KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
- Thread starter
- #141
Giza na mwanga wa mbalamwezi viliambatana na kushindana kutawala vichaka hivi,sauti za chura na wadudu mbalimbali ziliendelea kuhubiri huku mara hii zikiongezeka sauti zetu za hatua na mihemo kutokana na mbio za kumkimbia adui yetu!.
Alitangulia eve nikafuata mimi na kisha anitha alieonekana kuzidiwa na riadha hizi!,Kuna muda alionekana kukata tamaa na kuinama huku akihema kwa pupa,sikusita kumrejea na kumshika ili tuendelee na safari yetu ambayo hatukuijua mwisho wake..
Kwa mbali kiasi tuliweza kuona mianga ya tochi kadhaa za adui zikija kwa kasi kutufuata,muda mwengine walipeana maelekezo fulani ambayo sikuweza kuyasikia vyema kutokana na mbio tulizotimka!.
Eve alionekana kuwa bado imara katika kuzichukua hatua zake vilivyo!,nyuma yake tulijikongoja huku akitutupia jicho mara kadhaa na kuhimiza tumfuate.. penye vijito tuliruka,penye mawe tulipita pia. Ilifika hatua hata nami nguvu zilianza kuniishia,miguu ikaanza kuchoka riadha hii lakini kukimbia ndio ilikuwa nafasi yetu ya mwisho katika kuziponya nafsi zetu,kusimama na kuwasubiria adui hawa wasio na huruma ilikuwa kama kumkaribisha yule malaika mtoa roho ndani ya chumba chako!.
"Siwezi Tena" ilisikika sauti ya anitha nyuma yangu,niligeuka na kusimama.
alikuwa pale akitweta na kutojiweza huku amejiinamia.. niligeuza macho yangu tena kumuangalia eve nae alisimama akitutazama.
Nilipoangalia nyuma ya anitha kwa mbali sikuweza kuziona tena zile tochi zikitufuata bali ukimya ulitawala!,nilimkaribia nakumshika mkono wake wa kushoto nakumnyanyua lakini aligoma hata kufanya hivyo huku akionyesha ishara kwa mkono wake ya kuwa nimuache.
Eve alirudi na kutufikia nae akihema,alimtizama anitha kisha akanitazama mimi ndipo tukasikia sauti tena ya anitha ikiomba maji ya kunywa!,punde hiyohiyo kabla sentensi yake haijamalizika vyema ulisikika mlio wa risasi kutuelekea!.
Ilipita patupu bila madhara yoyote japo ilikuwa kama ishara nyengine ya kuziendeleza mbio zetu.. kwa spidi eve aliichomoa bastora yake nakujibu mapigo kule kuliposikika mlio wa risasi ulipotokea,Kisha akajibanza nyuma ya mti mkubwa uliokuwepo karibu.
Nami bila kungoja mara hiyohiyo nilimvuta anitha kwa mkono wake wa kushoto kisha nikamuweka mkabala nami nakuanza kumkokota tukielekea mbele, ulisikika mlio mwengine wa risasi ambao nao ulipita patupu ila ukiniacha mapigo ya moyo yakidunda zaidi!,nilihisi kama cheche zikipita kwenye mwili wangu na nguvu kunijaa zaidi.. nilivuta pumzi na kumkokota zaidi anitha,niliuhisi uzito wake wa miguu kwa kushindwa hata kukimbia,nilimvuta na kukaza mikono yangu katika mwili wake nakuanza kupiga hatua kubwakubwa. Niligeuza shingo yangu nyuma nakumuona eve akijibu risasi nyengine mbili kisha nae akatimka kutufuata.. alipotufikia alijibanza tena kwenye mti nakutuacha sisi tukizidi kujikokota.
Ilikuwa ni picha ambayo ilinihuzunisha na muda huohuo kunipa tumaini baada ya kuona eve akitimiza wajibu wake wa kuhakikisha usalama wetu japo nilimpoteza rafiki yangu kipenzi Jeff!,mara hii hata ule uhalali wa maneno yake walau nilianza kuuona.
Ghafla eve aliniita nami nikasimama na kugueka.. "jitahidini kuna gari hapo mbele!" Alinena huku akihema.
Sentensi yake ilikuwa kama ushindi mwengine uliotangazwa pasipo kutarajia!,hata nguvu na hali vikanivaa tena nakujikuta nikimeza funda la mate ambalo hata halikuwepo nakujikuta nikimeza hewa!..
Kabla sijachukua hatua yoyote nilijisachi katika mifuko yangu nakutoa magazine mbili zilizojaa risasi kisha nikamrushia eve,niliirejesha sura yangu kwa anitha na kumuangalia alivyokuwa akitweta huku akikunja sura yake kama mtu mwenye maumivu fulani.. sikujali hilo hata ile haja ya kumkokota sikuiona tena bali niliinama na kum'betua nikam'beba kama mtoto!. Miguu yangu ilizichukua tambo kubwakubwa na spidi kiasi huku nikihema na macho yangu mbele yakiangalia kwa umakini.
Huku nyuma kuliendelea kusikika milio ya risasi ambayo sikujua ipi ilikuwa ya upinzani ama ya eve.
Baada ya kutimka kama mita mia hivi niliweza kuliona barabara la vumbi huku upande wangu wa kushoto nikiliona gari jeupe likiwa limepaki pembeni,haraka nililifikia na kufungua mlango wa nyuma na kumuweka anitha kisha nikauendea mlango wa dereva na kuufungua huku nikiiikalia siti tayari kwa safari!, sikusubiri nilibetua mara kadhaa funguo za gari nalo likakubali kuwaka.. hatua niliyokuwa nikisubiri ni kuiona sura ya eve tu nami nizisurubishe tairi kwa kukanyaga ardhi!.
Milio ya risasi iliendelea kusikika ila mara hii ilisikika zaidi ikitusogelea,nilimtizama anitha nyuma ya siti akiwa amelala hovyo akihema taratibu huku akiyatumbua macho yake. Niliyahamishia macho yangu nje nakumuona eve akija kwa spidi nami hapohapo nilitia gia huku nikisubiri tu autie mwili wake ndani.
Punde hii alikuwa ndani ya gari nami nikaziamrisha tairi za gari ziichimbue ardhi na kuwaachia vumbi adui zetu waliobaki waking'aa macho katika kiza hichi amacho kulianza kukucha!.
Tulipita vilima na mabonde hatimae tukaifikia rami ambayo kwa kufuata maelekezo ya eve nilipinda usukani vile ilivyohitajika mpaka pale tulipofika mbele ya nyumba moja yenye isiyo na uzio.
Nilipaki na kutelemka,akafata eve na kisha anitha..
"Vipi hali yako..?" Nilimuuliza anitha,
Alinitazama kwa jicho legevu lililoonyesha hali zote za kuhitaji huduma katika tumbo lake!.
"Angalau sahivi" alijibu anitha.
Nilimsogelea nakumkagua kwa macho nikijaribu kutafuta tofauti yoyote katika mwili wake,lakini sikuona tofauti yoyote zaidi ya uchovu ambao sahivi ulianza kushuka.
Nilishusha pumzi zangu na kuhamishia macho yangu kwa eve,nae alinitazama pasipo kusema chochote Kisha nikamuona akiusogelea mlango wa nyumba ile nakutoa funguo alizozitumia kufungulia mlango.
Baada ya kufungua alitutazama mimi na anitha tuliokuwa tumesimama nasi tukimtazama,kwa macho yake tu ilitosha kufahamu kuwa alitutaka tuingie ndani,nasi pasipo hiana tulifanya hivyo.
Ilikuwa ni nyumba ya vyumba vitatu na sebule moja kubwa ambayo ilipakana na jiko huku likitenganishwa na ukuta uliokuwa na mlango wa kuingilia jikoni huko.. marumaru kadhaa na thamani zilizopatikana katika jengo hili zilitupokea kwa husda!. Sofa seti tatu zilizopangiliwa vizuri ziliizunguka meza ya kioo huku chini kukiwekwa zuria la manyoya na kufanya sebule hii kupendeza vilivyo..
Meza ya runinga ilituangalia huku ikiwa imejidhatiti kwa kubeba vitu vilivyohitajika kukaa hapo..
Eve alitukabidhi kila mtu chumba chake,nami nikazama kwenye chumba hicho kilichopambwa vyema kwa kuwepo kwa kitanda kikubwa kilichotandikwa vizuri huku kabati lenye kioo kikubwa likiwa pembeni likinitazama kama lililohitaji nilitazame ndani yake kulikuwa na nini,nililisogelea na kufungua!.
Lahaula! Nilipokelewa na nguo nzuri za kiume zilizopangwa vilivyo.
Pembeni kulikuwa na mlango nilivyofungua nilikutana na bafu yenye choo ndani yake ambayo ilipendezeshwa kwa vigau kuanzia sakafuni mpaka kwenye kuta zake.
Sikuwa na subira hapohapo nikavua nguo zangu nakutopea bafuni kujimwagia maji!.
Nilichukua takribani dakika 20 kukoga na kuutakatisha mwili wangu kisha nikalifuata taulo jeupe lililokuwa limening'inizwa nakuanza kujifuta maji,wakati nikifanya hivyo taratibu nikakisogelea kioo kilichokuwa kwenye kabati nakusimama mbele yake.
Nikiwa uchi wa mnyama nilianza kuudalizi mwili wangu,nilianza kuyatazama macho yangu yaliyojawa na uchovu Kisha nikafuata nywele zangu ambazo zilikuwa wastani tu huku zimenyolewa kwa mtindo wa panki. Nililitazama paji langu la uso ambapo kwa pembeni yake kulikuwa na mchubuko mdogo.. kilifuata kifua changu ambacho kilijitutumua kwa kuwa na manyoya hafifu kana kwamba yaliweka mgomo wa kuchomoza zaidi,tumbo langu nalo lilianza kufifia nakukisahau kile kitambi ambacho kilianza kujijenga ndani ya wiki kadhaa tu!. Nilijikuta naguna
"Mh!"
Kisha nikaongeza
"Siku tatu tu za dhoruba zimetosha kuupukutisha mwili wangu!".
Mawazo yakabadili mkondo na kuukumbuka ule usemi wazamani
"Dunia duara".
Nilikiri kweli kuwa ni duara kwani sikuwahi kufikiri kama leo hii mimi Jonas ningekuwa katika changamoto hii iliyonikuta!.
Changamoto ambayo ilinikuta kiajabu pasipo kutarajia,punde hiyohiyo nikamkumbuka rafiki yangu kipenzi Jeff!!.
Huzuni kwa mara nyengine ikanitawala,hasira nazo zikanitamalaki.
Maisha ya rafiki yangu niliyapoteza kizembe sana!,nilijiona nastahili lawama juu yake.
Kumbukumbu zikanivuta mpaka ile siku tulipokutana kule machimboni,hulka yake ya upole ndio zaidi iliwavutia wengi,ucheshi wake pia ulikuwa bayana kwa kila mtu.
Nani hakumjua Jeff gozabi!,
Uchapa kazi wake ndio haswa ulinivuta kuwa rafiki yake wa karibu. Niliikumbuka hata ile siku yakwanza tuliyoshirikiana katika uchimbaji nakutoka na chochote kitu.
Machozi ya uchungu yalinibubujika hata kuambaa katika mashavu yangu na hatimae kuanguka chini.
Nilijikuta nikiikunja ngumi yangu ya kulia na kujiapiza kulipiza kisasi kwa wale wote waliotiririsha damu ya rafiki yangu kipenzi!.
Taratibu huku nikitawaliwa na huzuni nilijivuta hadi kitandani nakujikuta nikitopea kwenye lindi la usingizi isivyo kifani.
**
"Hodi"
"Hodi"
Mlango ukafunguliwa na mgonga hodi pasipo ruhusa!.
Nilisikia sauti yake kwa mbali huku nikihisi viganja laini vikinigusa mashavuni kwa kunipigapiga!.
"Jonas"
"Jonas"
Niligutuka nakukutuna na sura ya eve ikiniangalia huku ikichanua tabasam zito!.
"Amka" alihizima eve huku akiendelea kunitazama!.
Ndipo fahamu zikanirudi nakutahamaki kumbe nilipitiwa usingizi huku nikiwa uchi!
Sikumuonea haya bali nilijivuta na kukaa sawia huku nikimtizama na macho yangu ya usingizi!
Nilipiga mwayo wa sekunde tano kisha nikapikicha macho yangu na kumtizama huku nikingoja aseme kile kilichomfunya aje anikatishe lepe langu la usingizi nililokuwa nikilitungua!.
Wala hakusema kitu!,ndo kwanza alijigeuza na kulielekea kabati la nguo akatafuta alichotafuta akachomoka na kaushi nyeupe pamoja na pensi iliyochorwa picha kubwa ya marijuana!.
Akaniletea na kunihimiza nivae mara, "ooh sorry,nimesahau boxer!" Akalirudia tena kabati nakutoka na boxer ambayo nayo hivyohivyo ilitamalaki picha ndogondogo za ule mmea wa Marijuana!.
Nilimuangalia na kumtupia swali la utani.
"Mwenye nazo alikuwa anatumia sana haya majani..?"
Akacheka kisha akajibu "hakuna mwenye nacho isipokuwa ni wewe,nimeyafanya haya kwaajili yako!" Aliyasema hayo huku uso wake mzuri ukiwa umejawa na tabasam ambalo sikuwahi kuliona hapo kabla!.
Eve alinisaidia kuvaa huku akinipigisha stori za uchokozi
"Sangapi sahivi..?" Nilimuuliza
"Nane na nusu mchana" alijibu huku akiiweka vyema kaushi yangu akiyomalizia kunivisha.
"Tumbo langu linamadeni!" Niliongezea.
"Ndicho nilichokufuatia"...........
Tutaendelea usiku wakuu.