EWURA yatangaza bei mpya za mafuta ya Julai, 2022. Petroli, Dizeli zapanda

EWURA yatangaza bei mpya za mafuta ya Julai, 2022. Petroli, Dizeli zapanda

Si huwa tunawaambia hakuna Rais hapa na mnabisha. Rais huwa hapimwi kwa kuvaa suti na kupanda ndege, Rais hupimwa kwa changamoto anazopitia na response yake na mikakati endelevu. Huwezi beba mtu mwenye elimu haieleweki imepatikaje, timeline na mtiririko wake havieleweki ukampachika cheo kutimiza usawa wa kijinsia kisha ukampa nafasi ya juu ya nchi "kwa kudra za Mwenyezi Mungu" ukatarajia maajabu. Sanasana akiweza ni kusoma hotuba anayoandikiwa, kuigiza jambo ambalo hata Ebitoke anaweza na kusafiri.

India inanunua mafuta bei nafuu kutoka Urusi na inauza tena soko la dunia, inanunua pia makaa ya mawe kwao. China inanunua gesi nafuu kwao. Tanzania haiwezi nunua kwa Urusi kwa sababu HAINA AKILI, nchi nzima ni vilaza watupu. Nchi zenye akili huwezi ongoza bila maono ukabaki. Ujerumani na nchi kibao za Ulaya zinanunua gesi Urusi, anayesema hatuwezi nunua kwao kisa sanctions mbona hao wazungu walioweka sanctions bado energy sources wananunua uko na isitoshe nishati haina sanctions kivile. Sanasana tatizo hapa ni SWIFT ya kufanyia malipo, ila mbona India wanalipa kwa njia mbadala. Hapa ndio akili zinatakiwa kuwa na alternatives.

Nenda Urusi agiza mafuta subiri tankers zije. Mambo ya vibari na mikataba ndio tujue umuhimu wa kuwa na mikataba inayotupa advantage
Kwaiyo pro NATO na wewe sahivi unataka tukanunue mafuta ya baei rahisi kwa urusi,[emoji16]
 
Si walidai wanawekeza bln 100 kwenye ruzuku ya mafuta ili yapungue bei!
Kwani hujasoma hilo jedwali la bei za mafuta! Wameandika bei kabla ya ruzuku na bei baada ya ruzuku, kwahiyo unaweza kuona kama wasingepewa hela za ruzuku mafuta yangeuzwaje!?
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazo anza kutumika Tarehe 6 Julai 2022 saa 6:01 usiku.

Aidha, Katika kukabiliana na ongezeko la bei za mafuta hapa nchini, Serikali imetoa ruzuku nyingine ya Shilingi billioni 100 kwa mwezi Julai 2022, iliyoelekezwa katika mafuta ya petroli na dizeli
-
EWURA imefafanua kuwa Kiasi kikubwa cha ruzuku kimeelekezwa katika mafuta ya dizeli kwa lengo la kudhibiti mfumuko wa bei nchini (inflation) kwa sababu dizeli hutumika zaidi katika shughuli za kiuchumi ikiwemo katika uzalishaji viwandani na katika usafirishaji wa mazao na bidhaa nyingine.
Kikwete na kampuni zake zaafuta watatumaliza, Samia hafai kuwa rais kabisa yuko mikononi mwa mafisadi papa wakisingizia vita ya Ukraine wa lkati mafuta ya urusi yanapatikana kwa bei raisi
 
Mkuu sina connection kwa mama.
Wasukuma wangu wametupwa nje wanalia na kusaga meno nami nilikuwa naponea migongoni mwao[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sasa hivi ni kipindi cha kujenga urafiki wa karibu na Wazanzibari aka wa Pemba, Wasukuma tupa kule kwa Sasa, ukiwakosa Wapemba angalu tafuta Wakwere wa Chalinze kidogo Mambo yako yanaweza nyooka vizuri!!
 
Kale ka nyongeza ka 23% naona kakifunikwa kwenye bei ya wese, hapa ndo maamuzi magumu yanatakiwa kufanyika kutafuta mafuta ya bei chee ya mrusi kwa kumwekea beberu uso wa mbuzi.
 
Wananchi tunapigwa mbele nyuma ni mwendo wa kukamuliwa tu, leo parking hadi uchochoroni yaani usitoke na gari home hata ukienda tu bar we park ukitoka tu unadaiwa hela ya parking. SAsa hadi nje ya mji ushuru wa parking wa nn chanika, tegeta, mbagala huko. Maana tujuavyo lengo la parking ni kupunguza foleni city center, sasa mbona mwatufata hadi nje ya mji, leo ukitoka tu na gari andaa elf 5 parking, hela ya traffic,achilia gharama za kuliingiza nchini. Wamekosa ubunifu kabisa wa kupata vyanzo vya pesa zaidi ya kuwakamua wananchi masikini ambao wameshindwa wajengea uwezo wa kuziona fursa wazalishe.
Parking fee inakuwa implemented kwa ajili ya ku discourage msongamano wa magari maeneo ya katikati ya mji na si vinginevyo. Kutoza parking fee kwenye maeneo ya pembezoni mwa mji kwenye barabara za mitaani na pembeni ya maduka na maeneo ya huduma kama baa, mahoteli, mabenki nk. ni uporaji wa mchana kweupe.
 
Vipi kauli ya Magu mwenyewe kwamba sukari ilikuwa 5000 akaishusha?

Zanzibar ipi Mkuu? Hii ni bei elekezi ya Mafuta Zura Zanzibar ya June
View attachment 2282174
Petroli 2924 sawa na mikoa ya pwani June, Diesel 3582 Ghali kuliko mikoa ya Pwani June.

Bado ya July haijatoka.
Kauli ya Magu? Mm nawezaje kumuamini Magufuli?

Afu kuhusu mafuta zenj, hebu soma tena vizuri hizo Bei na kilichoandikwa. Umeleta ww mwenyewe lakini umeshindwa kusoma kwa makini. Hakuna sehemu mafuta yanauzwa 2924 kwa petrol Wala 3500 kwa diesel. Narudia tena soma vizuri ulichokileta hapo
 
Mlishaambiwa mkiona mziki mzito
Pakini magari yenu

Ova
Mkuu hivi hizi bei zinawahusu wenye magari tu? Mafuta kupanda bei inamhusu kila mtu hata ambae hana gari kwa kuwa gharama ya safirishaji wa bidhaa utaongezeka na bidhaa zitaongezeka Bei.
Muuza ndizi mabibo Kama alikua analeta fuso pale kwa mil 1, Sasa hivi ataleta kwa mil 1.2
 
Kuna kitu huwa sielewi hapa inaonesha Bagamoyo bei ya mafuta ni 3521 na ndio wanapopunguzia,mbona hii bei siioni sheri za hapa Bagamoyo? Bei ya mpaka jana tarehe tano ni Tsh 3142 kwa diesel hapa Bagamoyo mjini. Naomba nieleweshwe hizi zinazoandikwa humu huwa ni zinatoka wapi maana mwisho wa siku mafuta yanashuka lakini ndio kiuhalisia yanabaki pale pale. Au hizi ni expected prices za mzigo mpya unaoingia?
Kusoma hujui kabisa? Mbona hayo majedwali yameandikwa kwa kiswahili?
 
Parking fee inakuwa implemented kwa ajili ya ku discourage msongamano wa magari maeneo ya katikati ya mji na si vinginevyo. Kutoza parking fee kwenye maeneo ya pembezoni mwa mji kwenye barabara za mitaani na pembeni ya maduka na maeneo ya huduma kama baa, mahoteli, mabenki nk. ni uporaji wa mchana kweupe.
So tunayo haki ya kugoma kulipa kwa mujibu wa sheria.
Shida wanabeti siku hizi maana wamewekewa malengo kwa siku hivyo ni rahisi kuweka namba yeyeto.
Nimewahi kuwa daladala kuchek kwenye system limepigwa cheti route ambayo halijawahi kwenda tena kwa tarehe likiwa juu ya mawe gereji.
 
Kauli ya Magu? Mm nawezaje kumuamini Magufuli?

Afu kuhusu mafuta zenj, hebu soma tena vizuri hizo Bei na kilichoandikwa. Umeleta ww mwenyewe lakini umeshindwa kusoma kwa makini. Hakuna sehemu mafuta yanauzwa 2924 kwa petrol Wala 3500 kwa diesel. Narudia tena soma vizuri ulichokileta hapo
Hio ni fidia ina maana yamekuwa subsidized hivyo inaprove point yangu kwamba mafuta yamepanda.

Leo Bakhresa akifidia bei ya mafuta yakashuka toka hio 3000 Kuja 1500 inamaanisha Soko la Dunia hayajapanda?
 
Mama anafungua nchi…tumepigwa.
 
Unafki ndo Jambo tunaloliweza sisi wantanzania watu wanasahau mapema Sana...Magufuli alipatia kwenye miundombinu tu japo nako huko alitupiga hasa
Hata kuleta Discipline Magufuli alijitahidi, na kukusanya pesa.

Ila Magu alikuwa akitafuta pesa kwa Akili ya CCM na genge lake, budget muhimu muhimu kama Afya na Elimu zilitupwa huko.

Kama Mtu alikuwa Ana Guts za kupunguza Bajeti hadi ya Elimu unategemea atamsaidia Masikini kujikwamua na Majanga?
 
Tumefika Patamu Lita 2 za mafuta Tshs 7000 hadi mama akijakushitukia hu mchezo watu watakuwa wameshaumia sana
 
Back
Top Bottom