Midimay
JF-Expert Member
- Apr 12, 2015
- 3,036
- 5,039
Habari za asubuhi wana JF,
Tunaendelea na hili jambo ambalo sasa lipo katika ngazi ya familia kabisa. Tunaulizwa majumbani mwetu. Kuna mambo kadhaa ambazo ni facts kabisa katika mkataba huu na zinaufanya ukose sifa.
Wao wanasema ni makubaliano tu, lakini makubaliano ni mkataba. Baadhi ya facts hizo nilizoziona ni hizi zifuatazo:
1. Makubaliano hayana ukomo. Kama ambavyo imeonekana kwa wengi, makubaliano haya hayaonyeshi muda maalum katika umilikishaji wa bandari zote kwa DPW.
2. Umilikishaji wa Bandari zote. Kwanini DPW wapewe bandari zote za Bahari, Mito na Maziwa katika iliyokuwa Tanganyika? Tumezichoka au tamaa ya watawala au kulambishwa asali?
3. Kutohusishwa kwa bandari za upande wa Zanzibar. Hili linasababisha mtanziko wa kikatiba kabisa (Constitutional Crisis). Sheria wanayosema inaipa TPA mamlaka ya upande ya iliyokuwa Tanganyika, imeipa TPA mamlaka ya Tanzania bara na Tanzania Zanzibar katika kifungu cha 2 cha sheria hiyo ya TPA.
4. Hakukuwa na ushindani katika kutafuta mwekezaji. Hiyo inaipa DPW nguvu ya kuinyanyasa na kuifanya kuwa wanyonge serikali ya Tanzania kupitia hiyo timu ya Hamza Johari. Lakini pia ni uvunjaji na ukiukaji wa sheria za nchi juu yw manunuzi ya umma na uwekezaji katika rasilimali asili za nchi.
5. Pesa yenyewe inayotajwa, siyo kiasi cha kuvutia. Hivi leo nchi hii inayokusanya 2+ T kwa mwezi kama mapato ya kodi tu, inawehuka na uwekezaji wa 2T? kiasi cha kuachia bandari zote kwa DPW?
6. Kukosekana kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hadi sasa hatuoni katika document na katika ufafanuzi, mahali popote ambapo ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imehusika katika kushauri na kuyabariki makubaliano haya. Hili pia linavunja katiba na sheria kadhaa za nchi.
7. Kukosekana kwa sahihi ya Katibu Mkuu-Uchukuzi. Sehemu ya sahihi ya Katibu Mkuu-Uchukuzi imesainiwa kwa niaba yake na hadi sasa hakuna ufafanuzi wowote juu ya hilo. Je, kama alikataa? Wenye tamaa wakalazimisha? Kwanini waziri alisaini kwa niaba ya Katibu Mkuu?
8. Tanzania kutakiwa kuijulisha Dubai juu ya uwekezaji mpya katika bandari au maeneo mengine. Hili ni dharau kwa nchi na kuikosesha nchi wawekezaji wapya ambao wangekuja na terms bora kuliko za DPW.
9. Utatuzi wa migogoro unaenda kinyume na sheria ya Natural Resources (permanent sovereignty).
10. Wananchi hatuyataki haya makubaliano. Hili nalo kisidharuliwe. Haya makubaliano yamekataliwa na wananchi.