EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

Bei imetangazwa muda huu. Ingetangazwa mapema watu wangeendaa kununua
Wafanyabiashara wa jumla walijua ndio maana walificha mafuta wiki iliyopita .hali ni tete kwa mtanzania wa kawaida
 
Na bado

Hii hadi wapiga mapambio wa Lumumba waelewe
 
Unazungumzia nn ambacho mm nimekikataa? Crude oil ni lazima iwe refined, hii mbona ipo wazi.
Ila bei ya dunia inapigwa kwa crude oil, crude oil ikipanda mafuta Safi nayo yatapanda, ilishuka nayo yatashuka. Au unazungumzia nn?
Au unataka kusema crude oil leo ikishuka hadi $80 kwa pipa mafuta yanaweza yasishuke kwa sababu yanatakiwa kuwa refined?
Kuna post nimeandika kuhusu average costing za inventory na mambo ya procurement contract.

Wazalishaji wa mafuta yaliyosafishwa bei zao zinaangalia wastani wa gharama za mwezi mzima na other risk factors za muda husika kupanga bei awauzi kwa bei ya siku hadi siku.
 
Hatupo kuisifu Urusi...vita ndio sababu kubwa ya kupanda mafuta..
Kwa nini unamwangilia aliyefanya kitendo,angalia chanzo-chanzo cha matatizo yote ni NATO.hao NATO wasingekuwa wakorofi dhidi ya Russia hayo yasingetokea.
 
Kuna post nimeandika kuhusu average costing za inventory na mambo ya procurement contract.

Wazalishaji wa mafuta yaliyosafishwa bei zao zinaangalia wastani wa gharama za mwezi mzima na other risk factors za muda husika kupanga bei awauzi kwa bei ya siku hadi siku.
Sijui hata kama tunaelewana
 
Hata aweke 4000 watanzania nao wajua Mimi watalalamila siku chache tu watasahau...Kama mlivosahau tozo na kuona kawaida...nyie lalamikeni kesho mtazoea na mtasahau..
 
Soma tena ulichoandika na nilichokujibu.
Nimekuambia miezi mitatu nyuma bei ilikua $90, ikapanda hadi $126 Kati Kati ya Machi. Mwishoni mwa mwezi Machi Bei ikaanza kushuka, na ndio sasa ipo $106
Sasa haya uliyoeleza sijui unaeleza nn
Nimekwambia taja nchi moja duniani mafuta hayajapanda moja tu. Shida sio kupanda shida ni umaskini wetu. Nimekujibu bei 126 ni wiki moja tu average ni 96$ kutoka kwenye 60 sasa yamepanda au yameshuka kwa tafsiri yako.
 
Tukimlaumu Rais samia tunamuonea tu nina uhakika huyu mama mambo mengi ya Tanzania hayajui

Rais samia anamsikiliza mstaafu katika kuongoza nchi na teuzi nyingi anapangiwa na mzee na mama analipa fadhila kwani ndiye aliyempa umakamu wa Rais uliopelekea akaupata uRais

Ndugai yale maneno hakuropoka anajua nchi imeharibika

Hili kundi linaiba pesa litakalowafanya uchumi ubaki kwa watu 15 tu na ndio watakuwa na maamuzi ya siasa za Tanzania

Wameshamiliki chama
Wameshamiliki uchumi
Wameshamiliki media kubwa
Watamiliki nishati
Wanamiliki biashara

Magufuli umekufa na ndoto zako baba za kuifanya tanzania kuwa nchi ya usawa
Lazima tumlaumu yeye si ndio kiongozi
 
Mafuta yamepanda tena Bei, Dar Lita ya petrol kuanzia kesho ni 3148, dizeli 3258

View attachment 2210381

Bei za mafuta kuanzia April 4, 2022

Bei ya petrol kwa Dar itakuwa ni Tsh 3,148 kwa lita. Kwa watu wa Tanga watanunua kwa Tsh 3,161 na kwa watu wa Mtwara kwa 3,177 kwa lita.

Dizeli itauzwa Tsh. 3,258 kwa lita kwa Dar, na kwa Tanga watanunua kwa Tsh. 3,264. Mtwara watauziwa kwa Tsh. 3,309 kwa lita.

Mafuta ya taa hayako nyuma ambapo bei ya lita kwa Dar itakuwa Tsh 3,112. Mikoa mingine itakuwa na bei kutokana na hesabu zitakvyofanyika.

EWURA wamesema mabadiliko ya bei katika soko la dunia yamesababisha 93% ya mabadiliko ya bei

Bei za Jumla
PortPetrol
(TZS/Litre)
Diesel
(TZS/Litre)
Kerosene
(TZS/Litre)
DAR ES SALAAM3,015.883,125.182,980.56
TANGA3,028.723,131.39--
MTWARA3,044.883,176.87--

View attachment 2210436

View attachment 2210437

View attachment 2210438

View attachment 2210439

View attachment 2210440

0991F027-F761-4C2E-8DDB-66A8FB09A83D.jpeg
 
Kama ulisikiliza kipindi cha kipima joto kuhusu kupanda kwa bei ya walishaelezea mwezi wa tano bei zitaongezeka.

Sababu zilizotolewa ni za msingi kwa mfumo wa manunuzi, mafuta yanayotumika leo yalinunuliwa wakati bei ipo juu kidogo mwezi wa tatu.

All in all mfumo wa ‘bulk procurement’ inabidi waufanyie assessment una mazuri yake kwa upande wa serikali kuhakikisha wana uwezo wa ku control supply ni swala muhimu kwa usalama wa uchumi.

Alikadhalika una mapungufu yake kwenye procurement strategies, kununua kwa mwezi kuna wanyima waagiza advantage za price hedging.

Ukiwa reliable buyer unaweza strike long term deals za miezi sita ata mwaka (depending na muuzaji) kupata mafuta kwa bei za price ‘ceiling and floor’ bei zikipanda na kushuka chini ya bei za soko.

Kwa sasa Bulk procurement inazuia advantages hizo pamoja na ushindani wa biashara.

mfanyabiashara inakuwa ngumu kutumia average costing za inventory ajipe advantage sokoni kupambana na ushindani au kutumia mbinu zingine za kujipa advantage.

Unaweza elewa kwanini serikali iliamua kwenda na Bulk procurement kutokana na masahiba ya huko nyuma kushindwa ku monitor reserves and supplies; but surely inahitajika amendments kwenye supply control baada ya kuwasikiliza na kuwaelewa umuhimu wake lakini huu mfumo unaondoa ubunifu pia wa ushindani na kupata good deals sokoni.

Kuna mambo ya taasisi kufanya overlapping works na zenyewe zinategemea tozo za mafuta, serikali kujitwika mzigo wa investment kwenye mabomba ya kupokea mafuta wakati port inatumiwa na rwanda, Burundi, congo, Zambia ata wao mafuta yao yakija meli zao zina wa-charge demmurage za siku. So kuna investments ambazo na wao wanaweza changia bure it’s in their interest too.

Hii nchi ina mambo mengi vitu vingine ukisikiliza unashindwa kuelewa baadhi ya watu hizo nafasi wamezipata vipi, ukiwasikiliza hawana majibu kabisa ya changamoto za sector zao zaidi ya kuongelea mambo ya kukariri.
Hii Nchi inahitaji Rais mwenye akili zaidi ya Nyerere na mwendawazimu zaidi ya Magufuli lasivyo hakuna chochote tuta achieve kama Nchi.Tatizo kubwa ambao wanatakiwa wafanye maamuzi wa hayo mambo uliyo suggest hapo ndio hao hao wanufaika na hizo biashara-what do you expect??.

Mfano mzuri karibu Nchi 6-8 mafuta yao yanapita katika bandari yetu,tunaweza kutumia charges za shehena za mafuta yanayopita kwetu kwenda hizo Nchi na Yale mafuta yetu tukaweka tozo kidogo sana.

Hii Nchi tunakwamisha na viongozi wetu-na sisi tupo kama mazezeta hatufanyi chochote.
 
Sijui hata kama tunaelewana
Mimi nakuelewa sema wewe labda ndio unielewi.

Nimekueleza bei ya mwezi mzima kwa wasafishaji inakuwa gauged with average costing not FIFO. So mwezi wa tatu on average bei ilikuwa juu zaidi.

Good Morning 👋
 
Mafuta kwenye soko la dunia yameshuka kidogo, Ila huku Bei imepanda. nadhani unaelewa nn kinaendelea
Mafuta tunayotumia mwezi huu wa tano yamenunuliwa mwezi wa tatu ambapo yalikuwa yameanza kupanda baada ya vita, na bado ya mwezi ujao yatakuwa juu zaidi maana ni yale ambayo bei ilipita USD 113+ per barrel [emoji28][emoji28][emoji28] so tujiandae tu
 
Hii Nchi inahitaji Rais mwenye akili zaidi ya Nyerere na mwendawazimu zaidi ya Magufuli lasivyo hakuna chochote tuta achieve kama Nchi.Tatizo kubwa ambao wanatakiwa wafanye maamuzi wa hayo mambo uliyo suggest hapo ndio hao hao wanufaika na hizo biashara-what do you expect??.

Mfano mzuri karibu Nchi 6-8 mafuta yao yanapita katika bandari yetu,tunaweza kutumia charges za shehena za mafuta yanayopita kwetu kwenda hizo Nchi na Yale mafuta yetu tukaweka tozo kidogo sana.

Hii Nchi tunakwamisha na viongozi wetu-na sisi tupo kama mazezeta hatufanyi chochote.
Tatizo lao wana elimu ya kukariri sio ya ubunifu.

Magufuli was special and the good die earlier.
 
Back
Top Bottom