Ewe mzazi, kabla ya kumpa mtoto jina, fikiria kitaa, ujana wake na shuleni ataishije nalo. Mtoto wa kiume anaitwa "Cesi"....

Hahahahaa balaa Bichwa wangu. Haujawahi kuniangusha kwa vituko..
 
Nakubaliana na wewe kabisa
 
umeandika vizuri ila mwishoni umezingua, Baba Junior hilo jina lina shida gani ? ni jina la kike hilo ??

Wewe unaitwa nani kwanza ?
 
Mkuu unaelewa nini kuhusu Culture Diversity?

Ishu ya Deborah na mfano wa mleta mada ni mazingira mawili na nyakati tofauti.
Cecil ni jina la kibantu? mfano nilioutoa unaendana na hilo jina alilosema mtoa mada kama issue ni culture diversity
 
Ni kweli hilo ni jinala kisukuma,uchagani kuna ukoo wa mboroo walijibadilisha ukoo sababu ya ukakasi wa jina
Sas shida hapo mkuu sio jina ila shida ni hilo jina linaendana na nature ya mahala ulipo baasi.
 
Ujinga kama huu utaukuta Afrika na hsa Tanzania tu. Watu wanaona ni kashfa kufananishwa na mwanamke! Mbaona kuna majina yanatumika kwenye jinsia zote?
 
Mimi ishu ilikuwa ni kwenye kuliandika na kulitaja jina langu "Umar" shule niliyosoma primary kulikuwa na ticha mmoja kila tukifanya hzi test za mwezi unakuta kabadilisha kwenye "U" kaweka "O" anahisi nimekosea

Siku moja akaja kuniita ananiambia niwe naandika vizuri jina nikamwambia jina langu ndo linaandikwa hivyo. Na kwenye kutaja kuna wengine waliita "yumari" wengine "Uma". Nikawa nawaacha tu kila mtu aite anavyotaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…