Facts kadhaa zinazoufanya Mkataba wa Tanzania na Dubai juu ya Bandari kuwa batili. Tuwe nazo Makini

Facts kadhaa zinazoufanya Mkataba wa Tanzania na Dubai juu ya Bandari kuwa batili. Tuwe nazo Makini

Umeshaambiwa termination clause ipo, inasema ukomo utafikiwa kuvunja mkataba pale shughuli za bandari zitakapokoma. Labda sijui kama zitakapokauka maji? Au mwisho wa dunia. Ndo hicho kipengele unachosema kiwekwe
Usichotwe akili na wapotoshaji .
Termination clause haijasema hivyo..
Lakini wamesema uhai wa IGA uko sambamba na uhai wa HGA ambayo itaweka mda wa mkataba..
Wenzio wanalipwa kupotosha ...
 
Tumieni akili acheni kulalamika,hao waarabu wakija ndio fursa ya kufunguka biashara za mazao,hao watataka kula
1.Viazi,Ngano,Michele,mihogo,!
Mapapai,ndizi,matunda nk
Kwamba kwa akili za hawa CCM unategemea wewe ndio utanufaika kwa kuwauzia hao viazi 🤣??? Unaonekana ni mgeni wa hili taifa wewe utakuwa Diaspora
 
Usichotwe akili na wapotoshaji .
Termination clause haijasema hivyo..
Lakini wamesema uhai wa IGA uko sambamba na uhai wa HGA ambayo itaweka mda wa mkataba..
Wenzio wanalipwa kupotosha ...
Umesema vizuri, mimi hamna mtu anaenilipa, lakini umejionesha kwamba wewe umetumwa na unalipwa. Tatizo hizo clause mnazosema nyinyi hamuweki hapa ili kulinda hoja zenu. Kama mkataba ukomo wake mpaka shughuli ziishe hii ina maana gani kwa mujibu wa sheria zako uchwara?
 
Ignorance is bliss...
 
Kuna watu wana agenda zao na kwa kawaida watu hao wanakubaliana hata kusema uongo. Sioni kama kelele hizi ni za mkataba, sioni. Ukiwabana wanakwambia "wanasheria nguli wamesoma" au watakwambia "wewe siyo mwanasheria" utadhani watu tunajuana fani humu. Ukiwauliza mnataka mkataba uwe vipi kwenye hayo maeneo mnayoona yana shida, wanahama mada na kumwambia DP World hakushindanishwa, pumbavu.

Lakini pia kama ulivyosrma, hivi wanadhani Dubai ni mjinga?
Ule mkataba wa hovyo una kasoro zaidi ya moja, sio hiyo duration pekee, ambayo hata nyie hamuijui zaidi ya kubuni tu, mnasema labda miaka 25 or whatever!..

Ule mkataba umevunja sheria kibao za hii Tanganyika yetu, usomeni vizuri muuone.
 
Habari za asubuhi wana JF,

Tunaendelea na hili jambo ambalo sasa lipo katika ngazi ya familia kabisa. Tunaulizwa majumbani mwetu. Kuna mambo kadhaa ambazo ni facts kabisa katika mkataba huu na zinaufanya ukose sifa.

Wao wanasema ni makubaliano tu, lakini makubaliano ni mkataba. Baadhi ya facts hizo nilizoziona ni hizi zifuatazo:

1. Makubaliano hayana ukomo. Kama ambavyo imeonekana kwa wengi, makubaliano haya hayaonyeshi muda maalum katika umilikishaji wa bandari zote kwa DPW.

2. Umilikishaji wa Bandari zote. Kwanini DPW wapewe bandari zote za Bahari, Mito na Maziwa katika iliyokuwa Tanganyika? Tumezichoka au tamaa ya watawala au kulambishwa asali?

3. Kutohusishwa kwa bandari za upande wa Zanzibar. Hili linasababisha mtanziko wa kikatiba kabisa (Constitutional Crisis). Sheria wanayosema inaipa TPA mamlaka ya upande ya iliyokuwa Tanganyika, imeipa TPA mamlaka ya Tanzania bara na Tanzania Zanzibar katika kifungu cha 2 cha sheria hiyo ya TPA.

4. Hakukuwa na ushindani katika kutafuta mwekezaji. Hiyo inaipa DPW nguvu ya kuinyanyasa na kuifanya kuwa wanyonge serikali ya Tanzania kupitia hiyo timu ya Hamza Johari. Lakini pia ni uvunjaji na ukiukaji wa sheria za nchi juu yw manunuzi ya umma na uwekezaji katika rasilimali asili za nchi.

5. Pesa yenyewe inayotajwa, siyo kiasi cha kuvutia. Hivi leo nchi hii inayokusanya 2+ T kwa mwezi kama mapato ya kodi tu, inawehuka na uwekezaji wa 2T? kiasi cha kuachia bandari zote kwa DPW?

6. Kukosekana kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hadi sasa hatuoni katika document na katika ufafanuzi, mahali popote ambapo ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imehusika katika kushauri na kuyabariki makubaliano haya. Hili pia linavunja katiba na sheria kadhaa za nchi.

7. Kukosekana kwa sahihi ya Katibu Mkuu-Uchukuzi. Sehemu ya sahihi ya Katibu Mkuu-Uchukuzi imesainiwa kwa niaba yake na hadi sasa hakuna ufafanuzi wowote juu ya hilo. Je, kama alikataa? Wenye tamaa wakalazimisha? Kwanini waziri alisaini kwa niaba ya Katibu Mkuu?

8. Tanzania kutakiwa kuijulisha Dubai juu ya uwekezaji mpya katika bandari au maeneo mengine. Hili ni dharau kwa nchi na kuikosesha nchi wawekezaji wapya ambao wangekuja na terms bora kuliko za DPW.

9. Utatuzi wa migogoro unaenda kinyume na sheria ya Natural Resources (permanent sovereignty).

10. Wananchi hatuyataki haya makubaliano. Hili nalo kisidharuliwe. Haya makubaliano yamekataliwa na wananchi.
Unapoteza muda kuja na orodha ndefu ya mambo ambayo yameshatolewa ufafanuzi.

Wapigaji hapo bandarini siku zao zinahesabika. Hizi juhudi za kuja na mada ni sawa na mtu anayekaribia kufa jinsi anavyopaparika wakati roho inatoka.
 
Umeshaambiwa termination clause ipo, inasema ukomo utafikiwa kuvunja mkataba pale shughuli za bandari zitakapokoma. Labda sijui kama zitakapokauka maji? Au mwisho wa dunia. Ndo hicho kipengele unachosema kiwekwe
Mjinga haelewi hata hiki!.
 
Ule mkataba wa hovyo una kasoro zaidi ya moja, sio hiyo duration pekee, ambayo hata nyie hamuijui zaidi ya kubuni tu, mnasema labda miaka 25 or whatever!..

Ule mkataba umevunja sheria kibao za hii Tanganyika yetu, usomeni vizuri muuone.
TICTS wamekaa miaka 22, mkataba wao haukuwa na ukomo kama huu wa DPW?.
 
Umesema vizuri, mimi hamna mtu anaenilipa, lakini umejionesha kwamba wewe umetumwa na unalipwa. Tatizo hizo clause mnazosema nyinyi hamuweki hapa ili kulinda hoja zenu. Kama mkataba ukomo wake mpaka shughuli ziishe hii ina maana gani kwa mujibu wa sheria zako uchwara?
Huyo ni dini tu, nothing else.
 
Ndio umeandika nini hapa? Miaka 32 kwako sio ukomo?!

DPW hauna ukomo, coz shughuli za bandaruni haziwezi kwisha.
IGA haina ukomo lakini HGA inayotengenezwa kwa makubaliano kati ya mwekezaji na mzalendo inao ukomo.

Na kumbuka kuwa hawataweza kufanya biashara bila ya kwanza kusajiliwa BRELA, hivyo moja kwa moja watafuata sheria na kanuni za nchi hii.
 
sina.ndugu.anayefanya kazi.bandarini kwamba DP wakija atakosa ajira ila kwa uzalendo wangu Samia aachane.na.huu.ujinga.Wa
DP
 
Uelewa wako mdogo, hauwezi kuwa na access na HGA bila ya kwanza kuwepo makubaliano ya kibiashara kati ya pande mbili, muwekezaji na mzalendo.
Hujanielewa. Nachomaanisha, hakuna siku HGA itawekwa public. Sisi umma tunaweza kusoma IGA, au BITs tu.

Ndio maana tunataka hii IGA ikae sawa, huko kwenye HGA, wanasaini tu hata wakiwa mahotelini marekani. Watajua wenyewe
 
Hawana chakula kwao ni jangwa,Hakuoti kitu chochote wala kufuga chochote,zaidi ya ngamia,hawana
1.Kuku
2.Ng'ombe
3.Mbuzi.
4.kondoo
5Viazi,ndizi,Michele,matunda,nk
Badala sisi kuanzisha njia za kibiashara kunufaika kwao,twapoteza wakati bure,!nafasi hiyo ya vyakula akichukuwa wa nchi nyingine tutakuja lalamika.Hapo Zanzibar kuna soko kubwa la vyakula na mifugo na matunda,kutokana na mahotel ya kitalii,fursa hatuzitumii.
Kuna visiwa vya Ngazija,Mauritius,Madagascar,!fursa za vyakula kuuza kule,na mifugo,hatutumii.
Kama hivi sasa mbuzi amefika mpaka 170000,ng'ombe mpaka mamilioni,kwa ajili ya sikukuu ya Eid,dini inawahimiza watoe sadaka ya nyama!,bado visima watachimba vya maji.kusaidia kwenye matatizo ya maji,maana dini ya uislamu imehimiza kutoa sadaka ya maji,sisi tumekaa kubishana yasio na faida.Ukiwa na mbuzi 20 si tayari una 36milioni.Bado ng'ombe
Ukiwa nao 20,hujainuka kiuchumi.Na hapo bado waarabu hawajaanza Bandarini.Hawa waislamu waacheni waje,watuinue kiuchumi,siku kuu zao zote na siku za kawaida ni neema.Bado kipindi cha sikukuu ya mwezi wa Ramadani,wananua Michele kwa wingi,kwa kutoa sadaka.Bado hatujagusia wavuvi wa samaki,hawa ni walaji sana wa samaki,kwa wavuvi ni fursa hiyo.
Wakulima na wafugaji,kwa ujio wa hawa waarabu waislamu ni neema kwao.
Uwape bandari bure, uwauzie mahindi na mchele, ...

Kweli wewe ni mangungo promax..
 
Hujanielewa. Nachomaanisha, hakuna siku HGA itawekwa public. Sisi umma tunaweza kusoma IGA, au BITs tu.

Ndio maana tunataka hii IGA ikae sawa, huko kwenye HGA, wanasaini tu hata wakiwa mahotelini marekani. Watajua wenyewe
IGA imetengenezwa kwa ushirikiano kati ya wanasheria wa Tanzania na wale wa Dubai kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita.

Hawa ni wabobezi wa sheria. Kwa upande wa Tanzania ni Dr Possi na Hamza hawa licha ya kusomea sheria pia ni waalimu wa vyuo vikuu ngazi ya masters.

Upande wa DPW pia unao wataalam ambao sio waarabu wa pale ni waajiriwa tu wanaowakilisha kampuni hiyo na wao ni wataalam waliobobea katika sheria.

Watanzania kila kitu tunajifanya tunakijua, kila mahali tunao wepesi wa kukosoa, wepesi wa kutoa mapendekezo, huwa tunachekesha sana na huu ujuaji wetu.

Kwamba mtu mmoja tu humu JF anaandika akikosoa IGA yaani kama vile anajua analoliongea kumbe ni upuuzi mtupu mbele ya mwanasheria mbobezi. Hizi mada za sheria sio sawa na zile za Yanga na Simba kwamba kila mtu anaweza tu kuzielewa na kuzikosoa.
 
Uwape bandari bure, uwauzie mahindi na mchele, ...

Kweli wewe ni mangungo promax..
Akili za kiduwanzi ndio hizi. Nani anayetoa bandari bure?. Fanya utafiti ujue ni kiasi gani cha pesa serikali inakwenda kuingiza kwa mwaka mmoja tu wa mkataba na DPW.
 
Back
Top Bottom