EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

Naona giant wote wamejikita kwenye biashara ya mafuta. Wacha tuendelee kuuza Sumu ya panya kwa kutembeza
 
Sasa si ajiuzulu kama anapelekeshwa
 
Mbona kipindi hiki hawajaandika yameongezeka kwa kiasi gani? Wametubandikia bei tu
 
Maelezo mengi umeruka swali la MSINGI ... Bei ya mwezi uliopita ilikuwa chini na bei ya soko duniani ilikuwa juu ...mind you (walisema stock IPO mpaka mwezi July) ..leo bei ya soko ipo chini bei imepanda ..msitufanye wajinga kiasi hicho kaka HIZO PRICE CEILING NA PRICE FLOOR ZIPO KWENYE MAZAO(product) YOTE ... HEDGING VILEVILE so usilete viterminology kufichia upigaji wenu....
 
Hiyo Bei ya $130 ilikaa siku 3 tu , na baada ya hapo yakashuka. Unataka kusema ndani ya hizo siku 3 ndio walinunua hayo mafuta?
Not necessary isipokuwa refinery zinakuwa na anticipation how much the prices are likely to rise and fall during the month utapewa average anticipate price or highest anticipated price.

Halafu usisahau hiyo ni bei ya crude for refined by products the price is even higher.
 
Sii kuwa yameshuka kidogo bali yako kama mwezi ulopita, mshangao ni hiyo bei imepandaje
Yameshuka kidogo, mwezi uliopita yalikua $110, Sasa hivi ni $106
 
Mafuta yameshuka duniani,. Kabla yalikua $126, ikaenda $110 na sasa ndio hiyo $106. Kwa hiyo yameshuka. Njoo na sababu zingine
126$ ilifika muda mdogo sana kama wiki tu mafuta kabla ya mwaka yalikuwa 60 kufika 106 ndio yamekaa muda mrefu lazima ujuwe hiyo ni bei ya crude sio refining products kikubwa fahamu mafuta hawanunui kila siku watu wananunua miezi mitatu mbele kama minada. Kama ilikuwa 126$ sasa bei zilikuwa bei gani kwetu? zilikuwa juu au? maana kama ilikuwa 126 kwa maneno yako basi wasifie serikali kuwa waliuza bei ya chini wakati huo. 126 ilifika short sana 100-106 imekaa kwa muda na hii ni brent sio wote wanazalisha standard ya brent yako ya bei ya chini tu. Kuna mafuta mpaka 80$ sasa hujiulizi kwanini yote bei moja kwenye refining. System yetu ya kutumia plat kwenye bulk ndio shida hata kama mtu kanunua huko chini ya plat kwa dola 10 huku wana calculate plat price ndio maana nasema hii system itazamwe upya ina kasoro nyingi haina ushindani.
 
Wanaposema stock ipo mpaka mwezi July ni kutokana purchase agreement zilizopo. Lakini uwezo wetu wa kuhifadhi mafuta sidhani kama unazidi mwezi.

Ebu muwe mnawasikiliza wanapotoa maelezo sio kuwa bias kuelewa kile mnachotaka nyinyi.

Ndio maana nchi hii kuna viongozi uwa wanaweza fafanua we mpaka inafika mahala wanachoka bora wafanye tu.

Walichosema kuhusu mafuta ya July yashanunuliwa so hayo itakuwa bei ya April, lakini aina maana yapo nchini tayari.

We elewa kwamba bei za Ewura ni nyuma mwezi + ya bei z soko.
 
Kwani tusinge shangilia Putin hasinge ivamia Ukraine.
 
Najua hiyo ni Bei ya crude, na wakishasafisha ndio inakuja sasa bei halisi
Lakini hij bei halisi ipo determined na bei ya crude. Ndio maaana crude ikupungua na mafuta yanapungua Bei. Ikipanda na mafuta Safi yanapanda pia.
 
Hiyo bei ya $126 ilikua mid March, kwa maeezo yako ya miezi mitatu nyuma basi Bei ilikua $90.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…