Facts kadhaa zinazoufanya Mkataba wa Tanzania na Dubai juu ya Bandari kuwa batili. Tuwe nazo Makini

Facts kadhaa zinazoufanya Mkataba wa Tanzania na Dubai juu ya Bandari kuwa batili. Tuwe nazo Makini

IGA imetengenezwa kwa ushirikiano kati ya wanasheria wa Tanzania na wale wa Dubai kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita.

Hawa ni wabobezi wa sheria. Kwa upande wa Tanzania ni Dr Possi na Hamza hawa licha ya kusomea sheria pia ni waalimu wa vyuo vikuu ngazi ya masters.

Upande wa DPW pia unao wataalam ambao sio waarabu wa pale ni waajiriwa tu wanaowakilisha kampuni hiyo na wao ni wataalam waliobobea katika sheria.

Watanzania kila kitu tunajifanya tunakijua, kila mahali tunao wepesi wa kukosoa, wepesi wa kutoa mapendekezo, huwa tunachekesha sana na huu ujuaji wetu.

Kwamba mtu mmoja tu humu JF anaandika akikosoa IGA yaani kama vile anajua analoliongea kumbe ni upuuzi mtupu mbele ya mwanasheria mbobezi. Hizi mada za sheria sio sawa na zile za Yanga na Simba kwamba kila mtu anaweza tu kuzielewa na kuzikosoa.
Soma..


Utapata kitu cha kuongeza ktk ubongo wako
 
Usichotwe akili na wapotoshaji .
Termination clause haijasema hivyo..
Lakini wamesema uhai wa IGA uko sambamba na uhai wa HGA ambayo itaweka mda wa mkataba..
Wenzio wanalipwa kupotosha ...
Una uhakika gani mkataba mdogo utafuata mkataba mama? Na je kama ukitaja vinginevyo tutajikwamua vipi na huku Bunge limeridhia? Unazungumziaje kuhusu mkataba kuamuliwa na sheria za kimataifa? Hili nalo halikupi tatizo? Kuna matokeo mengi mabaya na ya nchi kudhalilishwa na kufilisiwa kwa vipengele kama hivyo.
 
Ule mkataba wa hovyo una kasoro zaidi ya moja, sio hiyo duration pekee, ambayo hata nyie hamuijui zaidi ya kubuni tu, mnasema labda miaka 25 or whatever!..

Ule mkataba umevunja sheria kibao za hii Tanganyika yetu, usomeni vizuri muuone.
Hakuna hata sheria moja iliyovunjwa. Ni kelele zenye agenda binafsi tu. Nchi hii hata Serikali ikisema kila mtu ajengewe nyumba, lazima kuna kundi litabisha. Cha muhimu Serikali ifanye kama enzi ya Magufuli. Ikiona jambo linafaa, ifanye maamuzi maisha yaendelee.
 
Kusema hutaki termination clause..Kwa kuwa wewe huna access na HGA sio Sawa nakusema "hakuna termination clause"...
Kwahiyo kabla huja demand kuona HGA kwanza mkiri mnafanya upotoshaji...
Kingine hutaki wewe na nani??

Usiseme hatutaki ,sema wewe hutaki
Wewe ni Maulid Kitenge au Zembwela?
 
Tena kifungu hiko kinatupa Sisi Uhuru wetu ...tunaweza piga Kura Kui favour Israel badala ya Palestine na Dubai wasiseme lolote .. kipengele kimewekwa kuwa hata tukitofautiana mitazamo ya kimataifa isihusishe bandari...Dubai wanaweza unga mkono NATO,Sisi tukaunga mkono Russia kwenye ugomvi wa Ukraine....watu wanazusha kuwa ndo tumefungwa uhuru. Dah
Hawa watu hawaelewi asee, wameamua tu kuvamia agenda za wapotoshaji
 
Nimesoma, pote, hakuna fedha inayoelezewa kuwekwa. Kasome
Namaanisha biashara hii itakuwa na teknolojia za kisasa kiasi cha kuongeza pato na kupunguza muda wa bandari kuhudumia meli moja.

TRA inakusanya trilioni 7 kwa sasa, utendaji ukibadilika pale TPA itakusanya trilioni 26, mara tatu zaidi ya hiki kinachopatikana.

Usishangae sana hawa wawekezaji kupigwa vita, ni vita inayotoka kwa mafisadi wa bandarini watu wanaofaidika na huu utendaji wa sasa.
 
Habari za asubuhi wana JF,

Tunaendelea na hili jambo ambalo sasa lipo katika ngazi ya familia kabisa. Tunaulizwa majumbani mwetu. Kuna mambo kadhaa ambazo ni facts kabisa katika mkataba huu na zinaufanya ukose sifa.

Wao wanasema ni makubaliano tu, lakini makubaliano ni mkataba. Baadhi ya facts hizo nilizoziona ni hizi zifuatazo:

1. Makubaliano hayana ukomo. Kama ambavyo imeonekana kwa wengi, makubaliano haya hayaonyeshi muda maalum katika umilikishaji wa bandari zote kwa DPW.

2. Umilikishaji wa Bandari zote. Kwanini DPW wapewe bandari zote za Bahari, Mito na Maziwa katika iliyokuwa Tanganyika? Tumezichoka au tamaa ya watawala au kulambishwa asali?

3. Kutohusishwa kwa bandari za upande wa Zanzibar. Hili linasababisha mtanziko wa kikatiba kabisa (Constitutional Crisis). Sheria wanayosema inaipa TPA mamlaka ya upande ya iliyokuwa Tanganyika, imeipa TPA mamlaka ya Tanzania bara na Tanzania Zanzibar katika kifungu cha 2 cha sheria hiyo ya TPA.

4. Hakukuwa na ushindani katika kutafuta mwekezaji. Hiyo inaipa DPW nguvu ya kuinyanyasa na kuifanya kuwa wanyonge serikali ya Tanzania kupitia hiyo timu ya Hamza Johari. Lakini pia ni uvunjaji na ukiukaji wa sheria za nchi juu yw manunuzi ya umma na uwekezaji katika rasilimali asili za nchi.

5. Pesa yenyewe inayotajwa, siyo kiasi cha kuvutia. Hivi leo nchi hii inayokusanya 2+ T kwa mwezi kama mapato ya kodi tu, inawehuka na uwekezaji wa 2T? kiasi cha kuachia bandari zote kwa DPW?

6. Kukosekana kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hadi sasa hatuoni katika document na katika ufafanuzi, mahali popote ambapo ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imehusika katika kushauri na kuyabariki makubaliano haya. Hili pia linavunja katiba na sheria kadhaa za nchi.

7. Kukosekana kwa sahihi ya Katibu Mkuu-Uchukuzi. Sehemu ya sahihi ya Katibu Mkuu-Uchukuzi imesainiwa kwa niaba yake na hadi sasa hakuna ufafanuzi wowote juu ya hilo. Je, kama alikataa? Wenye tamaa wakalazimisha? Kwanini waziri alisaini kwa niaba ya Katibu Mkuu?

8. Tanzania kutakiwa kuijulisha Dubai juu ya uwekezaji mpya katika bandari au maeneo mengine. Hili ni dharau kwa nchi na kuikosesha nchi wawekezaji wapya ambao wangekuja na terms bora kuliko za DPW.

9. Utatuzi wa migogoro unaenda kinyume na sheria ya Natural Resources (permanent sovereignty).

10. Wananchi hatuyataki haya makubaliano. Hili nalo kisidharuliwe. Haya makubaliano yamekataliwa na wananchi.
Umesahahau kwamba pamoja na uwekezaji wa matrillion tuliyokopa katika kuendeleza bandari, DPW watachukua 100% ya faida, kana kwamba bandari wameijenga wao from scratch, kwamba sisi hakuna tulichojenga hapo bandarini?

Pia umesahau kwamba akitaka sehemu yeyote ya ‘territory’ ya Tanganyika, inabidi tufukuze wananchi kwa gharama zetu, na tumpatie bure, na hili halina ukomo!
 
Hayo ni maswali ya darasa la 3 ambayo hayawezi kuulizwa ili kuvutia uwekezaji wa mabilioni. Ni wapuuzi tu wasiojua kazi ya IGA, HGA na nakubaliana ya miradi itakayotekelezwa.
Bandari wanaichukulia kama kukodisha fremu kkoo vile 🤣
 
Kama ni mtego basi mngesema kipengele cha termination kipo Ila kimekaa kimtego kuliko kusema hakuna ...huko ni kupotosha
Boss, usishabikie tu. Nenda kwenye logic.

Mathalani, HGA ya bandari ya Dar port, ikasema ni miaka 10. Mwaka wa 9, DP anaamua kwenda kuwekeza ziwa Nyasa. Mnasaini HGA ya miaka 15. HGA inaanza ya bandari ya Nyasa, wakati HGA ya bandari ya Dar imebakiza mwaka 1 tu. Baada ya mwaka mmoja wa HGA ya Nyasa, HGA ya bandari ya Dar inaisha. Lakini kwa sababu ya HGA ya bandari ya Nyasa, IGA inaendelea. Kwa sababu IGA inaendelea, maana yake ni kwamba, japo HGA ya bandari ya Dar imeisha, IGA inakuzuia kumwingiza mwekezaji mwingine kwenye bandari ya Dar ambayo wakati inakuwa haina mkataba wowote, na pengine baada ya kwisha HGA ya Dar, tungetaka kuendesha wenyewe au kumpa mwekezaji mwingine!! Sijui kama unanielewa.

Huu ni mkataba wa kuitia kitanzi nchi.
 
Una uhakika gani mkataba mdogo utafuata mkataba mama? Na je kama ukitaja vinginevyo tutajikwamua vipi na huku Bunge limeridhia? Unazungumziaje kuhusu mkataba kuamuliwa na sheria za kimataifa? Hili nalo halikupi tatizo? Kuna matokeo mengi mabaya na ya nchi kudhalilishwa na kufilisiwa kwa vipengele kama hivyo.
DP imeenda Djibout, wananchi wameikataa baada ya kugundulika DP iliwahonga viongozi kuukubali mkataba mbaya.

Wamewafukuza DP. Dp imeenda mahakama ya Uingereza, Djibout imeamriwa na mahakama kuilipa DP dola milioni 700. Haya ndiyo yatatokea hapa kwetu.

Pesa walizohongwa viongozi wa serikali, wanahabari na wabunge, zinaenda kuliangamiza taifa la Tanzania.
 
Namaanisha biashara hii itakuwa na teknolojia za kisasa kiasi cha kuongeza pato na kupunguza muda wa bandari kuhudumia meli moja.

TRA inakusanya trilioni 7 kwa sasa, utendaji ukibadilika pale TPA itakusanya trilioni 26, mara tatu zaidi ya hiki kinachopatikana.

Usishangae sana hawa wawekezaji kupigwa vita, ni vita inayotoka kwa mafisadi wa bandarini watu wanaofaidika na huu utendaji wa sasa.
Iko wapi?
 
IGA haina ukomo lakini HGA inayotengenezwa kwa makubaliano kati ya mwekezaji na mzalendo inao ukomo.

Na kumbuka kuwa hawataweza kufanya biashara bila ya kwanza kusajiliwa BRELA, hivyo moja kwa moja watafuata sheria na kanuni za nchi hii.
Hamjui mnachotetea, na wala hamjausoma ule mkataba (IGA) mwanzo mpaka mwisho, mnajiongelea tu.

IGA inajieleza wazi kwenye objectives zake, kwamba the aim of that agreement is to "set a legally binding framework" kwenye maeneo ya operation, management, improvement, na development..

Ndio maana mnaambiwa mwarabu yuko huru kuanza sheghuli zake since October 2022, mpaka hapo, hiyo HGA yenu tayari haina maana, sijui kama someni kitu kizima muelewe, sio kuokota nusu nusu kuja kubisha hapa...
 
Hamjui mnachotetea, na wala hamjausoma ule mkataba (IGA) mwanzo mpaka mwisho, mnajiongelea tu.

IGA inajieleza wazi kwenye objectives zake, kwamba the aim of that agreement is to "set a legally binding framework" kwenye maeneo ya operation, management, improvement, na development..

Ndio maana mnaambiwa mwarabu yuko huru kuanza sheghuli zake since October 2022, mpaka hapo, hiyo HGA yenu tayari haina maana, sijui kama someni kitu kizima muelewe, sio kuokota nusu nusu kuja kubisha hapa...
Hawasomi. Wanaishia kulalamika eti anasalitiwa au anabaguliwa.
 
Back
Top Bottom