Fahamu hili kuhusu Fao la Urithi/Mirathi
Uliwahi kwenda kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii (PSSSF/NSSF) kudai Mafao yako?

Je, ni changamoto gani ulipitia?
 
Nikikwambia unawajua? na kwa nini wasote na wakati ni haki yao ile! umeshakutana na haya ktk familia yako?
Unaweza Eleza sababu inayo wakwamisha kupata hilo fao..!?
Kwenye Mafao hakuna Fao gumu kulipata kama fao la URITHI/MIRATHI wengi huwa wanashindwa kulipata kwa kukosa kupeleka document muhimu zinazo itajika.
 
Hii sheria si aliitunga shujaa kwa madai ya kwamba wastaafu wanakula pesa zinapotea kumbe nia yake azuie ondokeo la fedha pale apeleke kwenye miradi uchwara
 
Hii mifuko ina ujanja ujanja sana


Mtu kachangia mfuko kwa miaka 40.

Anastaafu akiwa na miaka 60. Ile anaanza kupokea pensheni tu anafariki baada ya mwezi mmoja

Mke na watoto wake hawaambulii chochote kutoka kwenye michango ya baba yao ya miaka 40
Hii ni kwa hiki kikokotoo cha sasa labda ila kile cha kabla ya 2023 ni tofauti
 
Unaweza Eleza sababu inayo wakwamisha kupata hilo fao..!?
Kwenye Mafao hakuna Fao gumu kulipata kama fao la URITHI/MIRATHI wengi huwa wanashindwa kulipata kwa kukosa kupeleka document muhimu zinazo itajika.
Wizi unadhihirika pale unapoambiwa upeleke documents tena na tena na tena!
Ishara nyingine ni kwamba zikibaki kwao wanazikwapua!
 
Hii ni kwa hiki kikokotoo cha sasa labda ila kile cha kabla ya 2023 ni tofauti
Kikokotoo cha sasa kimebadili namna ya malipo ya pension tu! Ambapo zamani mnufaika wa pension alikuwa anapata asilimia 25 kiinua Mgongo na Asilimia 75 Malipo ya kila mwezi.

Kwasasa ni asilimia 33% kwenye kiinua Mgongo na Asilimia 67% kwenye malipo ya kila mwezi.. Na hii sheria imeanza kutumia July 2022
 
sheria imebadilishwa 2018 hujui kwamba zamani watu walikua wanapewa pesa zao zote?
Umesahau jina la kikokotoo lilianzia lini?
Hakuna mtu aliye wai kupewa mafao yake yote kwa mkupuo..!!

2018 ndipo LAPF, PPF,GEPF na PSPF ziliungana na kuunda PSSSF hii nikwa watumishi wa serikali na NSSF kwa Sekta binafsi.. Na wakaanza kutumia njia moja ya kikokotoo...

Kabla ya kuungana kila Mfuko ulikuwa na njia yake ya malipo, lakini hakuna mfuko ulikuwa unalipa mwanachama kwa Mkupuo/Mafao yake yote kwa wakati mmoja.
 
Back
Top Bottom