EWURA: Wasambazaji wa bidhaa mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara kuchukua bidhaa kutoka bandari ya Tanga pekee

EWURA: Wasambazaji wa bidhaa mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara kuchukua bidhaa kutoka bandari ya Tanga pekee

Tatizo msiojua kitu huwa mnaandika sana
Hivi unazan bei ya mafuta ya kichukuliwa Tanga na ya kichukuliwa Dar kwa mtumiaji wa Dongobesh,hydom,longido,Pasua na hata maramba ya Tanga zitapishanaa?
Kuna kitu hujui hii kitu inampango wa kuua biashara ya mafuta nchini
Wewe unaejua sana vitu tueleze vizuri umbali wa Dar Arusha na Umbali wa Tanga Arusha wapi karibu??? Serikali imesema lengo ni kupunguza gharama zisizokuwa na maana na ndio hizo, wewe professor unasema ooh lengo ni kuua biashara ya mafuta, zero mind...
 
EWURA imeagiza wasambazaji wote wa bidhaa za petroli mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara kuanza kuchukua bidhaa hizo kutoka Bandari ya Tanga, na si sehemu nyingine...
HAKI, UHURU NA MAENDELEO YA WATU. Tayari wauzaji wemenyanganywa uhuru wao wa kununua kwa wanayetaka
 
Wewe unaejua sana vitu tueleze vizuri umbali wa Dar Arusha na Umbali wa Tanga Arusha wapi karibu? Serikali imesema lengo ni kupunguza gharama zisizokuwa na maana na ndio hizo, wewe professor uchwara unasema ooh lengo ni kuua biashara ya mafuta, zero mind...
Hivi ushawahi kutoa mzigo bandarini?

Shida sio distance ndio maana nakuambia hata petrol station za tanga zinatumia mafuta ya dar Tatizo ni msururu wa vikwazo vya kibiashara.

Hizi biashara kubwa zina mambo mazito ambayo kama hujawahi shiriki utabaki kujiuliza why
 
Tatizo msiojua kitu huwa mnaandika sana
Hivi unazan bei ya mafuta ya kichukuliwa Tanga na ya kichukuliwa Dar kwa mtumiaji wa Dongobesh,hydom,longido,Pasua na hata maramba ya Tanga zitapishanaa?
Kuna kitu hujui hii kitu inampango wa kuua biashara ya mafuta nchini

Tatizo nyinyi wenye akili sana na ufahamu hapa jamvini mna majivuno na tambo sana, mnakashifu wasio na uelewa badala ya kuwaelekeza kwa ustaarabu. Haya hebu tuambie hatua hiyo itaua vipi biashara ya mafuta nchini?
 
Kama unajua kwa nini wafanyabiashara wanafuata mafuta DAR na sio Tanga tueleze,wakati Tanga ni karibu.Kama ni gharama kufuata mafuta Tanga kuliko Dar mseme sio kulaumu watu.Kama Deport Tanga hazitoshi si mseme au makampuni mengine hayana Depot ndio mseme sasa.Maana naona GBP ndio anadepot kubwa,Je PUMA,ORXY,OILCOM,TOTAL wanaDEPORT?
 
Ukute wengi wanakopeshwa dar
Sasa tanga labda wanataka cash
Ila biashara ni biashara tu
 
Wanaumia vipi?? wakati mwingine tuwe wakweli hivi unapochukua mafuta Dar ukauze Segera wakati Tanga ni Km 70 tu kutoka Segera na unaweza kuyapata Pale Tanga ni kipi bora?? maana ya serikali ni kuwa na maamuzi Mazuri ambayo yanasaidia watu wengi kwa pamoja na hilo ndio maana ya kuwainua watu. Kuwainua sio kuwapa mihela hilo halipo wala kuwambia kaaeni tu nyumbani bila kazi!!!
Ndugu huoni wewe umeshindwa kufikiri kwa kina? Jambo la kwanza hapa ni kutafuta sababu kwanini mtu anachukuwa mafuta Dar halafu anakwenda kuuza Segera wakati Tanga ni km 70 tu! Dara ni mbali hivyo kwa hali ya kawaida gharama itakuwa juu. Sasa kwanini mfanyabiashara anaamua kuingia gharama kubwa wakati kuna option ya kupunguza gaharama kwa kwenda Tanga? Je Tanga kulikuwa hakuna hii huduma? Haya ndiyo mambo ya mtu mwenye akili anatakiwa kujiuliza kabla hujaandika ulichoandika.
 
Usikimbilie kutukana
Hivi ushawahi kutoa mzigo bandarini?
Shida sio distance ndio maana nakuambia hata petrol station za tanga zinatumia mafuta ya dar Tatizo ni msururu wa vikwazo vya kibiashara
Hizi biashara kubwa zina mambo mazito ambayo kama hujawahi shiriki utabaki kujiuliza why
Yaseme hayo Mazito ili yajulikane ambayo Tanga Ni Mkoa wa Nchi hii unayo na Dar Hayapo na ni Nchi Moja
 
Kwa nini wanayafata sehem nyingine licha ya bandari ya Tanga kuwepo?.
We jamaa una bifu sana na tanga mara uiponde mara ivi kaa utulie tuachie kwetu bandari itatumika tu we endelea kuponda mara sio jiji mara ooh tulikuja kuomba kwenu mshamba kuwa mjanja usikimbilie majiji ya watu tanga raha we itakuwa wa moshi au arusha au msukuma tu mna chuki binafsi
 
EWURA imeagiza wasambazaji wote wa bidhaa za petroli mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara kuanza kuchukua bidhaa hizo kutoka Bandari ya Tanga, na si sehemu nyingine.

Atakayekiuka agizo hilo atatozwa faini TZS Milioni 100 au kifungo kisichopungua miaka 10, au vyote.



Mkuu wa nchii amesisitiza matumizi ya lugha yetu, hawa wanapingana naye, hivi wafanyabiashara wote hapa nchini ni waingereza?
 
Na waagizaji wa bidhaa zingine mseto waanze kutia maji kabla ya kunyolewa,tumeanza na bidhaa za mafuta na petroli
 
Back
Top Bottom