EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta zinazoanza kutumika Juni Mosi

EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta zinazoanza kutumika Juni Mosi

Baada ya Selikari kutangaza ruzuku kwenye mafuta baadaye tulipata kusikia pia bei ya mafuta duniani imeshuka kiasi.
.
Hivyo kuongeza na hii ruzuku tulitegemea bei ingerudi kama awali lakini kinachoonekana ni mabadiliko ni kidogo sana kuliko yalivyopanda nini hasa shida Wakuu?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Yaani nashangaa watu hawaelewi nn hapo,ni kwamba inonekana bei inazidi kupanda na mwezi huu ingekua Tshs 3000 kwa dar,lkn ruzuku imeishusha na kua Tsh 2994.
Mbona hesabu rahisi iyo mnakwama wapi kuelewa??
Ni ruzuku ya Tshs 300
Soma tena ulochoandika
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya ya mafuta zinazoanza kutumika Juni mosi, huku kukiwa na unafuu kutoka na ruzuku ya shilingi Bilioni 100 iliyotolewa na Rais Samia mapema mwanzoni mwa mwezi huu...
Hakuna punguzo hapo. Hiyo ni danganya toto. Kesho kutwa tu watapandisha tena kufikia hiyo hiyo elfu tatu na kitu. Wana siasa hawawezi kuongoza nchi wameshindwa kabisa. Vitu vinapanda bei kila siku!!!!!
 
Hizi ni ngonjera flani hivi.
Walijua watatoa ruzuku kwa nini wapaishe nauli?

Leo wamepunguza bei issue ya nauli inasimamia wapi?.
Kama unakumbuka vizuri nauli zilipandishwa bei ya mafut ilipopanda na kufikia 2800 na kitu hivi. Hatukupiga kelele. Ilivyopanda mpaka 3300 na kitu ndipo watu wakapiga kelele. Nauli haiwezi kushushwa kwa vile ilipanda kipindi cha 2800 na kitu.
 
SAWA,ILA WAPUNGUZE NAULI SASA
MAANA SISI WENGINE HATUNA VYOMBO VYA MOTO TUNATEGEMEA USAFIRI WA DALADALA NA BODABODA

Ova
 
#NISAMIATENA EWURA kuweka bei kikomo ya mafuta inayotokana na Ruzuku ya Bilioni 100 iliyowekwa na serikali ili kuleta ahueni ya bei ya mafuta Nchini.
@SuluhuSamia
#UVCCMDSM
#Ewura
#SSH #KaziIendele
#jiandaekuhesabiwa
#ShirikiUchaguziKwaUadilifu
Screenshot_20220601-135203.jpg
 
Yamekuwa maji ya kunywa.
Mtakatiliwa mbali, na Bei zitashuka.

Viongozi Wanafanya biashara za mafuta na kuagiza mafuta ndo wahujumu wa wananchi kupata ahueni ktk Bei za mafuta na bidhaa.


Siku inakuja. Amen
 
Back
Top Bottom