Facts kadhaa zinazoufanya Mkataba wa Tanzania na Dubai juu ya Bandari kuwa batili. Tuwe nazo Makini

Facts kadhaa zinazoufanya Mkataba wa Tanzania na Dubai juu ya Bandari kuwa batili. Tuwe nazo Makini

Unaponiambia nitafute mwanasheria ina maana wewe hujui unachoandika hapa, unabisha tu; terms za IGA zinajieleza zenyewe, tatizo wewe hata kuzisoma naamini hujazisoma.

Ningetegemea kama unauelewa wa haya mambo kama unavyodai, wewe ndie uwe wa kwanza kunielewesha, ajabu unaniambia nitafute mwanasheria!.
Terms za IGA hazina nguvu katika utekelezaji wa terms za HGA ambazo zitategemea mikataba mipya ya uwekezaji itakayoandaliwa kwa misingi ya biashara inayofanyika hapa nchini.

Kumbuka kuwa DPW watalazimika kujisajili BRELA na kufuata kila kanuni ya biashara iliyopo nchini. Kufa kwa biashara au kuwa na uhai mrefu kutategemea makubaliano ya HGA.

IGA ni makubaliano ya jumla yaliyopitia bungeni. NI kati ya Tanzania na Dubai. HGA ni makubaliano ya kibiashara kati ya mzalendo na mwekezaji na ndio yenye kuweza kuifanya biashara ikawa na uhai mrefu au mfupi.

IGA na mbwembwe zote zilizowatisha watanzania haina nguvu mbele ya HGA, kufa kwa HGA ndio kifo cha moja kwa moja cha IGA.
 
Huu mkataba una shida na najua Rais Samia amekwisha ukataa ila wapiga debe wanahangaika kuufanya ionekane ni mzuri ili akubali ila yeye ameishaukataa

Mkuu, unahisi? unadhania? Una hakika? ama unatamani iwe hivyo?

-Kaveli-
 
Hakuna hata sheria moja iliyovunjwa. Ni kelele zenye agenda binafsi tu. Nchi hii hata Serikali ikisema kila mtu ajengewe nyumba, lazima kuna kundi litabisha. Cha muhimu Serikali ifanye kama enzi ya Magufuli. Ikiona jambo linafaa, ifanye maamuzi maisha yaendelee.

Kwa maoni yako binafsi, hili la DP WORLD linafaa? ama halifai?

-Kaveli-
 
Usichotwe akili na wapotoshaji .
Termination clause haijasema hivyo..
Lakini wamesema uhai wa IGA uko sambamba na uhai wa HGA ambayo itaweka mda wa mkataba..
Wenzio wanalipwa kupotosha ...

IGA ni moja.

HGA zitakuwa nyingi tofauti tofauti kwa kila mradi kwa mazingira husika.

Inawezekanaje IGA na HGA ziende sambamba kwenye lifetime?

Aidha unapotosha makusudi ama unaongea usichokifahamu.

-Kaveli-
 
H
Habari za asubuhi wana JF,

Tunaendelea na hili jambo ambalo sasa lipo katika ngazi ya familia kabisa. Tunaulizwa majumbani mwetu. Kuna mambo kadhaa ambazo ni facts kabisa katika mkataba huu na zinaufanya ukose sifa.

Wao wanasema ni makubaliano tu, lakini makubaliano ni mkataba. Baadhi ya facts hizo nilizoziona ni hizi zifuatazo:

1. Makubaliano hayana ukomo. Kama ambavyo imeonekana kwa wengi, makubaliano haya hayaonyeshi muda maalum katika umilikishaji wa bandari zote kwa DPW.

2. Umilikishaji wa Bandari zote. Kwanini DPW wapewe bandari zote za Bahari, Mito na Maziwa katika iliyokuwa Tanganyika? Tumezichoka au tamaa ya watawala au kulambishwa asali?

3. Kutohusishwa kwa bandari za upande wa Zanzibar. Hili linasababisha mtanziko wa kikatiba kabisa (Constitutional Crisis). Sheria wanayosema inaipa TPA mamlaka ya upande ya iliyokuwa Tanganyika, imeipa TPA mamlaka ya Tanzania bara na Tanzania Zanzibar katika kifungu cha 2 cha sheria hiyo ya TPA.

4. Hakukuwa na ushindani katika kutafuta mwekezaji. Hiyo inaipa DPW nguvu ya kuinyanyasa na kuifanya kuwa wanyonge serikali ya Tanzania kupitia hiyo timu ya Hamza Johari. Lakini pia ni uvunjaji na ukiukaji wa sheria za nchi juu yw manunuzi ya umma na uwekezaji katika rasilimali asili za nchi.

5. Pesa yenyewe inayotajwa, siyo kiasi cha kuvutia. Hivi leo nchi hii inayokusanya 2+ T kwa mwezi kama mapato ya kodi tu, inawehuka na uwekezaji wa 2T? kiasi cha kuachia bandari zote kwa DPW?

6. Kukosekana kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hadi sasa hatuoni katika document na katika ufafanuzi, mahali popote ambapo ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imehusika katika kushauri na kuyabariki makubaliano haya. Hili pia linavunja katiba na sheria kadhaa za nchi.

7. Kukosekana kwa sahihi ya Katibu Mkuu-Uchukuzi. Sehemu ya sahihi ya Katibu Mkuu-Uchukuzi imesainiwa kwa niaba yake na hadi sasa hakuna ufafanuzi wowote juu ya hilo. Je, kama alikataa? Wenye tamaa wakalazimisha? Kwanini waziri alisaini kwa niaba ya Katibu Mkuu?

8. Tanzania kutakiwa kuijulisha Dubai juu ya uwekezaji mpya katika bandari au maeneo mengine. Hili ni dharau kwa nchi na kuikosesha nchi wawekezaji wapya ambao wangekuja na terms bora kuliko za DPW.

9. Utatuzi wa migogoro unaenda kinyume na sheria ya Natural Resources (permanent sovereignty).

10. Wananchi hatuyataki haya makubaliano. Hili nalo kisidharuliwe. Haya makubaliano yamekataliwa na wananchi.
huna facts zozote zaidi ya fitna na majungu.
 
Point namba 5 inanipa hasira sana ☹️☹️☹️☹️☹️☹️☹️☹️☹️ unatafuta mwekezaji wakati pesa ya uwekezaji unauwezo nayo
 
Think twice. Kuwa na hela pekee sio kigezo cha kuweza kufanya biashara au uwekezaji fulani, nadhani hilo unalijua vema.
 
Point namba 5 inanipa hasira sana ☹️☹️☹️☹️☹️☹️☹️☹️☹️ unatafuta mwekezaji wakati pesa ya uwekezaji unauwezo nayo

Mkuu, labda yawezekana serikali inakosa huo 'uwezo' unaousema? Let alone uwezo wa kumanage kwa standards za kimataifa.

-Kaveli-
 
Think twice. Kuwa na hela pekee sio kigezo cha kuweza kufanya biashara au uwekezaji fulani, nadhani hilo unalijua vema.

Mkuu, kuhusu 'mapungufu' na 'madoa' ya kisheria kwenye hii IGA ambayo wataalam na wabobevu mbali mbali wamekuwa wakiyapazia sauti, nini maoni yako kama mwananchi?

-Kaveli-
 
Mkuu, labda yawezekana serikali inakosa huo 'uwezo' unaousema? Let alone uwezo wa kumanage kwa standards za kimataifa.

-Kaveli-
Mnachagua mkurugenzi wa TPA kwa Sababu ya ukada mnategemea nini. Aliyeiba bilioni kesi inamchakato mia ila aliyeiba kuku miaka 10 jela fasta. Tunachokijenga wallah ni majanga
 
Think twice. Kuwa na hela pekee sio kigezo cha kuweza kufanya biashara au uwekezaji fulani, nadhani hilo unalijua vema.
Uhuni tu wa viongozi Hamna lolote. Uwezo upo ila nafasi za hayo mashirika tunaleana kikada na ki CCM. Hata mkiwapa hao waarabu hata mtakacho vuna mtapigwa tu. Nipe maelekezo kuhusu gesi ilivyobinafsishwa kwanza ndio unieleweshe huu mkataba wa DP. Yaan kwenye gas tayr mshatupiga leo hii mnajisahaulisha alafu mnatuaminisha huu mkataba wa Bandari utakuwa Bora. Aisee
 
Mkuu, labda yawezekana serikali inakosa huo 'uwezo' unaousema? Let alone uwezo wa kumanage kwa standards za kimataifa.

-Kaveli-
Na huo ndio msingi wa kutafuta muwekezaji ambaye anaijua vema biashara ya Bandari na whole logistic chains ya Bandari. Wengi wetu tunadhani biashara ya Bandari sasa hivi ipo kama zamani, kwamba ukiwa na Bandari pekee basi tushamaliza.
 
Uhuni tu wa viongozi Hamna lolote. Uwezo upo ila nafasi za hayo mashirika tunaleana kikada na ki CCM. Hata mkiwapa hao waarabu hata mtakacho vuna mtapigwa tu. Nipe maelekezo kuhusu gesi ilivyobinafsishwa kwanza ndio unieleweshe huu mkataba wa DP. Yaan kwenye gas tayr mshatupiga leo hii mnajisahaulisha alafu mnatuaminisha huu mkataba wa Bandari utakuwa Bora. Aisee
Kwenye gas umepigwaje, usiongee hearsay za mtaani mkuu.
 
Back
Top Bottom