EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta zinazoanza kutumika Juni Mosi

EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta zinazoanza kutumika Juni Mosi

Yaani nashangaa watu hawaelewi nn hapo,ni kwamba inonekana bei inazidi kupanda na mwezi huu ingekua Tshs 3000 kwa dar,lkn ruzuku imeishusha na kua Tsh 2994.
Mbona hesabu rahisi iyo mnakwama wapi kuelewa??
Ni ruzuku ya Tshs 300
 
Hi
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya ya mafuta zinazoanza kutumika Juni mosi, huku kukiwa na unafuu kutoka na ruzuku ya shilingi Bilioni 100 iliyotolewa na Rais Samia mapema mwanzoni mwa mwezi huu.

Bei mpya zilizotangazwa na EWURA zinaonesha kuwa petrol itauzwa 2994 badala ya 3301 punguzo la Shilingi 306 huku Dizeli ikiuzwa kwa 3131 badala ya 3452, punguzo la 320 kwa mkoa wa Dar es Salaam.

View attachment 2246240View attachment 2246241View attachment 2246242
Hiyo ela ya ruzuku bora wangenipa tu nifanyie mambo yangu maana sioni cha maana hapo.
 
Siyo kwa Tanzania aseee, leo kuna binti kalipa nauli 2000 alipanda kituo A akashuka kituo D konda kamrudishia 1000 binti kadai 500 konda hakumjibu kagonga gari ikaondoka, abilia wengine wakapotezea.
😂
Nasikia hiyo ndo nauli 'halali' ya kutokea Kawe kukanyaga mafuta!
 
Hiyo ruzuku kwa mafuta ya Tanga haijafanya maajabu.
 
Hizi ni ngonjera flani hivi.
Walijua watatoa ruzuku kwa nini wapaishe nauli?

Leo wamepunguza bei issue ya nauli inasimamia wapi?.
Gharama za maisha zilipanda
 
Tengeneza tatizo, tatua tatizo, pata ujiko
 
Zanzibar bei zipoje?
Kwa Znz huwa hakuna sarakasi nyingi kwenye bei za mafuta.. Tofauti na Tanganyika ambapo kila Lita 1 ya mafuta ina utitiri wa Kodi na tozo mbali mbali zaidi ya 20🤔🙄 Wakati Bara bei ikiwa zaidi ya 3,000, Znz ilikuwa 2,600.
Kama nao wamepewa hiyo 'ruzuku' basi bei yao itakuwa poa!
 
Mikoa yenye bandari ndio bei imeshuka kwenye petroli ipo chini ya 3000 lakini Mikoa mingine petroli ni kuanzia 3000 kwenda juu.
Ukiangalia kwenye chati sehemu ambayo petroli inauzwa chini kabisa ni muheza Lita moja inauzwa 2990
Sehemu nyingine bado maumivu ni yaleyale
 
Nilitegemea hili!

Hakuna lolote la maana kwa watumiaji wa mwisho!
 
Mimi huwa najiuliza haya makato sijui ya EWURA na TBS ni ya nini? pesa hizi wanazifanyia nini? hawa ni watumishi wa serikali wako kwenye payroll hata kama wamelala hawana kazi.

Hizi pesa huwa wanazifanyia nini? kwa kazi gani? ku regulate bei tu? huwa najiuliza sipati jibu kama kuna mtu anajuwa hebu atueleze wanakusanya za nini? mishahara yao? hata mishahara mbona pesa ndefu inakusanywa inaenda kwenye matumizi gani?
 
Back
Top Bottom