DOMINGO THOMAS

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2023
Posts
365
Reaction score
365
Je, wajua mnufaikwa wa Fao la Uzee (Old Age Pension) akishachukua kiinua mgongo na kuanza kulipwa monthly pension (Malipo ya kila mwezi) na baada ya miezi miwili/mitatu+ akafariki, Dependant wake wanakuwa hawana kitu cha kwenda kudai kwenye Mfuko?

Kwa PSSSF tegemezi watakuwa hawana kitu cha kwenda kudai kwenye mfuko (hawana kitu cha kulipwa)

Kwa NSSF watalipwa Death Benefits tu (Fao la Kifo)
 
Hii mifuko ina ujanja ujanja sana


Mtu kachangia mfuko kwa miaka 40.

Anastaafu akiwa na miaka 60. Ile anaanza kupokea pensheni tu anafariki baada ya mwezi mmoja

Mke na watoto wake hawaambulii chochote kutoka kwenye michango ya baba yao ya miaka 40
 
Kwani hawezi kuchukua zote kwa mkupuo? Badala ya kulipwa kila mwezi. Je, ni hiari ya mtu au lazima?
Ndivyo malipo ya Pension ya livyo.. Mnufaika analipwa mara mbili, awamu ya kwanza ni mkupuo na yapili ni malipo ya kila mwezi.!
 
Sio wezi ni sheria zilizojadiliwa na bunge letu na kupitishwa kwa kura nyingi za ndiyooooooo!
 
Yes, Ndivyo sheria ilivyo.
 
Vibaka wakubwa hawa yaani nimeyashuhudia haya. Mwingine anakufa amebakisha mwezi mmoja astaafu lakini kupata stahiki zake sasa dooh!
Umeshuudia kwanani..!? Kama warithi wake wapo wanayo haki ya kwenda kudai fao la URITHI
 
Wanajeshi familia inalipwa pension ya mwaka mmoja halafu basi . Sijui kwann wasifanye hivi kwenye kila sekta.
 
Mbona hamsemi mme na watoto ??

Mmezidi uchuro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…