EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta zinazoanza kutumika Juni Mosi

EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta zinazoanza kutumika Juni Mosi

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya ya mafuta zinazoanza kutumika Juni mosi, huku kukiwa na unafuu kutoka na ruzuku ya shilingi Bilioni 100 iliyotolewa na Rais Samia mapema mwanzoni mwa mwezi huu.

Bei mpya zilizotangazwa na EWURA zinaonesha kuwa petrol itauzwa 2994 badala ya 3301 punguzo la Shilingi 306 huku Dizeli ikiuzwa kwa 3131 badala ya 3452, punguzo la 320 kwa mkoa wa Dar es Salaam.

View attachment 2246240View attachment 2246241View attachment 2246242
[emoji848]
 
Kenyata alitoa zaid ya 100 bilion na mafuta bado ni Ksh 150 = TSh 2988 kwa pesa ya Tanzania

Tunazungumzia uchumi wa Tanzania au kenya?? Yani Kodi zilizopo kwenye mafuta ni 51% ya bei. Manake hata wese likiuzwa 2500 serikali bado inapata kodi nyingi tu.
 
Ujinga sio huo tu, hii Dar, ni sehemu gani mafuta ya Petrol yalikuwa yakiuzwa kwa sh 3,301?

Nieleweshwe ninapokwama kwenye hizi namba, mimi kila nilikopita nikiona mabango yakisema sh 3,148 na sehemu chache sh 3,140.

Sasa hilo punguzo la sh 306 linatoka wapi ikiwa wameshusha kufikia sh 2,994? Ambapo pia ukijumlisha hizo namba mbili siipati hiyo 1 mwisho mwa 3301.

2994 + 154 = 3,148

Punguzo ni sh 154 kwa Dar. Sh 152 zimekwenda na maji.

Wahuni washakwenda nazo tayari[emoji28][emoji119]
 
Hata kama kweli hiyo 100bn imetoka, basi hesabu inasema karibu 40bn imekwenda kwa maji!

Kulikua hakuna haja ya kutoa hizo pesa wakati mchawi alikua kodi, serikali ingepunguza makodi yake yasiyokua na maana kuna kodi zingine ni kutukandamiza tu. Hakuna pesa iliyotoka wanacheza na mind zetu tu, ili mseme mama anaupiga mwingi
 
Kulikua hakuna haja ya kutoa hizo pesa wakati mchawi alikua kodi, serikali ingepunguza makodi yake yasiyokua na maana kuna kodi zingine ni kutukandamiza tu. Hakuna pesa iliyotoka wanacheza na mind zetu tu, ili mseme mama anaupiga mwingi
Inawezekana zimetoka kweli ila zikaingia kwao kisha wakawaambia baadhi ya watoza ushuru kuwa ile 100bn inatokana na ile tozo yenu hivyo sahauni hiyo kitu.

Ikawa, 100bn imetoka mfuko mkuu na wao kugawana ili waendeleze ufalme kwa pisi na escorts kutoka bongo movie, na tozo moja kupigwa stop; two in one.
 
wale inawezekana hawaendi haja, haiwezekani kwa kufikiri na kuamua namna hiyo..alafu wanakuja jipigia makofi lundo. Uchafu ukikaa sana mwilini unaathiri ufanyaji kazi wa ubongo
 
Msoga Jazz Band-walamba asali leo tupo Ukumbi wa EWURA.Nchi ngumu hii,akiiweka sana kichwani utaishia kunywa painkillers kupunguza maumivu ya kichwa.
 
Back
Top Bottom