Wakuu,
Tuambiane ukweli familia, asilimia kubwa ya vipaji tunavyoleta Simba hapa Tanzania ni aina ya vipaji ambavyo ukifanya proper scouting vipo hapa hapa ndani.
Nafasi ya goal keeper haihitaji foreign player, Onana, Saido, Luis, Baleke na Phiri wote ni average players tunadanganyana tu.
Ni vizuri tulete mtu ambaye ni kipaji kisichopatikana ndani! Kama tunataka nusu fainali tuingie hasara ya kuondoa wachezaji wengi wa kigeni tusajili watu wenye record na wataoingia kwenye kikosi direct.
Kama mfuko hauruhusu kununua wachezaji wa maana tuache kupotezea muda mashabiki na kumkausha koo Ahmed Ally! Tunaumiza makocha vichwa kwa vipaji very average na wachezaji wenyewe tunawalipa fedha nyingi.
Haya tumetolewa nishai na Mlandege yenye vipaji vingi local na bajeti ndogo! Tuache kuimbiana mapambio na kufukuza makocha! Viongozi wabadilike.
Kuitaja nusu fainali club bingwa kwa mikakati hii ni kutufanya watoto. Wachezaji wengi wa kigeni tumepigwa! Huyo kiungo mpya hamuwezi hata Aweso! Upumbavu tu!
Simbaaaa #nguvumoja[emoji109]