FACT CHECK: Roma hakutekwa, alijiteka kwa maslahi binafsi ya kiMuziki


Makonda ndio kakutuma kuandika huu utumbo?
 
Alijiteka ili aifunike Kiki ya mwenzake Nay wa Mitego?

Lakini kwenye video Roma anaoneka anachechemea sasa tusubiri kesho tuane another episode ambayo kila mtu anahamu nayo.
 
UKWELI WA ROMA NDIO UTAOMUWEKA WAZI KWAMBA HAJASHIRIKIANA NA BASHITE KUANDAA MOVIE YAKIHINDI,AKISEMA UONGO BASI IMEKULA KWAKE.
 
Sioni hoja yoyote hapo, haswa hapo unapohoji kuwa Watekaji walikuwa Wastaarabu....hivi uliambiwa na nani kuwa kuna formular maalum ya utekaji?

Kuna documenary ya 2013 "The captain and his Pirates"....ili base kwenye true story ya Captain wa meli iliyotekwa Somalia...Captain na Wenzake walipata treatment nzuri tu kwa muda wote wameshikiliwa kutoka kwa Wasomali ambao wengi tunaamini jamaa ni Watu Wakatili sana...kwa kifupi huwa inategemea Watekaji wana lengo gani na hakuna formular maalum ya kufuata.

Tukirudi kwenye mada, nadhani hata mimi nilihoji tangu awali kuhusu sababu haswa za kupelekea Roma atekwe....any way labda inawezekana......ila hofu yangu ni sisi Watanzani na tabia ya kurukia mambo tukiongozwa na mihemko na ushabiki....reasoning za wengi wetu zipo chini sana...tunahukumu na kuhalalisha mambo ambayo hata hatuyajui.

Labda kwa kuwa 'amerudi' hebu yeye sasa atuambie alikuwa wapi?
 
Swali muhimu ni hao waliotekwa walipatikana wapi??

Hapo ni wajibu wa police na serikali nzima ambayo imeonekana ikishutumiwa kujinasua katika hili na kuuthibitishia umma kwamba hao vijana walijiteka!

Ila hii issue Roma ,serikali lao Moja Bila shakaaa.
 
Hizi habari si zakuleta humu jF. Kawadanganye labda watu wa bush au ambao hawakwenda shule. Kajiteka na aliyempeleka kumkabidh ni nani?
Hapa Roma , serikali wanajua walichofanya wanaelewa vizuri.
 
Sio watakuwa wamepatikana rudia tena kuskiliza kauli ya bashite alisema haitafika jumapili tutakuwa tumewarejesha ndugu zetu wakiwa salama.rudia tena kumsikiliza
 
Umeandika mengi sana, yanayobewa na sentensi fupi.

".....kabla ya jumapili Roma na wenzake watakuwa wameishapatikana"

Sasa labda huyu ndio aseme walijiteka vipi maana kweli wamepatikana kabla hata J. Mosi haijaisha vizuri.
Alicho sahau ni kuwa Roma ,police na serikali lao Moja .
 
kuhu
kuhusu MAVAZI, tumeambiwa watekaji waliwarudisha akina Roma saa 9 usiku hapo walipo wachukua, baadaye ndio wakapelekwa Ostabay police, yawezekana mda huo ndio Roma kabadilisha mavazi
 
Uzi umetungwa na Bashite kwa ajili ya Mabashite..
Hauna tofauti na ngonjera ya domo
 
Non sense

Kilaza kingine hichi nacho
Kawadanganye watoto tena Wa chekechea ndio wataelewa huu upupu ulioandika

Vichwa vimewauma jinsi mlivyoumbuka,ndio mkaamua kuja na hizi porojo

Bashite mkubwa wewe
 
Haaaa. Yaani wewe mleta uzi umetumwa na nani kuleta uongo humu? Kawaaminishe bashite wenzako wewe. Inaonekana umejiunga Leo ili kupooza maneno!! Kwani watekaji unataka waje na bunduki ndo uamini? None sense
Huyu atakuwa kibaraka Wa bashite
Ndio kamwambia aje aanzishe Uzi Wa ki fa fa fa fa fa
 
Naungana nawe katika kuhoji hili
Kabisa mkuu..

Na kama hawakujiteka basi hao waliowateka wafikishwe katika vyombo vya kisheria..

Kama mtu anaweza kuwateka watu na kukaa nao hata siku tatu inamaanisha angeweza kuwafanya lolote atakalo.. Je hapo tunaweza kusimama na kujipiga vifua vyetu na kusema nchi ipo salama au raia wetu wako salama??
 
Ukweli ni upi?,
Mawazo yako Ndo ukweli?

Soma acha kama ilivyo.
Huyu anaeleza alichokipata.

Ukweli anao Roma. Ni mchungu, Muwe tayari kuusikia
 
kuhu

kuhusu MAVAZI, tumeambiwa watekaji waliwarudisha akina Roma saa 9 usiku hapo walipo wachukua, baadaye ndio wakapelekwa Ostabay police, yawezekana mda huo ndio Roma kabadilisha mavazi
Hahahahahah yaani mtekaji anakurudisha alipokutekaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…