Facts! Foreign Players wa Simba wengi kawaida sana!

Safi, mara moja moja tuwe tunaambiana ukweli kama hivi bhana......huyo barbacar sarr bado sijaona chochote mguuni mwake wala utimizaji wa majukumu kama DM wa uhakika mpaka sasa.
Saidoo yule ndo kila siku nawakumbusha viongozi wa simba wamtoe msimu huu.
Baleke pia atolewe, onana apelekwe timu yoyote kwa mkopo. Tubaki na phiri ndo then anunuliwe forward mpya wa kueleweka haijalishi kutoka ndani au nje ya nchi.
Fabrice Ngoma apewe kalipio kali la kuhakikisha anapandisha kiwango chake zaidi ya pale.
Mikson aambiwe aongeze zaidi juhudi mana ni kama kaanza kujipata kidogo.
 
Simba wameshageuka paka,..wachezaji wanakula mishahara ya bure tu hapo msimbazi
Fukuza wote tuanze upya..
Baleke,onana,phiri,ntibazongiza, na wengine
 
Wachezaji wazawa pia wapewe nafasi zaidi mana ni kama wakiwa uwanjani wanapambana sana kuliko haya mageni yanayokula tu mishahara mikubwe afu uchungu na timu ni sufuri.
 
Barikiwa Kwa bandiko zuri na lililojaa ukaweli. Tatizo lingine linasababishwa na mapambio ya Ahmed Ally. Onana kweli wa kutakiwa ligi Kuu Ufaransa?
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] walimtaka psg au monaco?
 
Its true! Kwa wachezaji wa kimataifa ni vizuri tukaanza moja. Tumpe kocha wigo ajenge timu mwenyewe! Bora wabakie local players na internationals wachache tuanze scouting ya maana. Kocha apewe fungu alete watu sisi tumpe project na malengo yake tuone.
 
Na mimavi juu...mpaka sasa Ni wachezaji wawili tu angalau tunaweza sema tuna professional player nao ni Ngoma na Inonga waliobaki unashika kichwa muda wowote wanachoma kibanda.
Chemalone vip
 
Kwamba kuna wapenzi wa yanga wanashindwa kuifanya kazi yao vyema ili kukwamisha juhudi za timu ?
 
Simba nilishaikatia tamaa toka washindwe kumsajili adebayor
 
Mpaka msemeee!
 
Hao vijana lazima wawe wazawa maana wageni wamezidi hata Sasa kwa hiyo lazima wapunguzwe

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Wachezaji wa kuletwa na kocha unawajua vizuri? unakumbuka Sawadogo, Dejan, Qattara?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…