Facts kadhaa zinazoufanya Mkataba wa Tanzania na Dubai juu ya Bandari kuwa batili. Tuwe nazo Makini

Facts kadhaa zinazoufanya Mkataba wa Tanzania na Dubai juu ya Bandari kuwa batili. Tuwe nazo Makini

Hiyo ndio hatutaki. Hatuna access na HGA, itamkwe huku huku kwenye IGA
Kusema hutaki termination clause..Kwa kuwa wewe huna access na HGA sio Sawa nakusema "hakuna termination clause"...
Kwahiyo kabla huja demand kuona HGA kwanza mkiri mnafanya upotoshaji...
Kingine hutaki wewe na nani??

Usiseme hatutaki ,sema wewe hutaki
 
Kuna mwanasheria anajiita Boniface somebody ame trend Sana mitandaoni kupinga mkataba..
Akasema eti Bandari ni mpaka...imagine that..na yeye ni msomi...hajui kabisa bandari ni entry point sio border...hajui kila nchi ina kilomita ngapi ndani ya maji za kuweka mpaka wala hajui territorial waters nini nini na international waters ni nini...lakini kaenda mitandaoni anawatukana wabunge kuwa hawajui Bandari ni Mpaka...imagine that...wala hajui Meli kabla ya kufika Bandarini zina procedures zinafanya...haziiingii bandarini kama daladala na hizo procedures zinasimamiwa. Na mamlaka ya nchi sio mwekezaji...
Mtu ignorant anakusanya kijiji kuwa ni Mtaalam aliechambua mkataba
In principle bandari as airports, sio mpaka, but in practice, as far as movement of people and goods, bandari na airports ni mpaka.

I know in and out.

Mpaka kwa sasa is not that line/boundaries. Things have changed a lot.

Understand the facts, not theories
 
IGA haiwezi kuvunjwa kwa vyovyote vile, kasome uelewe. Na hiyo clause ya kuvunjwa, inafutwa na hii clause.
 
In principle bandari as airports, sio mpaka, but in practice, as far as movement of people and goods, bandari na airports ni mpaka.

I know in and out.

Mpaka kwa sasa is not that line/boundaries. Things have changed a lot.

Understand the facts, not theories
Bandari sio mpaka, period..
 
Tena kifungu hiko kinatupa Sisi Uhuru wetu ...tunaweza piga Kura Kui favour Israel badala ya Palestine na Dubai wasiseme lolote .. kipengele kimewekwa kuwa hata tukitofautiana mitazamo ya kimataifa isihusishe bandari...Dubai wanaweza unga mkono NATO,Sisi tukaunga mkono Russia kwenye ugomvi wa Ukraine....watu wanazusha kuwa ndo tumefungwa uhuru. Dah
Hii tafsiri yako ni nyingine kabisa.

Hata tukivunja mahusiano ya kidiplomasia na Dubei, ....anzia hapo! Acha kuyumba eti akisapoti sijui nani, na sisi nani,
 
Habari za asubuhi wana JF,

Tunaendelea na hili jambo ambalo sasa lipo katika ngazi ya familia kabisa. Tunaulizwa majumbani mwetu. Kuna mambo kadhaa ambazo ni facts kabisa katika mkataba huu na zinaufanya ukose sifa.

Wao wanasema ni makubaliano tu, lakini makubaliano ni mkataba. Baadhi ya facts hizo nilizoziona ni hizi zifuatazo:

1. Makubaliano hayana ukomo. Kama ambavyo imeonekana kwa wengi, makubaliano haya hayaonyeshi muda maalum katika umilikishaji wa bandari zote kwa DPW.

2. Umilikishaji wa Bandari zote. Kwanini DPW wapewe bandari zote za Bahari, Mito na Maziwa katika iliyokuwa Tanganyika? Tumezichoka au tamaa ya watawala au kulambishwa asali?

3. Kutohusishwa kwa bandari za upande wa Zanzibar. Hili linasababisha mtanziko wa kikatiba kabisa (Constitutional Crisis). Sheria wanayosema inaipa TPA mamlaka ya upande ya iliyokuwa Tanganyika, imeipa TPA mamlaka ya Tanzania bara na Tanzania Zanzibar katika kifungu cha 2 cha sheria hiyo ya TPA.

4. Hakukuwa na ushindani katika kutafuta mwekezaji. Hiyo inaipa DPW nguvu ya kuinyanyasa na kuifanya kuwa wanyonge serikali ya Tanzania kupitia hiyo timu ya Hamza Johari. Lakini pia ni uvunjaji na ukiukaji wa sheria za nchi juu yw manunuzi ya umma na uwekezaji katika rasilimali asili za nchi.

5. Pesa yenyewe inayotajwa, siyo kiasi cha kuvutia. Hivi leo nchi hii inayokusanya 2+ T kwa mwezi kama mapato ya kodi tu, inawehuka na uwekezaji wa 2T? kiasi cha kuachia bandari zote kwa DPW?

6. Kukosekana kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hadi sasa hatuoni katika document na katika ufafanuzi, mahali popote ambapo ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imehusika katika kushauri na kuyabariki makubaliano haya. Hili pia linavunja katiba na sheria kadhaa za nchi.

7. Kukosekana kwa sahihi ya Katibu Mkuu-Uchukuzi. Sehemu ya sahihi ya Katibu Mkuu-Uchukuzi imesainiwa kwa niaba yake na hadi sasa hakuna ufafanuzi wowote juu ya hilo. Je, kama alikataa? Wenye tamaa wakalazimisha? Kwanini waziri alisaini kwa niaba ya Katibu Mkuu?

8. Tanzania kutakiwa kuijulisha Dubai juu ya uwekezaji mpya katika bandari au maeneo mengine. Hili ni dharau kwa nchi na kuikosesha nchi wawekezaji wapya ambao wangekuja na terms bora kuliko za DPW.

9. Utatuzi wa migogoro unaenda kinyume na sheria ya Natural Resources (permanent sovereignty).

10. Wananchi hatuyataki haya makubaliano. Hili nalo kisidharuliwe. Haya makubaliano yamekataliwa na wananchi.
Watanzania bara kazi yetu ni ushabiki usiokuwa na manufaa,fursa ziko nyingi,hatuna kazi nazo,Zanzibar hapo kuna fursa za kitalii,hatuna kazi nazo.Watu kutoka Kenya wanajinufaisha na fursa hizo.
Ukipeleka kitu chochote Zanzibar cha kibiashara au kuwauzia wafanyabiashara kutoka Zanzibar unanufaika kwa utalii ulioko kule
1:Ukiwa na duka au mkulima wa nafaka,wananunua kwako
2:Ukiwa na mazao ya shambani kuanzia Viazi,Nyanya,vitunguu,vitunguu saumu,karoti,pilipili hoho,nk.Ni kila wiki wanakuja fungasha magunia kwa magunia.
Wa Tanzania bara ni kukaa kwenye vijiwe vya kahawa na vijiwe vya pombe za kienyeji kulaumu tu.
 
Habari za asubuhi wana JF,

Tunaendelea na hili jambo ambalo sasa lipo katika ngazi ya familia kabisa. Tunaulizwa majumbani mwetu. Kuna mambo kadhaa ambazo ni facts kabisa katika mkataba huu na zinaufanya ukose sifa.

Wao wanasema ni makubaliano tu, lakini makubaliano ni mkataba. Baadhi ya facts hizo nilizoziona ni hizi zifuatazo:
1. Makubaliano hayana ukomo. Kama ambavyo imeonekana kwa wengi, makubaliano haya hayaonyeshi muda maalum katika umilikishaji wa bandari zote kwa DPW:

Weka ushhi wa fikra zako, hatuendi kifikra, tunaenda kiushahidi.
Kwanza tuoneshe hicho kifungu cha makubaliano / mkataba kinachosema "hayana ukomo". Pia tuoneshe kifungu kinachosema "
umilikishaji wa bandari zote kwa DPW:".

Tuoneshe hivyo, usifikiri wote tu wajinga. Ukishindwa kuvionesha hivyo vifungu basi wewe u muongo.

Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
 
Prove hiyo termination clause. Wewe, The Boss toka mwanzo unautetea huu mkataba kisa tu Rais ni muislamu. Kiti ambacho ni ujinga tu kukubali kitu kisichofaa kisa kiongozi unasali naye.
JPM alipingwa hadi na kina Fr. Kitima.
Tumieni akili acheni kulalamika,hao waarabu wakija ndio fursa ya kufunguka biashara za mazao,hao watataka kula
1.Viazi,Ngano,Michele,mihogo,!
Mapapai,ndizi,matunda nk
 
Hii tafsiri yako ni nyingine kabisa.

Hata tukivunja mahusiano ya kidiplomasia na Dubei, ....anzia hapo! Acha kuyumba eti akisapoti sijui nani, na sisi nani,
Kwani international events umeelewaje?..
 
Tumieni akili acheni kulalamika,hao waarabu wakija ndio fursa ya kufunguka biashara za mazao,hao watataka kula
1.Viazi,Ngano,Michele,mihogo,!
Mapapai,ndizi,matunda nk
Wamekwambia hawana chakula hao?!

Si wanaendesha bandari hapo msumbiji, nani kakwambia msumbiji wamepata soko la mazao?!

Zungumza facts za mkataba, achana na mengineyo, hewa hiyo
 
Wamekwambia hawana chakula hao?!

Si wanaendesha bandari hapo msumbiji, nani kakwambia msumbiji wamepata soko la mazao?!

Zungumza facts za mkataba, achana na mengineyo, hewa hiyo
Hawana chakula kwao ni jangwa,Hakuoti kitu chochote wala kufuga chochote,zaidi ya ngamia,hawana
1.Kuku
2.Ng'ombe
3.Mbuzi.
4.kondoo
5Viazi,ndizi,Michele,matunda,nk
Badala sisi kuanzisha njia za kibiashara kunufaika kwao,twapoteza wakati bure,!nafasi hiyo ya vyakula akichukuwa wa nchi nyingine tutakuja lalamika.Hapo Zanzibar kuna soko kubwa la vyakula na mifugo na matunda,kutokana na mahotel ya kitalii,fursa hatuzitumii.
Kuna visiwa vya Ngazija,Mauritius,Madagascar,!fursa za vyakula kuuza kule,na mifugo,hatutumii.
Kama hivi sasa mbuzi amefika mpaka 170000,ng'ombe mpaka mamilioni,kwa ajili ya sikukuu ya Eid,dini inawahimiza watoe sadaka ya nyama!,bado visima watachimba vya maji.kusaidia kwenye matatizo ya maji,maana dini ya uislamu imehimiza kutoa sadaka ya maji,sisi tumekaa kubishana yasio na faida.Ukiwa na mbuzi 20 si tayari una 36milioni.Bado ng'ombe
Ukiwa nao 20,hujainuka kiuchumi.Na hapo bado waarabu hawajaanza Bandarini.Hawa waislamu waacheni waje,watuinue kiuchumi,siku kuu zao zote na siku za kawaida ni neema.Bado kipindi cha sikukuu ya mwezi wa Ramadani,wananua Michele kwa wingi,kwa kutoa sadaka.Bado hatujagusia wavuvi wa samaki,hawa ni walaji sana wa samaki,kwa wavuvi ni fursa hiyo.
Wakulima na wafugaji,kwa ujio wa hawa waarabu waislamu ni neema kwao.
 
Hivi Tanzania inaweza kuwa na mgogoro wa kidiplomasia na Dubai wakati haina uhusiano wa kidiplomasia nayo
Kuna mwanasheria anajiita Boniface somebody ame trend Sana mitandaoni kupinga mkataba..
Akasema eti Bandari ni mpaka...imagine that..na yeye ni msomi...hajui kabisa bandari ni entry point sio border...hajui kila nchi ina kilomita ngapi ndani ya maji za kuweka mpaka wala hajui territorial waters nini nini na international waters ni nini...lakini kaenda mitandaoni anawatukana wabunge kuwa hawajui Bandari ni Mpaka...imagine that...wala hajui Meli kabla ya kufika Bandarini zina procedures zinafanya...haziiingii bandarini kama daladala na hizo procedures zinasimamiwa. Na mamlaka ya nchi sio mwekezaji...
Mtu ignorant anakusanya kijiji kuwa ni Mtaalam aliechambua mkataba
Bandari ni mpaka hata kama tuna mpaka wa maji au bahari. Mkataba mmbovu. Unauza nchi kwa DPW bila ukomo.
 
Mkataba mbona Una termination clause?
Unaweza iweka hapa tuone labda tatizo ni English na sio mkataba
Hebu weka Termination clause tukutafsirie
Umeshaambiwa termination clause ipo, inasema ukomo utafikiwa kuvunja mkataba pale shughuli za bandari zitakapokoma. Labda sijui kama zitakapokauka maji? Au mwisho wa dunia. Ndo hicho kipengele unachosema kiwekwe
 
Back
Top Bottom