Lucas philipo
JF-Expert Member
- Sep 1, 2017
- 2,039
- 2,676
Hahaha kuna watu mna akili hadi mnatamanisha!Paleomammalian Cortex (Limbic System)
Rudisha[emoji1489][emoji1489][emoji1489] kwa Kiswahili ili tuelewe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaha kuna watu mna akili hadi mnatamanisha!Paleomammalian Cortex (Limbic System)
Rudisha[emoji1489][emoji1489][emoji1489] kwa Kiswahili ili tuelewe
Hahaha kuna watu mna akili hadi mnatamanisha!
Karibu Mkwe wangu.Ahsante sana mama mkwe...Kwa neema zake Allah.
Namuandalia mwanao
Wuuuuu nilijua nikakitu kama maneno mawili,
Mwajuma njoo, nakupenda
Tayar anakubali.
Jamani Vers Kweli?Wanitamanisha...✌✌✌✌
Kwanini?
Kuna vitu hajaandika chunguza mtu huyo Kama yupo single ndo ufanye hayo ila Kama anamtu jua unatakiwa ujue udhaifu wa kwenye mapenzi aliyopo sasa ili wewe uitekeleze umroe Kama sangara,kumbuka hakuna Vita isiyo na mbinu.mkuu umeongea vema sana yote kwa yote ni ili kufanikisha dhamira iliyokusudiwa na mhusika.mkuu kuna kabinti nmetumia njia hzo.ulizoziorodhesha hapo juu lakini hazijatenda hisani zozote kwangu zaidi ya maumivu tu.mkuu.unaweza hisani ukafanikisha kusudi ila baada ya muda everthing change
Nitapingana nawe hapo kwenye humbleness!! Baadhi ya mambo kuna wanawake mkuu wanapenda mtu anaejikweza hii huwapa Hali ya kutaka kukujua vizuri na huo ndio mwanya wa kumtanua!!, Wewe uliowasema hapa Ni wale wapole ndio haswa hupenda watu wasiojikweza!!..Salute
Around mwaka 2017 mkuu Rakims alileta uzi unaoitwa “Jinsi ya kumuita mtu jua linapozama na linapo
chomoza “ mimi kama mchangiaji wa kawaida nilielezea jinsi mimi navyofahamu kuhusina na kumwita mtu unayempenda au kumfanya mtu unayempenda akupenda..It was some magical stuffs and spells
based… Im not witchcraft sorcerer but I know how to do and manipulate some magical spells but I don’t
practice them.
Mambo yote niliyoelezea kwenye uzi huo ni kweli na yanafanya kazi, waweza mpata yoyote umtakaye lakini njia ya mkato hua ina madhara au kila kitu hua na hasara zake so katika mambo hayo ni kweli unaweza mpata yoyote lakini kumbuka Yule mtu uliyempata unakua umempata kwa njia isiyo
halali..Dawa na mambo yale unayomfanyia yanaenda kumfunga akili muhusika unakua unamfanya utakavyo kiufupi unakua umemtia kama uzezeta Fulani au kama msukule Fulani. Mwisho wake ipo siku
mtu huyo atatoka kwenye kifungo hiko. Then you can guess the quencequences
Toka kipindi hiko nimekua napokea jumbe mbalimbali watu wakiulizia kama tunaweza fanya kitu, Upande wangu nakua nashindwa kuwasaidia kwakua sipendi kujihusisha na mambo haya ya giza nataka yabaki kama experience tu ya viti navyofahamu maishani. Basi mimi nilipenda leo tujadiliane njia mbalimbali zinazoweza kutupatia mpenzi uliyekua unampenda na unatamani siku moja awe wako wa
maisha..Nitatumia Psychological Manipulation, jinsi ya kumpata umpendae kwa kumteka kihisia na kiakili.
Kwanza kabisa ili uweze tengeneza computer inakubidi uelewe jinsi mifumo na vifaa vyote vilivyomo ndani ya Computer na jinsi vinavyofanya kazi..Chukulia mwili wa binaadamu ni Computer nzima, ubongo ni Processor,Monitor (kioo) ni Moyo. So inakua hivi unapomuona mtu unayempenda moyo hudunda haraka haraka mwili unajaa uoga pengine hua mtu anatoka hadi jasho usoni , hii inafanya watu wengi
tunaamini kua Upendo/Mapenzi yanatoka au yanakaa moyoni. Jibu ni NOOOO! Mapenzi hayakai moyoni wala hayatoki moyoni, moyo hauhusiani kabisa nawewe kumpenda mtu, moyo hua unafanya kazi ya kusukuma damu tu! Pia unatoa output ya Upendo.
Ubongo umegawanyika katika maeneo mbalimbali , ndani ya ubongo kuna sehemu inayoitwa
Paleomammalian Cortex (Limbic System) hii ndio sehemu ya ubongo inayohusika nma kupenda mtu, unapomuona mtu yoyote unayempenda hii sehemu ya ubongo inatoa chemicals mbazo zinapelekea moyo kwenda kasi, halafu unasikia moyo unampenda sana huyo mtu lakini ukweli huo upendo upo kwenye ubongo. Hizo hisia unazisikia kwenye moyo sababu kuna Nerve mbalimbali ndani ya moyo ambazo huhisi maumivu ua hali yoyote kutokana na jinsi ubongo ulivyoamua moyo uhisi…
Emotions zinakaa ndani ya Akili (Mind, kumbuka mind ipo ndani ya Ubongo) hivyo basi kupitia Limbic system Love
Emotions hutafsiriwa na kutolewa huko kwenye Moyo kama output Device.
NB. Mambo haya nitakyoelezea hapa yanaweza kufanywa na mtu wa jinsia yoyote, ila nimeegemea kwa jinsi ya kumpata mwanamke kwakua mwanamke ndio tamaduni yake kiafrika kutafutwa na mwanaume.
Je nifanyeje ili kumpata nimpendae…?
Ili kumpata mtu unayempenda baada ya kujua kua hisia za mapenzi ya mtu zinakaa kwenye Mind inabidi
ucheze na Mind ya muhusika na ukiweza kufanya hivyo nakuhakikishia utampata yoyote umtakae.
Unachotakiwa kufanya ni kua mvumilivu maana mazuri hua yankuja polepole ukiwa umayatolea jasho.
Yafuatayo ni mambo makuu matatu ambayo ukiyafanya una uwezo wa kumpata hata Beyonce kama una
ukaribu nae..
Hapa tunaweza kusema kua ni mtu kua mwema na kufanya matendo ya wema na huruma, matendo hayo yanaweza kua Uaminifu,Loyality,Heshima,Kua Romantic nk. Kama unampenda mwanamke Fulani
- Kindness (Wema)
tafuta kila njia uwe karibu nae, jua anavyopendelea na matatizo aliyonayo. Ukishamfahamu anza kumfanyia matendo ya wema kama Kumjulia hali, kusimama nae katika shida alizonazo, mtembelee, mtoe out, fanya kila kitu kuonyesha jinsi gani unavyomjali ,unamthamini, unamlinda,unamheshimu,nk.
mind ya kila binaadamu imewekea Wema, so Unapomfanyia mtu matendo ya wema unakua unaivuta
mind yake kujenga na attention kwenye mind yako.
Baada ya kua unamfanyia matendo ya wema mwanamke mind inaanza kutengeneza Emotions juu yako
kwakua unakua umekua umeigusa kwa kufanya vitu ambavyo Mind imeumbiwa kufanya na kufanyiwa.
Baadae zile emotions zitakua zinatolewa kutoka kwenye Mind na kupelekwa kwenye ile sehemu ya ubongo inayoitwa limbic system kisha moyo utakua unatoa outup sasa juu yako jinsi Mind inavyokufeel.
Ndio pale sasa ukimfanyia kitu Fulani anahuzunika pengine anaweza hata kulia kutokana na jinsi jinsi gani matendo yako yanvyogusa mind yake. Mwisho utakua ume win moyo wake kama tulivyozoea kusema lakini kiuhalisia ni Mind yake ndio unakua umeu-win. Utakua umejipatia mpenzi wa ndoto zako.
Hii njia inaweza kua ndefu, yenye vikwazo na yenye kukatisha tama, so itumie hii njia kwa Yule ambae
unayeona ndio wako wa maisha kama akikubalia ila kama unataka ku hit and run hii njia utaona ni
usumbufu na mzunguko mkubwa. Pia kuna vitu baadhi unaweza kuvitumia wakati unatekeleza hio njia,
vitakusaidia kuongeza point 3 muhimu katika kumteka moyo/akili mrembo huyo umtakae. Vitu hivyo ni..
Kua mtu usiye na makuu, hujikwezi,msikivu nk. Wanawake wanapenda watu ambao hawana makuu, sio
- Humbleness
wabishi bishi kwa kila kitu, sio mr misifa. Humbleness ni bure kabisa waweza kuimudu bila kutumia
ghalama yoyote ile, Heshimu mwenzako hisia na mawazo yake. Akikuambia sitaki kutoka leo
usilazimishe, muda mwingine inabidi ujifanye mjinga ili uweze kutimiza malengo yako.
Kua smart kichwani sio kila muda wewe mdomo wako unafyatua maneno yasiyo na staha au ya kihuni..Play smart and wise. Unaweza kua smart kichwani ila huna hekima, ukiwa na smart kua wise
- Be smart
katika vitendo na maongezi yako. Trust me ladies wengi wanapenda mno Man ambaye yupo vizurii kichwani akichambua kitu anakichambua . Jitambue kama mwanaume smart ambae unaweza
kumwongoza mwanamke pamoja na watoto mtakaowapata kama ikitokea mmeingia ndani ya ndoa! Kua
smart kichwani utapendwa na kila mwanamke.
NB. Katika maansishi yangu nimetaja Mwanaume sio Boy na mwanamke sio girl nikimaanisha kua njia hi itumiwe na watu wenye commitment na ndoa sio wanaotaka kufanya ngono na kuondoka. Kama utakua
unamuhitaji mtu kwa ajili ya ndoa hii njia itakua rahisi na utaweza kuvumilia usumbufu utakai upata si
unajua mambo mazuri huchelewa ili kukupima uwezo wako wa kuvumilia.
All the best MEN.
The End…
~Da’Vinci.
El maestro.
Ahsante kwa maelezo yako.. Shida sometimes ni ngumu kujua wanawake wanataka nini..Nitapingana nawe hapo kwenye humbleness!! Baadhi ya mambo kuna wanawake mkuu wanapenda mtu anaejikweza hii huwapa Hali ya kutaka kukujua vizuri na huo ndio mwanya wa kumtanua!!, Wewe uliowasema hapa Ni wale wapole ndio haswa hupenda watu wasiojikweza!!..
Kaa ukijua watu wanatofautiana ila unatakiwa kujua tofauti zao chunguza utaelewa!.. wanawake hupenda maneno sana na hapa ndipo karata yako unaweza itumia kisawasawa
Ni ngumu kujua wanataka nini ila Ni virahisi kujua anataka Nini!! Ukiwakombini wote watakuchanganya ila mmojammoja utajua tu anataka nini .. tatizo nililonalo juu ya wanawake Ni ktk kuwaamini😜Ahsante kwa maelezo yako.. Shida sometimes ni ngumu kujua wanawake wanataka nini..