Ewura: Bei ya gesi ya kupikia imepanda kwa kati ya Tsh 2000 hadi 5000 kutokana na kupanda kwenye soko la dunia

Ewura: Bei ya gesi ya kupikia imepanda kwa kati ya Tsh 2000 hadi 5000 kutokana na kupanda kwenye soko la dunia

KILA kitu bei leo bati moja reject eti ni 22000,mpya 35 Bandari laki 4 na nusu,huyu mama na mwigulu udhani watz wote wanamiliki iphone
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kupanda kwa bei ya Gesi ya kupikia kwa kati ya Tsh. 2,000 hadi Tsh. 5,000 kulingana na ujazo wa Mtungi

Mabadiliko ya bei hizo ni kutokana na kupanda kwa bei ya Gesi katika Soko la Dunia. EWURA imesema kampuni za Gesi ndizo zitaamua lini zipandishe bei na kwa kiwango gani

---
Watanzania aliyetuloga sijui ni nani

Hawa jamaa wanaamua kutufanya wanavyotaka na hatuna la kuwafanya

Tozo, mafuta juu, gas juu maji na umeme wa kuungaunga

Machinga ndiyo kama vile wametiwa hasara bila kujali

Kwa kifupi tu gas ya 22000 itauzwa 24000

Na ya 53000 itauzwa 58000

Nadhani hii imeanza leo au itaanza kesho kwa mitungi ya oryx

Wananchi tupo tu tunaona ewala

Kuna wakati najilaumu

Ukitaka kumjua mtanzania vizuri lete habari ya yanga au simba au watu waonewe katika nyanja hiyo ndiyo utajua hujui lakini kwenye habari za msingi zinazohusu maisha moja kwa moja hakuna anayejali
Poa tu wacha wapinzani waisome namba
 
Tafuta hela wewe uache kulialia kama mbweha kwa vitu vidogo vidogo
Unaye lia kama mbweha ni wewe unayeishi kwa shemeji yako.

Hujui sembe inapatikana vipi wala shuka ya kujifunika.
 
"Tatizo soko la dunia"

Hiyo gesi tuliambiwa ilishauzwa sio ya kwetu, bado hamuelewi?!
Hadi kupanda kwa sabuni napo sababu ni soko la dunia?
Kuna issue nyingine kabisa kwenye huu upandaji wa bidhaa
 
Huyo ni kula kulala tena kwa shemeji yake unategemea atajuaje ugumu wa maisha?
 
Ukiona mfanyab8ashara amepandisha bei ya kitu na bado watu wananunua tu, ujue watu wanamudu.

Watu wakishindwa kununua kwasababu ya bei maana yake, itabidi wafanyabiashara washushe bei ili mzigo uende.

Hilo ndio soko huria.
Hii elimu umepata wapi?
 
Watu wa JF wengi ni wanafki sana!
Mlimtukana JPM humi kwa kusema kuwa anapambana kwaajili ya wanyonge wa nchi hii. Mkasema ninyi sio wanyonge leo mnalialia nini?
Tulieni dawa iwaingie 'mwendazake kaenda!
Mkuu mtu kufanya makosa ya wazi haipi nafasi ya kumsafisha Jpm alifanya makosa na kuna sehemu alifanya vizuri ni kawaida ndio maana aliacha usemi mtanikumbuka kwa mazuri yangu sio mabaya
 
Mkuu wengine tunapikia UMEME gas ziada tu. Nilikuwa nikinunua gas NAONA hasara tu,nikatafuta msufuria wa umeme hautumii umeme mwingi, kila ninachotaka kupika nautumia huohuo Mkuu natumia 20 kwa mwezi
Msufuria gani huo mkuu namimi nika nunue,
 
Siku wabunge wakianza ishi maisha kama yetu ndipo watakuwa serious.

Haiwezekani wafeel ugumu wa maisha kwa posho wanayopewa, mafta lita 1000 kwa mwezi. Never ever.

Kuna muda naona waziri anaongea vitu ambavyo kiuhalisia ni tofauti na hali ya mtaa ilivyo.

Maji hakuna halafu waziri anapita mtaani anashika bomba la maji anawajazia watu kwenye madumu eti ionekane ndo anachapa kazi na watz wanafurahi eti waziri huyu mchapakazi asilaumiwe ukame ni maamuzi ya Mungu.

Sasa si serikali ikae pembeni tuishi kwa kudra na maamuzi ya Mungu tu
Huku Dodoma kuna bawa lilijengwa na Mjerumani tangu miaka ya 50 na bado mpk leo lipo na linatoa maji kwajili ya kilimo cha umwagiliaji na matumizi mengine na halijawahi kukauka
Mabawa kama hayo yangejengwa na Serikali km alivyofanya mjerumani shida ya maji isingekuwepo.
 
Ila ni mzuri wa sura isee!

Siku za mwanzoni, watu kumshangilia sana mabarabarani kila akatizapo, ilinipa wakati mgumu sana nikijiuliza maswali bila kupata majibu... "ni nini kipya kaleta huyu mama?"

Limeendelea kunitafuna hilo swali hadi juzi nilipokuja kufafanuliwa na mama mmoja kwamba: asilimia kubwa ya binadamu(wanawake kwa wanaume) huvutiwa sana na mishepu ya wanawake ama wanawake wenzao.

Huburudika na kuona kama dhiki zao zinapungua kila waangaliapo mshepu wa adabu!

Na kama kiongozi ana mshepu sawasawa, basi watu hujaa pomoni, msioelewa mtadhani wamevutiwa na sera, kumbe watu wana burudani zao!

Nilipojichunguza, nami nikahisi nnao huo udhaifu. Ninapenda sana viongozi warembo.
Tena tukiwa ofisi moja, napenda awe ananiita ita kunituma kazi mara kwa mara, ama kunifanya chawa wake kabisa ili nipate muda wa kumuangalia na kuongea naye.

Mfano mwingine mi' si shabiki wala sielewi formation za mpira wa wanawake "netball", lakini hujikuta navutiwa na kwenda kwenye viwanja vya netball kila nikisikia kuna timu za kina mama zina cheza uwanjani, hiyo ni kwaajili ya kwenda kuona mishepu na si kuangalia mpira.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiendekeza hizi tabia utaanza kuwa mtu wa ajabu kwenye jamii
 
Back
Top Bottom