EWURA inatia aibu kufungia vituo vya mafuta visivyouza

sasa kama mdhibiti kwa nini ukifungie kituo kwa hisia zako! yaani hisia zikufanye ufunge kituo...badala ya kutafta suruhisho la kupunguza bei kwa kuingiza mafuta mengi au kupunguza ushuru ili supply iongezeke
 
tatizo wala haliko kabisa chini, Sema EWURA Wanawalinda hao importer labda hawakamatiki

Wameanza na vituo vinavyokataa kuuza mafuta na kama Importer nae ni sehemu ya huu mchezo wa uhujumu uchumi nae achukuliwe hatua za kisheria.

Lakini makosa ya importer hayampi mwenye kituo uhalali wa kuyumbisha uchumi wa nchi. Kila mmoja awajibike kwa mujibu wa vigezo na masharti ya license zao.
 
Labda huyapi mafuta uzito unaostahili,

chukulia mafuta kama vituo vya afya.

Chukulia vituo vya afya vya private vigome kutoa huduma kwasababu wanazojua wao, unadhani hali itakuaje?
basi uzito huo huo peleka na kwenye mafuta ndugu dmkali
Tofautisha mgomo na muda wa kufungua!

Hata vituo vya afya bianafsi vina haki ya kutoa huduma kwa MUDA AMBAO WANAJIPANGIA WAO WENYEWE!
 
Ewura washushe bei za mafuta halafu tuone kama vituo vitauza kesho au la..
 
sasa kama mdhibiti kwa nini ukifungie kituo kwa hisia zako! yaani hisia zikufanye ufunge kituo...badala ya kutafta suruhisho la kupunguza bei kwa kuingiza mafuta mengi au kupunguza ushuru ili supply iongezeke
Unachofanya ni kukwepa mishale.
Sababu ya kufungiwa ni greediness.
 
tofautisha mgomo na muda wa kufungua!
Hata vituo vya afya bianafsi vina haki ya kutoa huduma kwa MUDA AMBAO WANAJIPANGIA WAO WENYEWE!
Kama ni hivyo basi ukubaliane namimi katika hili.

Kama huduma zote muhimu zinatolewa bila kuzingatia taratibu zozote, hatuna haki ya kulalamika kwa chochote kile endapo kutatokea uzembe wowote ule unaofanywa na mtu yeyote yule iwe serikali au private sector.

Ukikubaliana na hilo basi ntakua pamoja nawewe kwenye hili.
 

“Badala ya kuongeza ruzuku….”

Nimesema hapa juzi mnataka kuongezewa ruzuku mmenogewa sasa mnataka kulamba mwiko na kuutafuna kabisa!

The ugliest part about all this drama ni kuwa Serikali/Viongozi kwa kiasi fulani inao/wanao mkono katika hii na ndio wanaipeleka inavyoenda!

Mnanyonya mpaka maji maji maana damu mshaikausha!
 
Ewura washushe bei za mafuta halafu tuone kama vituo vitauza kesho au la..
Yes hayo ndiyo yanatakiwa kufanywa na EWURA na hii ndiyo maana ya REGULATOR! Siyo kukamata watu kama mgambo!

Ewura wanatakiwa waoneshe Taaluma yao kudhibiti!
Kufungia ni ukoloni ambao hata asiyekwenda shule anaweza fanya kazi hiyo ya kufungia
 
Hivi ile pesa ya ruzuku mama alikuwa akitoa kila mwezi, imefikia wapi?
 
Kwaiyo usipouza mafuta Wakati yapo tu utarudisha hizo gharama?
 

Umechelewa kung’amua hili.

Hii mindset ipo katika kila sehemu inayotoa huduma kwa wananchi/wateja kote Serikalini na Sekta binafsi.

Watoa huduma wa Tanzania hujihesabu kama miungu watu na wapewa huduma hujiona kama wanapata msaada.

Ni Utu kusema “naomba” na “ahsante” lakini mtoa huduma wa Tanzania ukishampa maneno hayo umempa majipu ya kwapa anaanza na kukuvimbia kabisa.
 
Point nzuri sana.

Wanaozuwia mafuta ni wahujumu uchumi, wasinyimwe leseni pekee, wafungwe kwa kuhujumu uchumi.
Sisi raia tunapiga kelele kuhusu kupata huduma, sasa serikali inapochukua hatua kulinda walaji ni jambo la baraka sana.

Hawa watu wanatukwamisha malengo yetu ya kiuchumi. Fikiria ambulance inakosa mafuta huku ikiwa na mahututi. Ni mjinga pekee atakayewatetea hao wanaogoma kuuza mafuta
 
unataka wauze kila siku kwa kanuni ipi?
Kanuni za utoaji wa huduma za kijamii zinajulikana hata kama ni private sector,huwezi ukafunga/ kuacha kutoa mfano huduma ya elimu halafu ukasema kila jumanne na juma tano ni holday.
 
Nani anayetakiwa kuyafanya mafuta yashuke
 
MHUJUMU UCHUMI NI YULE Importer anaekutangazia Kwamba hajaagiza mafuta kwa uhaba gola!

mtu ambaye yupo dukani kwake muda wa kuuza unategemea na ratiba zake!
SWALA la muda ni hiari ya mfanya biashara
Hizo porojo zako tu, una mafuta kituoni uza, kama huuzi ni mhujumu uchumi.
 
MHUJUMU UCHUMI NI YULE Importer anaekutangazia Kwamba hajaagiza mafuta kwa uhaba gola!

mtu ambaye yupo dukani kwake muda wa kuuza unategemea na ratiba zake!
SWALA la muda ni hiari ya mfanya biashara
Ishu ni mafuta usiseme tu dukani kwake,cha msingi uza hadi yaishe ndio tujue tatizo lipo kwa main impoter siyo unaacha kuuza wakati yapo, bila hivyo umetumwa
 
Hoja nzito kabisa na yenye maslahi mapana kwa taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…