mida ya jioni. Nilistaajabu kumbe nilitumia muda mrefu ktk chumba kile,nilipojitazama mkononi sikuiona saa yangu!,hata nilipojipapasa mifuko ya suruari yangu hakukuwa na chochote! Nilifyonza nilipojua walichukua hata simu yangu.

Kwambali nilianza kuhisi tumbo Kama likitoa lawama!. Zilikuwa ni lawama zilezile za njaa kiu chamaji nacho kilichombeza na kulikaba Koo langu!.

Ni mara hii ndipo machoyangu Kama yalipigwa na bumbuwazi!. Chumba hiki kipana kilikuwa kama na uwazi ambao kulikuwa na mlango kuacha ule niliouna mwanzo! Nilijiuliza ina maana sikuuona mlango huu hapo kabla!..?

Taratibu nilianza kuusogelea mlango ule ulioonyesha kuwa wazi kwa kijisehemu kidogo,nilipoukaribia niliufungua nakutahamaki kile nilichojionea ndani yake. Ilikuwa ni chumba kidogo chenye kiza zaidi,niliona watu wawili wenye jinsia mbili tofauti! Yule wakiume alikuwa kitini amefungwa huku kichwa chake akiwa amekielekezea kwa chini! Akiwa Kama mtu asiejiweza hata kutikisika!.. nae yule wakike alikuwa sakafuni penye mavumbi akiwa amelala pasipoutambuzi. Mapigo ya moyo yakaanza kunisaliti kwa kudunda hovyo! Kwaujasili niliamua kuingia na kuchunguza kile nilichokiona ili nijiridhishe Kama haikuwa ndoto.

Nilikaribia mpaka kitini alipokuwa ameketi yule wakiume kwa umakini mkubwa nilimsogelea nakumgusa ndipo nilipohisi ubaridi usiokuwa wa kawaida!,moja kwa moja nilijua mtu yule alikuwa tayari ameshapoteza uhai wake! Mapiga yangu ya moyo yaliendelea kunisaliti zaidi pale nilipougeukia ule mwili wakike uliokuwa umejilaza pale chini,nilijua nao utakuwa vivyohivyo Kama huyu!.. nilimeza funda la mate kisha nikausogelea mwili ule wakike,alionekana kuwa mdada mzuri mwenye nywele ndefu zilizofikia mabegani akiwa amevali Sweta jeupe lenye maneno niliyoyasomeka kwa tabu kutokana na giza yalisomeka "Sweetie" sikujishugulisha nayo bali niliiangalia miguu yake iliyokuwa imevalia suruari yakubana yenye rangi ya blue huku akiwa amevalia raba nyeupe zilizochakazwa na vumbi!.. hakuwa nakamba Wala kizingiti chochote kilichomzuia.. nilimsogelea na kushika mkono wake kwa sekunde kadhaa!,Jambo nililoligundua toafauti na yule wakiume binti huyu mwili wake ulikuwa na umotomoto jambo lililonipa ahueni na kuamua kupeleka sikio langu ktk kifua chake kilichojaa nyonyo za wastani,lengo lilikuwa ni kusikilizia mapigo yake ya moyo kama yalikuwa bado yapo ktk chati!.. lakini ktk punde hiyohiyo nilisikia muungurumo wa gari ukija kwa kufuata uelekeo chumba hiki tulimokuwemo!!..

Narudi..




Hakika! komaa tu hadi mwisho.
Sabskribed
Tuendlee jamnii

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kwa uchovu na uvivu niliyafumbua macho yangu kwa tabu!,hakuna kilichonipokea zaidi ya giza hafifu!
Malengelenge na mawenge machoni pangu ndio kwanza yalibisha hodi!.. hata masikio yangu yalinisaliti kwa muda,hakuna nilichoweza kusikia.
Nilipojaribu kujitikisa mwili wangu ilikuwa kama mtu ninaejitonesha vidonda! Ndo kwanza kwa tabu nikaanza kujitutumua kuamsha fikra zangu walau niku
Utunzi 100% uandishi 100%
Everything 100% tunasubili muendelezo
 
Duh! yanayoendelea yanatishaa....... twasubiri mwendelezo..
 
Back
Top Bottom