Serikali kuweka ruzuku ya shs100 billion siyo suluhisho,na ruzuku hii haiwezi kupunguza bei ya bidhaa za mafuta.
Ushauri
1). Serikali iangalie uwezekano wa kupunguza utitiri wa Kodi ya ushuru wa forodha na VAT kwenye mafuta kwa kipindi hiki cha mpito (cutdown tax rates on petroleum products by 50%)
2). Serikali iangalie uwezekano wa kuondoa/kupunguza levies zote zinazotozwa kwenye bidhaa za mafuta ña taasisi mbalimbali hapa nchini kwa kipindi hiki cha mpito.Hizi taasisi zinamapesa mengi zinazotumika vibaya na watumishi wao.
3). Serikali, iangalie uwezekano wa kuendelea na bei ya Mwezi Juni 2022 hata Kama ikibidi kuongeza ruzuku kutoka shs 100 bilioni kwenda shs150 billion kwa masilahi mapana ya wananchi. hali ni mbaya huku kitaa.