Habari wakuu,nawasalimu kwa jina la corona.
Natumaini hadi sasa hamna member wa JF humu anaeshukiwa kuwa na huyu mdudu wa corona.
Natamani kujua huyu corona akiingia katika mwili wa mzungu inasemekana hachelewi kuonesha sign, hazizidi siku 14.
Vipi kuhusu Wahadzabe na Wasukuma weusi kwasababu inasemekana tunakinga mara dufu katika kupambana na magonjwa tofauti tofauti.
Je, huyu virus hawezi kuwa ndani ya mbongo ila akawa ametulia tu may be mwezi mzima anadunda tu mwisho wa siku baada ya muda tunakuja ugua kwa pamoja?
Kama China ni marafiki zetu basi watupe hata vipimo viwili witatu tupate kuvitumia kupima watu ambao wamekutana na watu waliotoka ktk nchi zenye mlipuko, wasindikiza watalii, n.k
Licha ya hivyo, kuna watu wenye mafua ya kawaida, na kikohozi ambacho koo linakauka na kuwasha, pamoja na kichwa kuuma kwa sana. Naona hao wangepatiwa huduma ya kwanza kama dawa zipo alafu tuone, je inakuaje?
Watu tumekua waoga kana kwamba ndo ugonjwa pekee unao sababisha kifo, kwa hali tulionayo kwa sasa duniani kinaweza pitishwa kitu chochote, chanjo itakayo tolewa itakua world wide hapo kinaweza pitishwa kitu chochote.
Cha muhimu ni kujilinda wewe na familia yako sio kwa corona tu na magonjwa mengineyo.