EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta zinazoanza kutumika Juni Mosi

EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta zinazoanza kutumika Juni Mosi

Zaidi ya dar kote mafuta yatakuwa 3000+ hapo ndio wameshusha kwa mbwewe hakuna kipya..
Kwani nchi jirani kama Zambia na Kenya wanafanyaje mafuta yanakuwa bei rahisi kuliko Tanzania, au wao wana visima vyao vya mafuta?!!
 
Bado ipo juu sana, haitapunguza bei ya mafuta ya kula tuunge Dagaa.
 
Kwahiyo tunaposema bil 100 za Samia zilipaswa kupunguza bei ya mafuta kwa zaidi ya sh 300 usituletee utetezi kwa kuleta mfano wa nchi ya Kenya.
Maana yangu ni kuwa wamejitahidi kupunguza hata kufikia 300
 
Mama anajua anaujua mpaka anajua tena kama mpaka sasa hujamuelewi poga kifua na useme mimi ni mchawi
 
Bado ipo juu sana, haitapunguza bei ya mafuta ya kula tuunge Dagaa.

Ndio maana nasema kuwa hizi hela zimeliwa tuu hakuna kilichopungua chochote....hivi ni kwanini wasingeondoa mlolongo wa tozo zilizopo kwenye mafuta halafu wakajisifu? Hivi unatoa billion 100 halafu unapunguza 300? Yani sasa hilo punguzo likowapi?
 
Bei mpya za mafuta zinatarajiwa kuanza kutumika kesho, Jumatano Juni 01, 2022 ambapo zimeshuka tofauti na ilivyokuwa awali.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kuwa Dar es Salaam bei ya Petroli itakuwa ni Tsh. 2,994 badala ya Tsh. 3,301, Dizeli Tsh. 3,131 badala ya Tsh. 3,452.

Tanga petroli imeshuka kwa Tsh. 152 kwa lita na dizeli kwa Tsh. 486 kwa lita, Mtwara petroli imeshuka kwa Tsh. 282 kwa lita na Dizeli kwa Tsh. 486 kwa lita.
284647744_1054214661871144_3150028045884811782_n.jpg

284672034_1190805241732610_8522411232290400189_n.jpg

284839295_523545789481113_2056039119639996198_n.jpg

284910293_1080288702567863_8612971790789927181_n (1).jpg

284910293_1080288702567863_8612971790789927181_n.jpg

284968210_507257891190332_1422611573046186501_n.jpg
 
Nauli,Nauli,Nauli,kuanzia kesho nalipa 400 kwenye daladala.
 
Sijawahi kuona raia wapumbavu kama Watanzania asee. Yani mnashangilia eti "mama anaupigwa mwingi?" Hizo Billion 100 amezitoa mfukoni mwake au?

Aaahh huu ni ujinga mkubwa kabisa.
Ujinga sio huo tu, hii Dar, ni sehemu gani mafuta ya Petrol yalikuwa yakiuzwa kwa sh 3,301?

Nieleweshwe ninapokwama kwenye hizi namba, mimi kila nilikopita nikiona mabango yakisema sh 3,148 na sehemu chache sh 3,140.

Sasa hilo punguzo la sh 306 linatoka wapi ikiwa wameshusha kufikia sh 2,994? Ambapo pia ukijumlisha hizo namba mbili siipati hiyo 1 mwisho mwa 3301.

2994 + 154 = 3,148

Punguzo ni sh 154 kwa Dar. Sh 152 zimekwenda na maji.
 
Back
Top Bottom