Ewe Mwanaume, Jifunze Kutofautisha Kati ya Mapenzi na Huruma Unavyokuwa Unaishi na Mwanamke

Ewe Mwanaume, Jifunze Kutofautisha Kati ya Mapenzi na Huruma Unavyokuwa Unaishi na Mwanamke

Rorscharch

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
1,435
Reaction score
3,120
Katika mahusiano mengi ya watu wanaoishi kinyumba, mara nyingi mwanaume anaendelea kubaki na mwanamke hata kama moyoni alishamaliza safari—si kwa sababu ya mapenzi, bali kwa huruma. Unakuta kabisa mwanamke hana ile spirit ya kupambana na maisha; kwa wenzetu wengine kulelewa na kutegemea ni kama career choice.

Mwanaume anaumia kimya kimya, akijiuliza: "Nikimuacha, ataishije?" Lakini mwisho wa siku, tunapovunja mahusiano, wanaume tunageuka wabaya. Kauli inakuwa: "Nimempa kila kitu, nimemlea, nimempenda—ndo ananifanyia hivi leo?"
Na hicho “kila kitu”? Mara nyingi ni soksi tatu, mashati mawili na suruali moja—vyote ulivinunua kwa hela yake aliyokuibia baada ya kusahau wallet kwenye meza.

Tatizo ni kwamba hatusemi mchango wetu. Hatujigambi. Hatusemi jinsi tunavyohakikisha nyumba inakula, kodi inalipwa, na pesa za dharura zinapatikana. Na wakati mwingine, mapenzi yalikwisha miaka mitatu iliyopita; lakini kwa miaka miwili ya mwisho umekuwa unaishi kwa kuumiza nafsi yako—na mtu ambaye bora hata ungeishi na dada yako.

Ewe mwanaume, kama moyoni umemchoka, usijilazimishe. Acha mapema, okoa pesa zako, okoa akili yako, okoa muda wako.
 
Back
Top Bottom