- Mtu akiacha kazi mwenyewe, hato lipwa fao la kukosa ajira (Hakuna fao atakalolipwa)

- Fao La kukosa ajira (Unemployment benefits linalipwa kwa mtu ambaye mkataba wake wa kazi umefika ukomo, au amefukuzwa kazi).
Samahani, ni sheria ipi inayotumika kwa wasio na vyeti ila wamepoteza aijra kwa kufukuzwa
 
Mstaafu aliye staafu baada ya kikokotoo kipya kuanza kutumika July 2022 ( Ambaye mafao yake yalitumia kikokotoo kipya ) huyu akifariki dependant wake watalipwa Mara 36 ya kile alicho kuwa anakipata kwa mwezi.
 
Kikokotoo kinacho-tumika kukokotoa mafao ya uzee, ndio hichohicho hutumika kukokotoa mafao ya mirathi na ulemavu wa muda mrefu.
 
Vitu viwili vinanafanya pensheni ya uzee kuwa kubwa au ndogo ni:-
1. Kiwango cha Mshaara.
2. Miezi ya uchangiaji katika mfuko.
 
Ukiacha kazi mwenyewe, hutolipwa fao la kukosa ajira. Fao la kukosa Ajira ni kwa wale tu walio fukuzwa kazi, ajira kufika ukomo au kampuni imefungwa.
 
Fao la Uzazi hulipwa kwa Mama aliye jifungua ( iwe mtoto kafariki au yuko hai ) na kachangia kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii kwa kipindi cha miezi 36 au Miaka Mitatu.
 
Mstaafu baada ya kuanza kupokea malipo ya kila mwezi, anatakiwa kujihakiki kama yuko hai kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii, kila mwaka ili aendelee kupata malipo hayo, asipo fanya hivyo malipo hayo yatasimama.
 
Mishaara inayo chukuliwa kwenye kukokotoa pensheni ya uzee ni β€œMshahara wa kukokotoa mafao ya pensheni ni wastani wa mishahara bora ya miaka mitatu (3) ndani ya miaka 10 kabla ya kustaafu”
 
1/580 kwenye kikokotoo cha pensheni ya uzee inajulikana kama Kikokotoo limbikizi na 12.5 inamaana ya Makadirio ya miaka ya kuishi baada ya kustaafu
 
Hiki kikokotoo kipya kitumike pia kwenye kukokotoa mafao ya wabunge, spika, waziri mkuu, na pia Rais wa nchi. Na kisitumike kwa wafanyakazi wa ngazi za chini pekee.
 
Nani anatakiwa kufuatlia michango yako? Shirika ndio wajibu wake huo. Na lilishaongelewa bungeni kuwa si jukumu la mwanachama. Unakuta Shirika halijapeleka michango miaka kibao na wanajua lakini wamekaa tu maofisini kula hela za mfuko. Mbona TRA wanafuatilia kodi ? Kwa nini wao washindwe?
 
Sasa akilipwa 67% ikaisha halipwi tena?
 
Malipo ni 33% kwa malipo ya awari ( Kiinua Mgongo ) na Asilimia 67β„… Malipo ya kila mwezi, Ambayo atalipwa kila mwezi mpaka atakapo fariki.
 
HUO URONGO BWANA
 
Mstaafu aliye staafu baada ya kikokotoo kipya kuanza kutumika July 2022 ( Ambaye mafao yake yalitumia kikokotoo kipya ) huyu akifariki dependant wake watalipwa Mara 36 ya kile alicho kuwa anakipata kwa mwezi.
tufahamishe vizuri hao wategemezi wanatakiwa kuwa na umri gani ili walipwe huo urithi. maana nina jamaa yangu anaangaika kufuatilia mafao ya baba yake ambaye ashafariki wanamzungusha kila kukicha
 
tufahamishe vizuri hao wategemezi wanatakiwa kuwa na umri gani ili walipwe huo urithi. maana nina jamaa yangu anaangaika kufuatilia mafao ya baba yake ambaye ashafariki wanamzungusha kila kukicha
Tegemezi wanao tambulika kisheria ni Mjane au Mgane, pamoja na watoto ambao wako chini ya umri wa miaka 21
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…