Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

BREAKING: Idadi ya waliokufa kutokana na virusi vya Corona yafikia 635.

Idadi ya vifo 618 ni katika mkoa wa Hubei pekee nchini China, mkoa ambao umeripoti vifo vipya 69.
 
UPDATE: Idadi ya visa vipya vilivyoripotiwa katika mkoa wa Hubei ni 2,447 huku jumla ya visa vyote vikifikia 22,112 katika mkoa huo pekee.
 
Nahisi nina huu ugonjwa maana nasikia pua la kulia halina hali.. hafu nasikia harufu ya dumu ndani ya pua
 
Miongoni mwa vifo vilivyoripotiwa katika siku ya Alhamisi ni pamoja na kifo cha Daktari wa Kichina, Li Wenliang. Daktari aliyejaribu kutoa taarifa ya mapema zaidi kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Coronavirus mwezi Desemba mwaka jana.

Hospitali iliyokuwa ikimpatia matibabu imethibitisha kifo chake.

Taarifa kuhusu kifo cha Daktari huyu zimeenea katika mitandao mbalimbali ya habari na ya kijamii.

Li Wenliang aliambukizwa virusi hivyo wakati akifanya kazi katika Hospitali kuu ya mjini Wuhan.

Alituma taarifa ya tahadhari kwa madaktari wenzake mnamo Desemba 30 lakini alipewa onyo na polisi kuacha kutoa "taarifa za uongo".

1581033614401.png

1581032142245.png
 
UPDATE: Mtoto wa siku moja aambukizwa virusi vya corona.

Mtoto mchanga nchini China ameambukizwa virusi vya corona saa 30 baada ya kuzaliwa, kisa chenye kuhusisha mtoto mchanga zaidi kuwahi kurekodiwa, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Mtoto alizaliwa tarehe 2 mwezi Februari katika hospitali moja ya mjini Wuhan, ulio kitovu cha mlipuko wa virusi hivyo.

Mama wa mtoto alikutwa na virusi hivyo kabla ya kujifungua. Haijulikani ni kwa namna gani kichanga hicho kiliambukizwa.

Shirika la habari la China, Xinhua limeripoti taarifa za maambukizi siku ya Jumatano.

Ilieleza kuwa mtoto aliyekuwa na uzito kilogramu 3.25, alikuwa na hali nzuri na alikuwa akifanyiwa uchunguzi.

[BBC]
 
Here are five precautions you and your family can take to avoid infection:
  1. Wash your hands frequently using soap and water or an alcohol-based hand rub.
  2. Cover your mouth and nose when coughing or sneezing.
  3. Avoid close contact with anyone who has cold or flu-like symptoms.
  4. Go to the doctor if you have a fever, cough or feel that it is difficult to breathe.
  5. Avoid direct unprotected contact with live animals and surfaces in contact with animals.
[UNICEF]
 
UPDATE: CORONAVIRUS
  • 30,811 confirmed cases worldwide
  • 24,702 suspected cases
  • 635 fatalities
  • 4,664 in serious/critical condition
  • 1,337 recovered
  • Most cases in China
  • 25 countries reporting cases

More updates to come!
 
UPDATE: China imetangaza ongezeko la vifo vingine vitatu (3) hivyo idadi ya jumla kufikia 638.
 
UPDATE: China imethibitisha vifo 73 pamoja na visa vipya 3,143 kwa siku ya Alhamisi. Vifo vipya 69 pamoja na visa vipya 2,447 ni katika mkoa wa Hubei pekee.

1581040561381.png
 
UPDATE: Kuhusu meli ya Diamond Princess iliyowekwa karantini nchini Japan.

Watu wengine 41 wamethibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona hivyo mpaka sasa jumla ya watu 61 waliokuwa katika meli hiyo wamebainika kuwa na maambukizi.

1581041646410.png
 
UPDATE: Nationalities of 61 people with Coronavirus on Diamond Princess cruise ship near Tokyo:
  • 28 Japanese
  • 11 American
  • 7 Australian
  • 7 Canadian
  • 3 Chinese
  • 1 New Zealand
  • 1 Taiwan
  • 1 Philippines
  • 1 Argentina
  • 1 UK

More updates to follow!
 
Baada ya visa vipya kubainika katika meli ya Princess Diamond, Japan sasa inakuwa nchi ya pili yenye visa vingi zaidi duniani vya virusi hivyo baada ya China.

Japan ina jumla ya visa 86 mpaka sasa na bado vipimo vinaendelea kufanyika kwa abiria waliokuwemo katika meli hiyo.
 
Mataifa yaliyokwisha anza kuwaondoa raia wake kutoka Wuhan nchini China;
  • Marekani
  • Japan

Mataifa mengine yaliyothibitisha mpango wa kuwaondoa raia wake kutoka eneo hilo;
  • Australia
  • New Zealand
  • India
  • Korea Kusini
  • Ufaransa
  • Uingereza
  • Uturuki
Kumbe kanjibai naye yuko vizuri... Afrika tunakwama wapi?!!!
 
UPDATE: Rais wa Marekani Donald Trump amezungumza kwa simu na Rais wa China Xi Jinping.

Katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Trump ameandika haya;

"Nilikuwa na mazungumzo marefu na mazuri kwa simu na Rais Xi wa Uchina. Yeye ni hodari, shupavu na mwenye bidii katika malengo ya kukabiliana na virusi vya Corona. Anahisi wanafanya vizuri sana, hata kujenga hospitali katika siku chache tu. Hakuna kitu ambacho ni rahisi, lakini ...

... atafanikiwa, haswa wakati hali ya hewa inapoanza kuwa ya joto natumai virusi vitakuwa dhaifu, kisha kupotea. Nidhamu kubwa inafanyika nchini China, kwa vile Rais Xi anaongoza kwa ushupavu kazi itakayofanikiwa. Tunafanya kazi kwa ukaribu na China ili kusaidia!"


1581077539526.png

1581077624125.png
 
Back
Top Bottom