EWURA yatangaza bei mpya za mafuta ya Julai, 2022. Petroli, Dizeli zapanda

EWURA yatangaza bei mpya za mafuta ya Julai, 2022. Petroli, Dizeli zapanda

Kuna watu bado mnaiamini CCM eti bei ingeshuka?

Kama waliweza kuingiza kura zilizopigwa tayari kwenye mabegi na vkapu mchana kweupe na polisi wakiwepo watashindwa kuwazuga eti kuna ruzuku?
Nchi inaendeshwa kimchongo mchongo
 
Huoni sahv kuna kasi kubwa sana
Ya vituo vya mafuta kujengwa....
Njiaa ya tandale kuna vituo vingi vya mafuta, pita goba uone napo
Tokea magomeni kwenda moroco ona
Napo,njia ya kwenda kawe pale mlalakuwa jeshini napo kuna kituo kinawekwa,haya njia panda ya kawe maringo kuna kituo kinawekwa..

Mafuta deal

Ova
Kutoka mbezi mpaka kinyerezi kuna vituo vya wese si chini ya 6,now ni mwendo wa vitz tu
 
Awamu hii KILA kitu bei juu sio soda, mkate, dawa, bidhaa zote , halafu pesa Hakuna ukiipata haina thamani,
Elf 10 ni SAwa na mia 500.
Magu pesa ilikuwa ngumu kupata lakini vitu bei chini.
Yule jamaa pale wizaarani anachojua ni kuongeza sifuri tu kwenye bajeti, hana ubunifu kabisa wa kubuni chanzo vya mapato zaidi ya kukamua wananchi.
Bado aumize kichwa namna ya kupambana na mfumuko wa bei yeye ndio anatamani tozo ziongezeke hadi kwenye ving'amuzi kuzidi kuwaongezea mzigo wananchi,halafu kituko sasa anataka kupunguza kodi kwenye kamari!
 
Mkuu, Sio inawezekana

Nawaambieni, Petrol kufikia mwezi wa 1 -2 , Petrol itauzwa 10K.
Mimi natamani Sana ifike hiyo Bei ili kila kitu kisimame ndo wananchi tutapata akili ya kujua nyeusi na nyeupi maana kwa sasa KIJANI wamejimilikisha nchi wanafanya wanachotaka kwa kujua wananchi wengi karibu wote MAZUZU.
 
Hamna Kiongozi pale .. ni hewa kabisa, mtupuuuu .


Ukimuuliza Bilion 100 zimefanya nn?? Sasa mwezi wa nane ,wanatangaza Tena mpya..mwezi wa kumi, kumi na mbili , mwakani yaan Kila baada ya miezi miwili EWURA haoooo!!


Hamna kitu, tumepigwa Sanaa, kwenye nyakati kama hizi za Crisis Huwa UNAHITAJIKA KUA NA RAIS MWENYE AKILI, MBUNIFU, MISIMAMO, MWENYE UTHUBUTU NA KUJIAMIN ,MZALENDO .!!



SASA KAMA WAFANYABIASHARA WANDANI SAHIZI BEI WANAJIPANGIA WANAVYOTAKA, NCHI IMEKOSWA BEI ELEKEZI ,,,, ATAWAWEZA HAWA MABWANYENYE!????



Tukisema Magufuli Alikua Mwamba, muwe mnatuelewa !!.
Sawa kwa mtazamo wako Ila naye ni moja ya Viongozi walioharibu uchumi wetu kuliko uhalisia ya yanayosemwa, Jambo pekee naweza msifu Magufuli ni miundombinu na maamuzi magumu(japo Kuna wakati alitanguliza Chuki na ubaguzi) Kama angerekebisha hapo na kutawala kwa usawa nadhani angeweka rekodi ambayo kuvunjwa kwake ingechukua miaka zaidi ya 50.
 
Magufuli angeenda kupigana Huko ukraine?

Huyo unayemuita mwamba alikuta sukari Chini ya 2000 akaipandisha bei mpaka karibia 3000 haku kuwa na Vita wala Tatizo lolote,

Mazao ya wakulima kama mbaazi yakashuka mpaka kilo 200 watu wamemsusia.

Akaenda Korosho zao aliloliacha Kikwete kama dhahabu linaingizia Nchi mabilioni ya Hela akaliharibu haribu watu wakamsusia.

Tumbaku na Vitu kibao aliharibu.

Tatizo la Watanzania uwezo wenu wa kukumbuka ni siku 5 tu nyuma.
Unafki ndo Jambo tunaloliweza sisi wantanzania watu wanasahau mapema Sana...Magufuli alipatia kwenye miundombinu tu japo nako huko alitupiga hasa
 
Sawa kwa mtazamo wako Ila naye ni moja ya Viongozi walioharibu uchumi wetu kuliko uhalisia ya yanayosemwa, Jambo pekee naweza msifu Magufuli ni miundombinu na maamuzi magumu(japo Kuna wakati alitanguliza Chuki na ubaguzi) Kama angerekebisha hapo na kutawala kwa usawa nadhani angeweka rekodi ambayo kuvunjwa kwake ingechukua miaka zaidi ya 50.
Alafu Tanzania ikafikaje uchumi wa kati? Au aliwahinga world bank
 
Bado aumize kichwa namna ya kupambana na mfumuko wa bei yeye ndio anatamani tozo ziongezeke hadi kwenye ving'amuzi kuzidi kuwaongezea mzigo wananchi,halafu kituko sasa anataka kupunguza kodi kwenye kamari!
Ili wengi mbeti huko,pesa ziende nje
 
Serikali kwa mwezi hupata wastani wa Tshs bilion 350-400 kwa kodi /ushuru unaotokana na petrol,diesel na mafuta ya taa.
Wastan wa kodi/ushuru kwa kila lita moja ya mafuta hayo ni Tshs 940,na wastan wa matumizi ni lita 400 kwa mwezi.
Hivyo kusanyo hilo ni sawa na asilimia almost 30 ya kusanyo la mwezi ( Trilion 1.3)....
 
Kweli kabisa maana majanga yote tuliyopata kama Tetemeko la kagera na Ile Ajali ya Mwanza mahela kibao yalikuja kama Rambirambi Magu hajakula hata sh 10 hela zote zilifaidisha wahanga.

Ama nasema uongo ndugu zangu 🤣🤣
Yaani unazungumza vitu vidogo sana. Jaribu kurudisha akili zako vizuri.
 
Tatizo tunategemea misaada kutoka nchi za Magharibi na Bi mkubwa hawezi kwenda nao kinyume ujasiri huo hana,wewe si unaona juzi alisema safari ndizo zinampa hela za miradi ila kiujumla life gumu.

Naona ndani ya mwezi huu nauli mpya zitatangazwa.
Si huwa tunawaambia hakuna Rais hapa na mnabisha. Rais huwa hapimwi kwa kuvaa suti na kupanda ndege, Rais hupimwa kwa changamoto anazopitia na response yake na mikakati endelevu. Huwezi beba mtu mwenye elimu haieleweki imepatikaje, timeline na mtiririko wake havieleweki ukampachika cheo kutimiza usawa wa kijinsia kisha ukampa nafasi ya juu ya nchi "kwa kudra za Mwenyezi Mungu" ukatarajia maajabu. Sanasana akiweza ni kusoma hotuba anayoandikiwa, kuigiza jambo ambalo hata Ebitoke anaweza na kusafiri.

India inanunua mafuta bei nafuu kutoka Urusi na inauza tena soko la dunia, inanunua pia makaa ya mawe kwao. China inanunua gesi nafuu kwao. Tanzania haiwezi nunua kwa Urusi kwa sababu HAINA AKILI, nchi nzima ni vilaza watupu. Nchi zenye akili huwezi ongoza bila maono ukabaki. Ujerumani na nchi kibao za Ulaya zinanunua gesi Urusi, anayesema hatuwezi nunua kwao kisa sanctions mbona hao wazungu walioweka sanctions bado energy sources wananunua uko na isitoshe nishati haina sanctions kivile. Sanasana tatizo hapa ni SWIFT ya kufanyia malipo, ila mbona India wanalipa kwa njia mbadala. Hapa ndio akili zinatakiwa kuwa na alternatives.

Nenda Urusi agiza mafuta subiri tankers zije. Mambo ya vibari na mikataba ndio tujue umuhimu wa kuwa na mikataba inayotupa advantage
 
Gari linarudi kuwa anasa very soon. Ikiendelea hivi wengi tutayaona magari kama anasa tu. Kwamba 10ltrs ni 32,000 kweli?
 
Back
Top Bottom