Facts! Foreign Players wa Simba wengi kawaida sana!

Facts! Foreign Players wa Simba wengi kawaida sana!

Safi, mara moja moja tuwe tunaambiana ukweli kama hivi bhana......huyo barbacar sarr bado sijaona chochote mguuni mwake wala utimizaji wa majukumu kama DM wa uhakika mpaka sasa.
Saidoo yule ndo kila siku nawakumbusha viongozi wa simba wamtoe msimu huu.
Baleke pia atolewe, onana apelekwe timu yoyote kwa mkopo. Tubaki na phiri ndo then anunuliwe forward mpya wa kueleweka haijalishi kutoka ndani au nje ya nchi.
Fabrice Ngoma apewe kalipio kali la kuhakikisha anapandisha kiwango chake zaidi ya pale.
Mikson aambiwe aongeze zaidi juhudi mana ni kama kaanza kujipata kidogo.
 
Simba wameshageuka paka,..wachezaji wanakula mishahara ya bure tu hapo msimbazi
Fukuza wote tuanze upya..
Baleke,onana,phiri,ntibazongiza, na wengine
 
Wachezaji wazawa pia wapewe nafasi zaidi mana ni kama wakiwa uwanjani wanapambana sana kuliko haya mageni yanayokula tu mishahara mikubwe afu uchungu na timu ni sufuri.
 
Barikiwa Kwa bandiko zuri na lililojaa ukaweli. Tatizo lingine linasababishwa na mapambio ya Ahmed Ally. Onana kweli wa kutakiwa ligi Kuu Ufaransa?
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] walimtaka psg au monaco?
 
Matatizo ya Simba hayatokani na viongozi, bali yanatokana na mashabiki. Viongozi wanasajipi kwa lengo la kuwatuliza mashabiki na sio kuboresba timu.

Simba ilikuwa inahitaji namba 6, mkasajili Ngoma ambaye sio typically namba 6. Japo ameingia kwenye mfumo wenu, ila timu bado inahitaji namba 6. Babacar yawezekana akawa mzuri, ila hawezi kuclick ndani ya muda mfupi kama mnavyohitaji.

Timu imejaza winger kibao ambao ni mzigo. Kwa aina ya washambuliaji mlionao, wanahitaji sana mipira ya cross. Lakini hakuna winga hata mmoja mwenye kupiga cross, wote ni wale wa kupiga chenga kuingia 18, lakini finishing ni sifuri. Cross mpaka leo mnategemea Kapombe na Shabalala.

Simba inahitaji overhaul kama aliyokuwa anafanya Yanga kipindi kile. Walikuwa wanaleta wachezaji wengi, wakishindwa kudeliver, wanatimua na kuleta wengine. Mpaka msimu ule wa kina Bangala, ndio timu ikatulia. Tokea pale yanafanyika maboresho madogo madogo tu.

Mchezaji mmoja hatoshi kuibadilisha Simba. Na ni rahisi hata kwa mchezaji mzuri kuonekana mbaya.
Its true! Kwa wachezaji wa kimataifa ni vizuri tukaanza moja. Tumpe kocha wigo ajenge timu mwenyewe! Bora wabakie local players na internationals wachache tuanze scouting ya maana. Kocha apewe fungu alete watu sisi tumpe project na malengo yake tuone.
 
Na mimavi juu...mpaka sasa Ni wachezaji wawili tu angalau tunaweza sema tuna professional player nao ni Ngoma na Inonga waliobaki unashika kichwa muda wowote wanachoma kibanda.
Chemalone vip
 
Hivi kama sio hujuma za wazi, hii timu baada ya kuondoka Lwanga imeshindwa vipi kusajili DM? Hawa viongozi wanasajili kiungo na kutudanganya kuwa amekuja kutibu tatizo la DM huku mchezaji mwenyewe uwanjani hana sifa yoyote ya kuwa DM.

Sasa kwa huyu si bora wangemchukua Aweso au Himidi mbongo mwenzetu? Kaingia Hamisi Abdalah kaubonda kuliko kiungo mpya. Nina hofu pengine management ina watu wa Uto na hatujashtuka! Unafanyika ujinga ule ule!
Kwamba kuna wapenzi wa yanga wanashindwa kuifanya kazi yao vyema ili kukwamisha juhudi za timu ?
 

Attachments

  • Screenshot_20240114_143346_Chrome.jpg
    Screenshot_20240114_143346_Chrome.jpg
    105.4 KB · Views: 1
Wakuu,

Tuambiane ukweli familia, asilimia kubwa ya vipaji tunavyoleta Simba hapa Tanzania ni aina ya vipaji ambavyo ukifanya proper scouting vipo hapa hapa ndani.

Nafasi ya goal keeper haihitaji foreign player, Onana, Saido, Luis, Baleke na Phiri wote ni average players tunadanganyana tu.

Ni vizuri tulete mtu ambaye ni kipaji kisichopatikana ndani! Kama tunataka nusu fainali tuingie hasara ya kuondoa wachezaji wengi wa kigeni tusajili watu wenye record na wataoingia kwenye kikosi direct.

Kama mfuko hauruhusu kununua wachezaji wa maana tuache kupotezea muda mashabiki na kumkausha koo Ahmed Ally! Tunaumiza makocha vichwa kwa vipaji very average na wachezaji wenyewe tunawalipa fedha nyingi.

Haya tumetolewa nishai na Mlandege yenye vipaji vingi local na bajeti ndogo! Tuache kuimbiana mapambio na kufukuza makocha! Viongozi wabadilike.

Kuitaja nusu fainali club bingwa kwa mikakati hii ni kutufanya watoto. Wachezaji wengi wa kigeni tumepigwa! Huyo kiungo mpya hamuwezi hata Aweso! Upumbavu tu!

Simbaaaa #nguvumoja[emoji109]
Simba nilishaikatia tamaa toka washindwe kumsajili adebayor
 
Hivi kama sio hujuma za wazi, hii timu baada ya kuondoka Lwanga imeshindwa vipi kusajili DM? Hawa viongozi wanasajili kiungo na kutudanganya kuwa amekuja kutibu tatizo la DM huku mchezaji mwenyewe uwanjani hana sifa yoyote ya kuwa DM.

Sasa kwa huyu si bora wangemchukua Aweso au Himidi mbongo mwenzetu? Kaingia Hamisi Abdalah kaubonda kuliko kiungo mpya. Nina hofu pengine management ina watu wa Uto na hatujashtuka! Unafanyika ujinga ule ule!
Mpaka msemeee!
 
Bora hiyo. Kuna moja saido alienda chini na beki wa Mlandege, akatoa pasi moja nzuri sana kwa Baleke ya kupress tu kidogo upande wa kulia wa goli. Yeye akabambikizia tena mabeki upande wa kushoto kipuuzi kabisa akaharibu nafasi nzuri sana ya kushinda goli la wazi. Na bado akaendelea kuharibu nafasi nyingine nzuri tena na tena! i

Kama wanaanza kupunguza wachezaji, binafsi naona waanze na Baleke. Jamaa ana IQ ndogo sana ya ushambuliaji. Nguvu nyingi kwenye vitu vya kutumia akili kidogo tu.

Namna bora ya kuwapunguza hawa kina onana, saido, sarr na wengineo ni kuwaletea competition tu. Yani waletwe vijana wa kuwakata namba na wao bado wakiwepo. Waone namna walivyotakiwa kucheza kupitia wachezaji wengine halafu watimuliwe mazima, pumbav!
Hao vijana lazima wawe wazawa maana wageni wamezidi hata Sasa kwa hiyo lazima wapunguzwe

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Its true! Kwa wachezaji wa kimataifa ni vizuri tukaanza moja. Tumpe kocha wigo ajenge timu mwenyewe! Bora wabakie local players na internationals wachache tuanze scouting ya maana. Kocha apewe fungu alete watu sisi tumpe project na malengo yake tuone.
Wachezaji wa kuletwa na kocha unawajua vizuri? unakumbuka Sawadogo, Dejan, Qattara?
 
Back
Top Bottom