EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

Kwa nini unamwangilia aliyefanya kitendo,angalia chanzo-chanzo cha matatizo yote ni NATO.hao NATO wasingekuwa wakorofi dhidi ya Russia hayo yasingetokea.
NATO wana majeshi Ukraine? Wanaua watoto na wanawake? Wanapiga makombora shule na hospitali?..
 
Acha upuuzi wewe. Rais anahusika pakubwa sana. Chini ya jiwe hali isingefika huku hata kidogo
Chini ya Jiwe kivipi wote wale wale tu kwani huo mfumo wa ununiaji mafuta kwa bulk purchase si aliuleta yeye Magufuli,alitaka kila kitu ifanye Serikali.
Tena huyo Magufuli wenu ndio yangepaa mpaka 10,000.
 
Tatizo lao wana elimu ya kukariri sio ya ubunifu.

Magufuli was special and the good die earlier.
Magufuli ndio alioleta huo mfumo wa bilk purchase,kwa kigezo kuwa wafanyabiashara walikuwa wanapandisha bei za mafuta kiholela holela-so haya tunayoyazungumza ni matunda yake.
 
Wewe taarifa zako unatoa wapi mzee? Tuwekee reference hapa
Reference si hata we tu unaweza kuipata?
Bei kushuka unataka nayo uwe Siri?
Screenshot_20220503-214944_1.jpg
 
Mafuta yameshuka duniani,. Kabla yalikua $126, ikaenda $110 na sasa ndio hiyo $106. Kwa hiyo yameshuka. Njoo na sababu zingine
Hapa sababi kubwa ni uongozi,na kibaya zaidi uongozi huo ndio unaofanya hizo biashara.
 
Nimekwambia taja nchi moja duniani mafuta hayajapanda moja tu. Shida sio kupanda shida ni umaskini wetu. Nimekujibu bei 126 ni wiki moja tu average ni 96$ kutoka kwenye 60 sasa yamepanda au yameshuka kwa tafsiri yako.
Uwe unatumia akili. Mafuta yalipanda huko kwenye soko la dunia, na huku yakapanda na kufika hiyo 2800+ , ila huko kwenye soko la dunia yameshuka inapaswa na huku kushuka Ila badala yake yamepanda
Hapo kipo kigumu?
 
Mafuta tunayotumia mwezi huu wa tano yamenunuliwa mwezi wa tatu ambapo yalikuwa yameanza kupanda baada ya vita, na bado ya mwezi ujao yatakuwa juu zaidi maana ni yale ambayo bei ilipita USD 113+ per barrel [emoji28][emoji28][emoji28] so tujiandae tu
Mwezi ujao yatakua juu zaidi kivipi ikiwa bei zimeshuka?
Na haya maajabu yapo Tz tu? Kenya Lita ya petrol ni 2800, dizeli 2500
Tanzania 3140, dizeli 3250.
Wenzetu nyie ni wafaidika wa hizi bei?
 
Chini ya Jiwe kivipi wote wale wale tu kwani huo mfumo wa ununiaji mafuta kwa bulk purchase si aliuleta yeye Magufuli,alitaka kila kitu ifanye Serikali.
Tena huyo Magufuli wenu ndio yangepaa mpaka 10,000.
Umekosea mfumo wa bulk ulikuja wakati wa kikwete 2011.
 
Magufuli ndio alioleta huo mfumo wa bilk purchase,kwa kigezo kuwa wafanyabiashara walikuwa wanapandisha bei za mafuta kiholela holela-so haya tunayoyazungumza ni matunda yake.
Ni uongo. Mfumo wa Bulk ulikuja 2011
 
Ungekua ni ule utawala wa Mwendazake angetujibu simple tu kuwa yeye hajasababisha vita huko Urusi na Ukraine . Na wote mngetulia hapa.
 
Mafuta yamepanda tena Bei, Dar Lita ya petrol kuanzia kesho ni 3148, dizeli 3258

View attachment 2210381

Bei za mafuta kuanzia April 4, 2022

Bei ya petrol kwa Dar itakuwa ni Tsh 3,148 kwa lita. Kwa watu wa Tanga watanunua kwa Tsh 3,161 na kwa watu wa Mtwara kwa 3,177 kwa lita.

Dizeli itauzwa Tsh. 3,258 kwa lita kwa Dar, na kwa Tanga watanunua kwa Tsh. 3,264. Mtwara watauziwa kwa Tsh. 3,309 kwa lita.

Mafuta ya taa hayako nyuma ambapo bei ya lita kwa Dar itakuwa Tsh 3,112. Mikoa mingine itakuwa na bei kutokana na hesabu zitakvyofanyika.

EWURA wamesema mabadiliko ya bei katika soko la dunia yamesababisha 93% ya mabadiliko ya bei

Bei za Jumla
PortPetrol
(TZS/Litre)
Diesel
(TZS/Litre)
Kerosene
(TZS/Litre)
DAR ES SALAAM3,015.883,125.182,980.56
TANGA3,028.723,131.39--
MTWARA3,044.883,176.87--

View attachment 2210436

View attachment 2210437

View attachment 2210438

View attachment 2210439

View attachment 2210440
Tozo, tozo, tozo...
Culprit ni serikali kupitia utitiri wa Tozo!
Mi-5 tena🙄
 
Ungekua ni ule utawala wa Mwendazake angetujibu simple tu kuwa yeye hajasababisha vita huko Urusi na Ukraine . Na wote mngetukia hapa.
Labda huko kwingine Ila kwa JF tungesema tu. Jf ni sehemu ambayo haijawah kunyamazishwa
 
Uwe unatumia akili. Mafuta yalipanda huko kwenye soko la dunia, na huku yakapanda na kufika hiyo 2800+ , ila huko kwenye soko la dunia yameshuka inapaswa na huku kushuka Ila badala yake yamepanda
Hapo kipo kigumu?
Uko sahihi, mwezi wa tatu mafuta yalipanda hadi dola 123 kwa pipa huku bei ilipanda pia hadi shilingi 2800 kwa lita, kutoka mwezi wa tatu mafuta yalianza kushuka hadi yamefika dola 105 kwa pipa leo hii, lakini kwetu badala ya kushuka yamepanda.
 
Hii Nchi inahitaji Rais mwenye akili zaidi ya Nyerere na mwendawazimu zaidi ya Magufuli lasivyo hakuna chochote tuta achieve kama Nchi.Tatizo kubwa ambao wanatakiwa wafanye maamuzi wa hayo mambo uliyo suggest hapo ndio hao hao wanufaika na hizo biashara-what do you expect??.

Mfano mzuri karibu Nchi 6-8 mafuta yao yanapita katika bandari yetu,tunaweza kutumia charges za shehena za mafuta yanayopita kwetu kwenda hizo Nchi na Yale mafuta yetu tukaweka tozo kidogo sana.

Hii Nchi tunakwamisha na viongozi wetu-na sisi tupo kama mazezeta hatufanyi chochote.
You are right. Lakini niseme, tunahitaji mifumo bora ya kuwawajibisha viongozi. Kwa sasa kila kiongozi anafanya yake akijua hakuna consequences. Ok. Unahitaji mwendawazimu kuliko JPM. Swali ni vipi maamuzi yake yanalenga kumkomboa mwananchi wa kawaida? JPM was basically above the law na wote tukakubali (hatukuwa na namna) kwa kivuli kwamba anajenga uchumi. Lakini alitumia nguvu kubwa kujiimarisha kimamlaka kwa kuwaumiza wapinzani wake. Mimi sioni kuzuia bunge live, kuwafunga mdomo wapinzani, kuzuia uhuru wa kawaida na habari ulivyolinufaisha taifa. In fact ufisadi kipindi cha JPM ulishamiri. Ingawa haukuandikwa popote kwa sababu hakuna gazeti lililokuwa na courage ya kufanya hivo.
Mwisho wa siku viongozi wetu inabidi watambue kwamba wakifanya madudu wataadhibiwa kwa sanduku la kura au kwa sheria hata wakitoka madarakani. Kwa sasa baadhi ya wananchi na elites wanaofaidi nchi wanaona katiba ni agenda ya wapinzani. Lakini tunashindwa kuelewa katiba mbovu inatuathiri sote. Leo mtu anaweza kuja na maamuzi ya ajabu kweli kweli...na hakuna atakapowajibishwa. Siasa za kiimla na kukosa uwajibikaji haziwezi kutupa nafuu ya maisha kamwe.

Angalia akina Kinana, Membe nk..walionja joto ya jiwe kipindi cha JPM. Ungetegemea baada ya kupata second chance ndo wapambanie mifumo bora....lakini wapi....they are eating! Tanzania ufisadi haukuwahi kuisha wala kupungua. Tofauti ni kwamba JPM alifanikiwa kuuficha usiandikwe na Samia karuhusu ulipotiwe.
 
Tunalipia madhara ya vita!!...

Halafu kuna watu wanasifia Urusi kuvamia nchi nyingine....
Waoga na wanafiki waliokimbilia vikwazo ndiyo walaumiwe.Walipaswa kuingia uwanja wa vita kumpiga Urusi na siyo kuweka vikwazo kwa mtegemewa.
 
Upandaji wa bei ya mafuta safari hii una utata mkubwa kwa sababu kwenye soko la dunia bei imeshuka kutoka dola 123 kwa pipa mwezi machi hadi dola 105 kwa sasa lakini huku kwetu bei imepanda zaidi.
 
You are right. Lakini niseme, tunahitaji mifumo bora ya kuwawajibisha viongozi. Kwa sasa kila kiongozi anafanya yake akijua hakuna consequences. Ok. Unahitaji mwendawazimu kuliko JPM. Swali ni vipi maamuzi yake yanalenga kumkomboa mwananchi wa kawaida? JPM was basically above the law na wote tukakubali (hatukuwa na namna) kwa kivuli kwamba anajenga uchumi. Lakini alitumia nguvu kubwa kujiimarisha kimamlaka kwa kuwaumiza wapinzani wake. Mimi sioni kuzuia bunge live, kuwafunga mdomo wapinzani, kuzuia uhuru wa kawaida na habari ulivyolinufaisha taifa. In fact ufisadi kipindi cha JPM ulishamiri. Ingawa haukuandikwa popote kwa sababu hakuna gazeti lililokuwa na courage ya kufanya hivo.
Mwisho wa siku viongozi wetu inabidi watambue kwamba wakifanya madudu wataadhibiwa kwa sanduku la kura au kwa sheria hata wakitoka madarakani. Kwa sasa baadhi ya wananchi na elites wanaofaidi nchi wanaona katiba ni agenda ya wapinzani. Lakini tunashindwa kuelewa katiba mbovu inatuathiri sote. Leo mtu anaweza kuja na maamuzi ya ajabu kweli kweli...na hakuna atakapowajibishwa. Siasa za kiimla na kukosa uwajibikaji haziwezi kutupa nafuu ya maisha kamwe.

Angalia akina Kinana, Membe nk..walionja joto ya jiwe kipindi cha JPM. Ungetegemea baada ya kupata second chance ndo wapambanie mifumo bora....lakini wapi....they are eating! Tanzania ufisadi haukuwahi kuisha wala kupungua. Tofauti ni kwamba JPM alifanikiwa kuuficha usiandikwe na Samia karuhusu ulipotiwe.
Umesema kweli kabisa nguvu ilitumika kuzuia waandishi.
Ila pia sasa hivi kusema Samia karuhusu waandike ufisadi ni uongo. Kilichopo sasa hawatumii nguvu bali pesa.
Jana tu katoka kusema huwa wanamuomba pesa, na anawapa.
 
Back
Top Bottom