Ngao ya Sponji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2018
- 341
- 542
Wizara Ya Fedha na Wizara Ya Nishati zinabidi zijitafakari sana! Nategemea Rais aliongelee hili na Alitolee ufafanuzi wa Kueleweka, Hii ni Hujuma kabisa Kwa Wananchi wenye Kipato Cha Chini. Tuliambiwa Nchi Ina stock ya Kutosha ya Mafuta imekuaje Bei kupanda Kiholela namna Hii?Leo nimeenda kujaza mafuta ya dizeli kwenye gari langu nikitumaini kuwa bei niliyoizoea ni Tshs.2842 kwa lita hapa Mwanza. nilipotoa fedha ya lita 20 yaani Tshs.56,840 nikaitwa ili niongeze hela. Nikawa mbogo nikaambiwa unatakiwa kulipia Tshs.68,040. Tofauti ya Tshs.11,200. Bado ninajiuliza kuwa juzi ndo Latra iliwaongezea wamiliki wa vyombo vya usafiri gharama zao za nauli, itakuwaje tena jana bei tena zimeongezeka. Je itabidi waongezewe bei tena?. Vile vile bei ya dizeli ndo imeongezeka kuliko hata petroli ni kwa sababu gani?. Itakuwa vema kama Serikali ingekuwa inatoa elimu kwa wananchi kupitia luninga kwa vigezo ni kwa nini bei ya mafuta imepanda kwa kipindi husika. Tukiendelea hivi Serikali iliyo madarakani itaendelea kuchuchukiwa sana na wananchi.
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app