Ewe mzazi, kabla ya kumpa mtoto jina, fikiria kitaa, ujana wake na shuleni ataishije nalo. Mtoto wa kiume anaitwa "Cesi"....

Matokeo ya Usasa, hivyo Wazazi wengi tumejikuta tumeingia kwenye huu mkumbo wa kutumia Majina mengi ya Kizungu na kuacha Majina yetu ya asili

Tumeacha Majina yetu ya asili kama vile Kitila, Tundu, Palamagamba, Matembo, Warioba, Bhoke, Andendekisye, Maijo, Wanzita, Zitto, Warunya, Kinjikitile, Rugemalila n.k

Baada ya miaka 50 ijayo huenda tukakosa kabisa Majina ya asili yetu πŸ™Œ
 
Ishu ni kua wabongo wanapenda sana kukatisha majina, siipendi hiyo tabia nakumbuka hata mimi kwenye ukuaji wangu kama nisingekaza ilikua naitwa Mari ndo nini sasa😳 baadae wakataka iwe Posa nilivyompiga konzi la utosi ikawa mwisho hadi leo ni Mariposa
 
Usiombe ukutane na kamama chenye DIPLOMA yaanii ni full kujifanya mzungu koko, hata jina la mwanae atachagua yeye atatafuta majina ya kwenye tamthiliya za kizungu na kumbandika mtoto!

Mtoto anaitwa FRUCTOSE, mara sijui SALTELYN... 😁😁😁😁

MAMA CELTEL, mama JONEL 😁😁... mwenyewe akiitwa hivyo anaona raha anatikisa mkia kwa madoido kama BATAMZINGA
 
Kuna kijiji kimoja nilienda nikakuta kuna mmama kamwita mwanae kumalija ni jina asili ya kisukuma sio mbaya sas shida ikaja jamii aliyopo ni tofauti na usukumani basi wakawa wanamkatisha wanamuita mama k.....ma wanaitoa hiyo lija ya mwisho inabak tafran, hauwez amin ilikuja kuwa kero kwa mama mtu hata kabla ya mtoto kufikia huko uliposema.
 
Ni kweli hilo ni jinala kisukuma,uchagani kuna ukoo wa mboroo walijibadilisha ukoo sababu ya ukakasi wa jina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…