EWURA inatia aibu kufungia vituo vya mafuta visivyouza

EWURA inatia aibu kufungia vituo vya mafuta visivyouza

Wananchi tunapiga kelele kuwa serikali imelala haitusaidii walaji. Sasa inaamka na kuchukua hatua kwa maslahi ya walaji na taifa zinatokea kelele kuwa inakosea.

Kumbuka hao wauzaji wa mafuta wanapositisha biashara hata kwa nukta moja wanaikosesha serikali.kodi halali, pia wanazuia watoa huduma zinazohitaji nishati ya mafuta. Pia wanaleta taharuki kwenye jamii.

Nadhani lengo la serikali kuifanya sekta ya nishati ya mafuta kuwa huria ni kuimarisha ushindani wa soko na kupunguza ukiritimba wa ugavi. Sidhani kama ni busara kutumia fursa ya soko huria kuwatesa na kuwanyanyasa walaji kwa kuwanyima huduma kwa wakati.

Serikali imetuambia mafuta yapo ya kutosha. Lakini wenye vituo wanaivimbia kwa kusitisha kuuza mafuta kwa visingizio visivyo na kichwa wala miguu. Ni haki na wajibu wa serikali kutulinda sisi kwa kusitisha leseni za wote wanaogoma kuuza mafuta.

Je, lengo la wamiliki wa vituo vya mafuta ni kuidhoofisha hata kuiangusha serikali?

CC: ChoiceVariable Erythrocyte zitto junior Gwappo Mwakatobe FaizaFoxy figganigga Yericko Nyerere Retired Tindo raraa reree Extroverted Introvert Kenan john Depal JOANNA Mama Amon
Point nzuri sana.

Wanaozuwia mafuta ni wahujumu uchumi, wasinyimwe leseni pekee, wafungwe kwa kuhujumu uchumi.
 
Umeleta mawazo ya ki layman sana. Hivyo vituo kwanini havikufunga huko katikati ya mwezi vinafunga sasa hivi kusubiri bei mpya huoni kama huo ni uhujumu uchumi kabisa.
 
Point nzuri sana.

Wanaozuwia mafuta ni wahujumu uchumi, wasinyimwe leseni pekee, wafungwe kwa kuhujumu uchumi.
MHUJUMU UCHUMI NI YULE Importer anaekutangazia Kwamba hajaagiza mafuta kwa uhaba gola!

mtu ambaye yupo dukani kwake muda wa kuuza unategemea na ratiba zake!
SWALA la muda ni hiari ya mfanya biashara
 
Umeleta mawazo ya ki layman sana. Hivyo vituo kwanini havikufunga huko katikati ya mwezi vinafunga sasa hivi kusubiri bei mpya huoni kama huo ni uhujumu uchumi kabisa.
kwani kuna maelekezo ni wakati gani wanapaswa kupumzika?
 
unataka wauze kila siku kwa kanuni ipi?

Unafanya biashara ya petrol & diesel?

Unafahamu umuhimu wa petrol & diesel katika mzunguko wa maisha ya kila siku ya wananchi na nchi kwa ujumla?

Unafahamu kwamba petrol & diesel ni kati ya huduma ambazo sio tu kosa kisheria kucheza nazo bali ni almost an abomination kujaribu kuziyumbisha?

Unafahamu umuhimu wa petrol & diesel katika ukuaji wa uchumi wa nchi na watu wake?

Hebu jielimishe kwanza kazi ya EWURA ambazo nafahamu kwamba unazijua ila ndio nyakati zenu sasa wenye pesa kuyumbisha uchumi wa nchi uendane Sawa na matakwa yenu! Very selfish creatures!
IMG_7959.jpg

IMG_7957.jpg
 
Wew unayejua masharti ya leseni za biashara tuambie kazi ya Ewura ninini.....
kazi ya ewura ni kudhibiti ubora mafuta yabakie halisi,usalama usiathili majiran na miundombinu, bei kwa maana bei ibakie waliyoelekezwa huo ndiyo udhibiti!

MUDA WA KUFUNGUA NI UTARATIBU WAMFANYABIASHARA mwenyeww HAIWAHUSU
 
habari Wananchi

Ifahamike kwamba Siyo jukumu la serikali kulazimisha kuuza!

ewura kama mdhibiti mkuu anatakiwa afanye kazi kisomi siyo kikoloni!

Ifahamike ewura hana shea yoyote kwenye mitaji ya wafanyabiashara ya mafuta:

wakati mfanyabiashara anatafta mtaji huwa peke yake!
anapotafta eneo la kujenga huwa peke yake
anapodaiwa mikopo huwa peke yake
anapojenga kituo gharama huwa juu yake
anapoomba kibari ewura hutozwa fedha tena wakati mwingine na bahasha ili kupatiwa kibali
mafuta yakishuka huwa ni hasara kwa mfanyabiashara mwenyewe
kwa maana hiyo mfanyabiashara huyu mamlaka zinamtaka kuzingatia hali ya usalama na kuuza mafuta katika hali ya usalama lakini hawapaswi kabisa kumpangia wa kuwauzia!

Mfanyabiashara anayo haki ya kuamua Baadhi ya magari asiyauzie mafuta hiyo ni haki yake na hapaswi kushurutishwa

mfanyabiashara anaweza kuamua kuuzia magari mfano aina benz na BMW tu na akagoma kuuzia gari za toyota ni haki yake hapaswi kuuadhibiwa

anaweza kataa kuuza kwa kuomboleza kifo cha ndugu yake ni haki yake hapaswi kushurutishwa

anaweza kuamua kujipa likizo na wafanyakazi na hutakiwi kumshurutisha

Mtu ambaye hajawahi kuuza hata mihogo kisa kapewa mamlaka ya kudhibiti anaamua kufungia watu waliowekeza akili, pesa na nguvu! hii siyo sawa kabisa!

Ewura ni mdhibiti lakini ni katika hali ya ubora na usalama na siyo kupangia watu wakati na muda wa kuuza!

Ewura walipaswa kujiuliza wanakosea wapi kwanini wafanya biashara wafiche mafuta,

Kama wanaona ni raha kuuza basi wauze wao kila wilaya wajenge kituo cha mafuta wauze kwa bei rahisi kubalance soko,

ebu tuwaze kidogo tu kama kweli Ewura wanawapenda sana wananchi kwanini bei inapanda kiholeka?

kama ewura wanajali wananchi kwanini hawaruhusu vibali vya vituo vya gesi barabara za mikoani? kwanini huwa wanagoma kutoa leseni za kujenga vituo vingi vya gesi CNG ukiachilia hivi viwili/vitatu dar nzima?

kwanini vituo vya CNG vipo limited nani anayetoa hayo maelekezo kuzuia visijengwe kwa faida gani?

Badala ya kufungia hivi vituo vinavyojitafta kimaisha soko huria, Yangekuwa maoni yangu ningelifukuza team nzima ya Ewura ije akili mpya ambayo itadhibiti kwa Akili na siyo kizamani namna hii ambako kunaleta mwanya wa rushwa!

Nani atakuwa salama kama kituo kinaweza fungwa kwasababu kimejipa off? VIPI Kama watendaji wa Ewura wakiamua kuitumia hiyo kama fimbo kuomba rushwa na wasipopewa wanakifunga kwa KAULI ZA NAMNA HIYO?

Ni akili ya hovyo sana kufungia Wachuuzi wakati wenye matatizo ni EWURA WENYEWE

Wewe nadhani huwa unafikiri kwa kutumia kichwa cha chini!
 
Wananchi tunapiga kelele kuwa serikali imelala haitusaidii walaji. Sasa inaamka na kuchukua hatua kwa maslahi ya walaji na taifa zinatokea kelele kuwa inakosea.

Kumbuka hao wauzaji wa mafuta wanapositisha biashara hata kwa nukta moja wanaikosesha serikali.kodi halali, pia wanazuia watoa huduma zinazohitaji nishati ya mafuta. Pia wanaleta taharuki kwenye jamii.

Nadhani lengo la serikali kuifanya sekta ya nishati ya mafuta kuwa huria ni kuimarisha ushindani wa soko na kupunguza ukiritimba wa ugavi. Sidhani kama ni busara kutumia fursa ya soko huria kuwatesa na kuwanyanyasa walaji kwa kuwanyima huduma kwa wakati.

Serikali imetuambia mafuta yapo ya kutosha. Lakini wenye vituo wanaivimbia kwa kusitisha kuuza mafuta kwa visingizio visivyo na kichwa wala miguu. Ni haki na wajibu wa serikali kutulinda sisi kwa kusitisha leseni za wote wanaogoma kuuza mafuta.

Je, lengo la wamiliki wa vituo vya mafuta ni kuidhoofisha hata kuiangusha serikali?

CC: ChoiceVariable Erythrocyte zitto junior Gwappo Mwakatobe FaizaFoxy figganigga Yericko Nyerere Retired Tindo raraa reree Extroverted Introvert Kenan john Depal JOANNA Mama Amon

Wanataka Serikali irudi kuishi ndani ya mifuko yao kama enzi zile.

Wanataka waitwe Ikulu wabembelezwe!

Very very selfish!
 
Mtuhurumie na sisi wananchi ninyi watu wa mafuta
Uhaba wa mafuta unafanya bidhaa nyingi muhimu kupanda bei ghafla.
stop being greedy.
empoter wa mafuta wanamjua wao kama serikali, mfanyabiashara wa kituo cha mafuta anachukua mzigo kama ulivyoingia!
MUDA WA KUUZA NI WAKE MWENYEWE ANAWEZA KUUZA USIKU TU NA MXHANA AKALALA
 
regulator haimaanishi kulazimisha kufungua,
regulator waliyo nayo ni katika usala, ubora na upandaji bei!

REGULATOR Haiingilii uhuru wa mtu muda wa KUFUNGUA sijui unanielewa wewe!
MUDA WA KUFUNGUA ni maamuzi ya mfanya biashara!

Wewe huu mjadala unafanya makusudi kuandika haya ama ndio umetumwa?

Hao waliopewa hizo license za kuuza mafuta waulize vizuri vigezo na masharti ya kupata hizo license watakwambia.

Mmeshiba sasa mnataka kunya kwenye sahani kabisa!
 
Hawawezi kupumzika wote karibu nchi nzima kwa kipind sawa akili yako tu haitoshi kukwambia kua kuna uhuni hapo
sasa kama mdhibiti anasaidiaje kuzuia bei kupanda kama taifa wakati yeye ndiye anayeyapandisha bei, badala ya kuongeza ruzuku kama mamlaka mafuta yashuke,?
mafuta kwa lita kutoka inje ni tsh 950 ...kama serikali kwa wasipunguze ushuru unayapandisha mafuta hadi yafike elf 3500?
 
Leo nimehitimisha kuwa hii nchi haiwezi kuendelea mpaka ujinga uishe miongoni mwa Watanzania.

Hivi kumbe ukiwa na mtaji wa kutoa huduma fulani usifuatiliwe hata kama unatoa huduma chini ya kiwango? Du!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
kazi ya ewura ni kudhibiti ubora mafuta yabakie halisi,usalama usiathili majiran na miundombinu, bei kwa maana bei ibakie waliyoelekezwa huo ndiyo udhibiti!

MUDA WA KUFUNGUA NI UTARATIBU WAMFANYABIASHARA mwenyeww HAIWAHUSU
Mkuu nadhani kuna kitu unataka kulazimisha hapa.

Muda wa kufunga au kufungua kituo sio tatizo.
Tumeshuhudia na tumeona vituo vingi vikifungwa saa 12 jioni aidha kwasababu za kiusalama au la.

Tumeona vituo vikifungwa masaa 24 aidha kwa upungufu wa mafuta au matengenezo kadhaa lakini haijawa shida
lakini kitendo cha kufunga kituo makusudi bila sababu ya msingi, na sababu kuu ni kulazimisha bei ipande hilo ni tatizo kwa jamii nzima.

Na kingine ukumbuke nchi yetu ni state-guided capitalism, hivyo basi kuna regulations na government interference kwenye baadhi ya mambo ambayo yana athiri jamii kwa ujumla.
Ikiwa unataka uhuru huo unaotetea inawezekana hata mafuta yangekua lita 7000 au 10000 na hamna yeyote angeweza kutetea jamii ambayo wengi wao ni wa kipato cha chini.

Hivyo basi nakusihi usiangalie upande mmoja angalia na wale watu wa chini kabisa ambao hata kupata 1000 ni mtihani kwa siku.
 
kazi ya ewura ni kudhibiti ubora mafuta yabakie halisi,usalama usiathili majiran na miundombinu, bei kwa maana bei ibakie waliyoelekezwa huo ndiyo udhibiti!

MUDA WA KUFUNGUA NI UTARATIBU WAMFANYABIASHARA mwenyeww HAIWAHUSU
Aise! Bro hebu ficha ujinga wako.
 
Wanataka Serikali irudi kuishi ndani ya mifuko yao kama enzi zile.

Wanataka waitwe Ikulu wabembelezwe!

Very very selfish!
tatizo wala haliko kabisa chini, Sema EWURA Wanawalinda hao importer labda hawakamatiki
 
empoter wa mafuta wanamjua wao kama serikali, mfanyabiashara wa kituo cha mafuta anachukua mzigo kama ulivyoingia!
MUDA WA KUUZA NI WAKE MWENYEWE ANAWEZA KUUZA USIKU TU NA MXHANA AKALALA
Labda huyapi mafuta uzito unaostahili,

chukulia mafuta kama vituo vya afya.

Chukulia vituo vya afya vya private vigome kutoa huduma kwasababu wanazojua wao, unadhani hali itakuaje?
basi uzito huo huo peleka na kwenye mafuta ndugu dmkali
 
Back
Top Bottom